settings icon
share icon
Swali

Nataka mtoto, lakini mpenzi wangu hataki. Tufanye nini?

Jibu


Biblia inasema kuwa watoto ni baraka. Zaburi 127: 3 inasema, "Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu." Hii ni kinyume na jinsi ulimwengu unavyoona watoto — kama kizuizi na mzigo. Watoto hawapaswi kuchukuliwa kama dhima.

Ukosefu wa hamu ya kuwa na watoto wakati mwingine hutokea kwa nia za ubinafsi. Watu wengine hawataki watoto kwa sababu wanataka kujizingatia wenyewe, kazi zao, na pesa zao. Hawataki kuwa "amefungwa chini" au kuacha magari yao ya gharama kubwa, nyumba, au likizo. Aina hii ya mtazamo ni dhambi. Wengine hawataki watoto kwa sababu ya hofu ya kuwa hawawezi kuwa ulezi wa mafanikio au hawawezi kumudu kumlea mtoto vizuri. Wengine wana hofu kuhusu kujifungua kwenyewe. Mungu ni mkubwa na anatosha kushughulikia hofu hizi. Kwa wengine, kutotaka watoto kunahusiana na majeraha yanayotokana na uzoefu wa maumivu ya zamani. Mungu anaweza kuleta uponyaji kwa madhara haya. Kwa wengine, sababu ya kutotaka watoto inaweza tokana na kitu tofauti kabisa.

Bila kujua sababu za kutaka kuwa na watoto, ni vigumu kutambua kama hisia si "sahihi". Je, kuna masuala ya afya? Je! Kuna masuala ambayo hayajaweza tatuliwa kutoka utotoni? Haya ni mambo ambayo yanapaswa kujadiliwa kati ya wanandoa, na ikiwa ni lazima, ushauri wa ndoa ya Kikristo inapaswa kutafutwa.

Kama Wakristo, ibada yetu inapaswa kwanza kuwa kwa Mungu, ambaye anasema kuwa watoto ni baraka. Baada ya hapo, uhusiano muhimu zaidi ni pamoja na mwenzi wetu. Ikiwa ni muhimu sana kwa mwanandoa awe na watoto, inapaswa kusingatiwa, kwa mtazamo wa heshima na utii (ona Waefeso 5: 21-33). Kwa kawaida, hii ni mada ambayo inapaswa kujadiliwa kabisa kabla ya ndoa.

Ikiwa tunajijitoa kwa sala, kusoma Biblia, na kutafakari, Mungu atafunua mapenzi Yake ikiwa tunamweka wa kwanza. Warumi 12: 2 inasema, "Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu."

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nataka mtoto, lakini mpenzi wangu hataki. Tufanye nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries