settings icon
share icon
Swali

Je! agano la Kale la Kiyunani ni gani?

Jibu


Agano la Kale la Kiyunani (pia linaitwa LXX) ni tafsiri ya Biblia ya Kiebrania kwa lugha ya Kigiriki/Kiyunani. Jina "Agano la Kale la Kiyunani" linatoka kwa neno la Kilatini linalosimamia sabini. Tamaduni ni kuwa 70 (au 72) wasomi wa Wayahudi walikuwa watafsiri wa Agano la Kale la Kiyunani. Agano la Kale la Kiyunani lilitafsiriwa katika karne ya tatu na ya pili Kabla Yesu azaliwe (KK) pale Alexandria, Misri. Wakati Israel ilipokuwa chini ya mamlaka ya Ugiriki kwa karne kadhaa, lugha ya Kiyunani ilizidi kuwa ya kawaida. Kufikia karne ya 2 na ya 1 KK, watu wengi katika Israeli walizungumza Kiyunani kama lugha yao ya kwanza. Hiyo ndio sababu juhudi ilifanywa kuitafsiri Biblia ya Kiyahudi kwa Kiyunani-ili wale ambao hakuelewa Kiyahudi wangekuwa na Biblia katika lugha wangeweza kuielewa. Agano la Kale la Kiyunani linawakilisha juhudi za kwanza za kutafsiri maandishi muhimu ya kidini kutoka kwa lugha moja hadi nyingine.

Kwa kulinganisha nukuu za Agano Jipya za Biblia ya Kiebrania, ni wazi kwamba Agano la Kale la Kiyunani ilitumika mara nyingi. Nukuu nyingi za Agano Jipya kutoka kwa Biblia ya Kiebrania zimetolewa katika Agano la Kale la Kiyunani. Hii ni matokeo ya ukweli kwamba mwishoni mwa karne ya 1 KK, haswa karne ya 1 Baada ya Kristo (BK), Agano la Kale la Kiyunani likuwa "limeingia mahali pa" Biblia ya Kiebrania kama Maandiko ambayo watu wengi walikuwa wanatumia. Jinsi watu wengi walizungumza na kusoma Kiyunani kama lugha ya kwanza, mamlaka ya Ugiriki walihimiza sana matumizi ya Kiyunani, Agano la Kale la Kiyunani likawa la kawaida kuliko Agano la Kale la Kiyahudi. Watafsiri wa Agano la Kale la Kiyunani walipozidi kuwa na usahihi kama watafsiri wakitoa andiko la Kiyahudi kwa Kiyunani, tofauti zingine za tafsiri zilitokea. Lakini ukweli kwamba Mitume na waandishi wa Agano Jipya walihisi vyema, wakiwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, kuitumia Agano la Kale la Kiyunani inapaswa kutupa uhakikisho kuwa tafsiri ya lugha ya asili ya Biblia bado ni Neno la Mungu lenye mamlaka.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! agano la Kale la Kiyunani ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries