settings icon
share icon
Swali

Je! Watoto watanyakuliwa katika unyakuzi?

Jibu


Biblia haisemi hasa kile kitafanyika kwa watoto wadogo na wachanga wakati unyakuzi utatokea. Hii inawafanya Wakristo wengi kuwa na hofu kwamba ikiwa watachukuliwa katika unyakuzi na watoto wao watabaki nyuma kukabiliana na dhiki. Je! Hii inawezekana? La, hatuamini kuwa itawezekana. Tunapoelezea mtazamo wetu, tafadhali elewa kuwa ni dhanio bora. Tena, Biblia haizungumzii swala hili.

Ni mtazamo wetu kwamba watoto walio chini ya umri wa uwajibikaji watachukuliwa katika unyakuo. Ikiwa mtoto hajafikia hatua kwamba anaweza kufanya uamuzi kumfuata Kristo au dhidi ya Kristo, tunashikilia kwamba ikiwa atakufa, ataruhusiwa kuingia mbinguni. Tunashikilia pia kwamba kanuni hii, inategemea kabisa rehema za Mungu, itatumika kwa unyakuo. Wengine wanapendekeza kwamba ni watoto wa waumini tu ndio watanyakuliwa. Hatukubaliani. Ikiwa wokovu wa mtoto akiwa chini ya umri wa uwajibikaji hautegemei hali ya imani ya wazazi wake, vile vile mtoto hatashiriki kukombolewa wakati wa unyakuo. Ni imani yetu, ingawa haijafundishwa wazi katika Maandiko, kwamba wale wote walio chini ya umri wa uwajibikaji watachukuliwa katika unyakuo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Watoto watanyakuliwa katika unyakuzi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries