settings icon
share icon

Utafiti wa Biblia

Muhtasari mzuri / utafiti wa Biblia ni vigumu kuufikia. Biblia ina maagano mawili, vitabu 66 tofauti, sura 1189, mistari 31173, na maneno 773,692. Vitabu mbalimbali vya Biblia vinaguzia mada mbalimbali na vilikusudiwa kwa watu tofauti tofauti. Vitabu vya Biblia viliandikwa na takriban watu 40 mbalimbali kwa kipindi cha takriban miaka 1500. Muhtasari / utafiti wa Biblia nzima basi ni kazi/shughuli kubwa.

Wakati huo huo, Roho Mtakatifu alikuwa "msukumo" mwandishi wa Biblia. Mungu "alipumua " Neno lake na kutumika manabii na mitume kuandika Neno lake chini (2 Timotheo 3: 16-17; 2 Petro 1:21). Zaidi ya hayo, wale wote ambao wameweka imani yao katika Yesu Kristo wana Roho Mtakatifu aishiye ndani yao (Warumi 8: 9; 1 Wakorintho 12:13). Roho Mtakatifu anapenda kutusaidia kuelewa Biblia (1 Wakorintho 2: 10-16).

Madhumuni yetu ya kutoa muhtasari wa Bibilia / sehemu ya utafiti ni kutoa msingi dhabiti wa kila kitabu cha Biblia. Kwa kila kitabu cha Biblia, mwandishi, tarehe ya kuandikwa, madhumuni ya kuandikwa, mistari muhimu, na muhtasari mfupi utatolewa. Tuna matumaini ya dhati kwamba muhtasari wetu wa Bibilia / sehemu ya utafiti utakusaidia kuelewa Biblia vizuri, na utakutia moyo ujifunze Biblia kwa undani zaidi.

Utafiti wa Agano la Kale

Utafiti wa Agano Jipya

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Utafiti wa Biblia
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries