settings icon
share icon
Swali

Ninawezaje kushinda hisia za kukataliwa?

Jibu


Sisi sote tunaweza kughadhabishwa na hisia za kukataliwa, na hiyo hasa ni kweli baada ya uhusiano uliovunjika. Hata hivyo, kama waumini waliozaliwa upya tuna rasilimali katika Neno la Mungu ambayo inaweza kuleta faraja na uwazi kwa hali hiyo. Kukataliwa kwa mtu mmoja haimaanishi sisi hatuwezi pendeka. Lakini tunaweza kuruhusu kukataliwa na moja kuamua jinsi tunavyohisi na kuruhusu hisia hiyo kuathiri wazo letu kuhusu jinsi tulivyo, au tunaweza kuchagua kuendelea mbele kwa msingi wa kitu ambacho kinadumu sana.

Hiyo ni nini? Kwa waumini, ni nafasi yetu katika Kristo. Tunapozaliwa mara ya pili, tunakubaliwa. "Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa"(Waefeso 1: 3-6).

Ingawa hatukustahili wala hatuwezi kuipata (Waefeso 2: 8-9), Bwana Yesu Kristo ametubariki kwa kila baraka za kiroho na ametufanya sisi kukubalika kwake. Ukubali huu ni zawadi yake ya neema, na hupunguza hisia yoyote ambayo tunaweza kuwa nayo kwa sababu sio msingi wa ukweli wa Neno la Mungu. Tunapofaa ukweli huu kwa imani, inakuwa ukweli katika mioyo yetu na maisha yetu.

Kuishi kulingana na hisia zetu ni chungu. Tutateswa na tamaa, kwa maana tunaishi katika ulimwengu ulioanguka. Jinsi tunavyoitikia kuumizwa na tamusho aidha zitatusaidia kukua na nguvu katika kutembea na Bwana au itakuwa na maana kwamba tunatembea tukiwa tumejeruhiwa. Matokeo yote ni uchaguzi wetu. Mungu huifanya iwezekane tutembea katika hali ya kutamaushwa katika maisha na fahamu kwamba msaada wake kwetu hufanya kazi. Neema na faraja yake ni yetu ikiwa tunapumzika ndani yake. Kila mtoto wa Mungu aliyezaliwa upya tena ana masharti yote na baraka ndani ya Kristo, lakini tunapaswa kuchagua kuzitumia. Ni kama kuwa na dola milioni katika benki na kuchagua kufa njaa kwa sababu hatuzitumii fedha hizo kununua chakula.

Kama waumini hatufafanuliwi kwa makossa yetu ya zamani au kwa kukata tamaa au kwa kukataa wengine. Tunafafanuliwa kama watoto wa Mungu, tuliozaliwa tena na upya wa maisha na tukiwa na baraka zote za kiroho na kukubaliwa katika Kristo Yesu. Hiyo ndiyo sababu fafanusi tunapoongea kuhusu kuishi maisha ya ushindi. Tunaweza kutembea kwa nguvu zetu wenyewe kile Mtume Paulo anachokita "mwili" wetu, au tunaweza kutembea kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Ni uchaguzi wetu. Mungu ametupatia silaha (Waefeso 6: 11-18), lakini ni wajibu wetu kizifaa kwa imani.

Kwa hiyo, kama wewe ni mtoto wa Mungu, unaweza kuteseka katika maisha haya, lakini kama mtoto wa Mfalme kutalio hili ni utamauzo kidogo. Unaweza kuchagua kudai urithi wa mtoto wa Mungu na kuendelea mbele katika neema. Msamaha wa wengine na wa nafsi ni zawadi ambayo unaweza kutoa kwa sababu ni zawadi iliyotolewa na Bwana Yesu Kristo (Waefeso 4:32).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ninawezaje kushinda hisia za kukataliwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries