settings icon
share icon
Swali

Je! Je!Baadhi ya vielelezo maarufu vya Utatu Mtakatifu ni gani?

Jibu


Kuelezea Utatu ni lengo zuri sana, lakini ni zoezi hatimaye lisilo na maana. Wanatheolojia katika karne nyingi wamepiga bongo katika kujaribu kuunda mafundisho sahihi, vielelezo vya kuridhishisha vya Uungu wa Utatu. Kinachozuia juhudi zao ni ukweli kwamba Mungu ni mkuu, na baadhi ya sifa zake hazijulikani(Isaya 55:8-9).

Utatu ni neno la kitheoljia linalotumika kwa Mungu kuonyesha uwepo wake wa milele katika Nafsi tatu tofauti (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu) ambao wote hubaki kuwa Mungu mmoja asiyeweza kugawanyika. Dhana ya Mungu katika Utatu ni ngumu zaidi kueleweka-na haiwezi tambulika, kwa sababu rahisi, kwamba hatuna chochote katika ulimwengu wetu ambacho kina uwepo unaolingana. Wanadamu, viumbe tata zaidi tunaowajua ambao wapo kama nafsi moja, na sio kama vitu vilivyounganishwa.

Licha ya ukweli kwamba hakuna kitu katika ulimwengu wetu kinachoweza elezea kikamilifu Utatu Mtakatifu, waalimu na wanatheolojia katika miaka mingi wametoa mlinganisho kadhaa kutoka kwa ulimwengu wa asili na hisabati ili kusaidia kuelezea jambo lisiloelezeka. Hapa kuna mifano chache:

Mfano mmoja maarufu na rahisi wa Utatu ni yai. Yai la kuku lina ganda, kiiniyai na yai leupe, lakini kwa ujumla zote ni yai moja. sehemu zote tatu huunda kitu kimoja kizima. Upungufu wa mfano huu na minginevyo kama hii, ni kwamba Mungu hawezi kugawanywa katika “sehemu.” Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni kitu kimoja, lakini hio sio sawa na mfano huu wa ganda, kiiniyai na yai leupe.

Mfano sawia unatumia tufaha: ngozi ya tunda, nyama na mbegu zote zinatengeza tufaha, kama vile Baba, Mwana, na Roho vinavyojumuisha Mungu. Mfano huu una udhaifu sawia na ule mfano wa yai, sehemu zilizotajwa za tufaha zikizingatiwa kando kando, sio tufaha. Kinyume chake, kila Mtu wa Utatu, akichukuliwa kwa kujitegemea, bado ni Mungu.

Mfano mwingine unasemekana kutoka kwa Patrick mtakatifu. Patrick alipokuwa akieneza injili kwa watu wa Ayalandi, alifafanua dhana ya Utatu kwa kutumia mmea wa kawaida nchini Ayalandi: Shamroki, mshirika wa familia ya klova wenye majani matatu, majani ya kijani kibichi kwa kila shina. Hadithi moja inasema kuwa Patrick katika safari zake alikumbana na baadhi ya wakuu wa Ayalandi kwenye mbuga. Viongozi wa makabila walitatanishwa na fundisho la Utatu, na hivyo Patrick akainama chini na kukwanyua shamroki. Patrick alisema kwamba majani matatu, bado ni mmea mmoja, kama vile Nafsi tatu za Utatu ni Mungu mmoja. Hadithi nyingine inakaribiana ni hiyo, isipokuwa Patrick alipokuwa akifunza katika mkoa wa Connaught, ambapo alizungumza na binti wa Mfalme Laoghaire, Ethne na Fedelm. Linganisho la Shamroki pengine ni bora kulio mlinganisho wa yai na tufaha, ingawa lina udhaifu wa uwezekano wa kumgawanya Mungu katika “sehemu.”

Mfano mwingine wa kawaida wa Utatu unahusisha hali tofauti za maada (yabisi, kioevu, na gesi). Kielelezo hiki kwa kawaida hutumia maji kama mfano: maji yapo katika hali ya yabisi (barafu), kioevu, na gesi (mvuke wa maji). Haijalishi maji yapo katika hali gani, bado ni maji. Muundo wake wa kikemikali hubaki vile vile-ni H2O, haujalishi ikiwa yanaelea bila kuonekana katika angahewa ili kuunda unyevu, au kuelea vipande vipande kwenye chai yako ili kusaidia kupunguza unyevunyevu. Tatizo ya kielezo hiki ni kwamba maji ya kioevu, wakati yanaganda, “hubadilisha” hali au namna. Maji oevu yanaweza kuwa yabisi au mvuke. Hata hivyo, Mungu “habadilishi” hali au namna. Maji oevu yanaweza kuwa yabisi au gesi lakini Mungu Baba hawezi kuwa Mwana au Roho. Wazo kwamba Mungu hujidhihirisha kwa njia tofauti katika nyakati tofauti na katika miktadha mbalimbali (kama vile maji hujidhihirisha kwa nama mbalimbali kuwa yabisi, oevu, au mvuke) huitwa mtindo, ni fundisho potovu linapaswa kuepukwa.

Watu wengine wamepata vielelezo muhimu vya Utatu katika miundo ya kijiometri. Kwa mfano pembetatu, ina pande tatu za kujitegemea zilizounganishwa ili kuunda umbo moja. Muundo mwingine ni ule pembetatu iliyo na pinde na zimefumana, ambayo ina safu tatu zilizounganishwa na kuingiana na kutengeza pembetatu katikati:

Kupanua muundo wa pembetatu/triquetra ni kielelezo hiki cha Utatu:

Katika kitabu chake kifupi Flatland: A romance of Many Dimensions, kilichochapishwa mnamo mwaka wa 1884, Edwin Abbott anaandika juu ya Mraba unaoishi Flatland (nchi tambarare), nchi ya vipimo viwili tu. Katika mkutano wa kubadilisha maisha, Mraba hupokea ziara kutoka kwa tufe (mviringo), ambaye anaishi katika Spaceland, eneo la vipimo vitatu. Ingawa mraba hauwezi kufikiria zaidi ya vipimo viwili (hana chochote katika ulimwengu wake wa kuhusiana), anakubali neno la Tufe na uwepo wa mwelekeo wa tatu. Walakini, anapojaribu kuwasilisha maarifa yake mapya kwa wakaazi wengine wa Flatland, Mraba unachukuliwa kama kichaa na kufungwa jela. Kwa njia fulani, shida za Mraba na sawia na zetu. Lakini tunalikubali neno la Mungu, na kwa imani tunaelewa kwamba Mungu anaishi katika ufalme na kwa njia ambayo inapita fahamu zetu. Yai, tufaha, shamaroki, hali ya maada, na maumbo mbalimbali ya kijiometri zinakaribia kile Utatu ulicho katika maelezo yetu. Hatuwezi kuelewa kabisa uwepo wa Mungu. Mungu asiye na kikomo hawezi kufafanuliwa kikamilifu katika kielelezo kilicho na mwisho.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Je!Baadhi ya vielelezo maarufu vya Utatu Mtakatifu ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries