settings icon
share icon
Swali

Je, sisi huwa malaika baada ya kufa?

Jibu


Malaika ni viumbe vilivyoumbwa na Mungu (Wakolosai 1:15-17) na ni tofauti kabisa na binadamu. Wao ni mawakala maalumu wa Mungu kutekeleza mpango wake na wahudumu kwa wafuasi wa Kristo (Waebrania 1:13-14). Hakuna dalili ya kwamba malaika zamani walikuwa binadamu au kitu kingine chochote - wao waliuumbwa kama malaika. Malaika hawana haja, na hawawezi kuwa na uzoefu, wa ukombozi ambao Kristo alikuja kutoa kwa binadamu. Petro wa kwanza 1:12 inaeleza haja yao ya kuangalia katika Injili, lakini si kwa ajili yao na uzoefu. zamani wangalikuwa binadamu, wazo la wokovu halingekuwa siri kao, huku wao wenyewe kuwa na uzoefu. Naam, wao hufurahi mwenye dhambi anamrudia Kristo (Luka 15:10), lakini wokovu katika Kristo si kwa ajili yao.

Hatimaye, mwili wa muumini katika Kristo utakufa. Nini kinatokea basi? Roho wa muumini huenda kuwa pamoja na Kristo (2 Wakorintho 5:8). Muumini habadiliki na kuwa malaika. Ni ya kuvutia kwamba wote Eliya na Musa walitambuliwa juu ya mlima wa ubadilisho. Hakubadilishwa na kuwa malaika, lakini walionekana kama wao wenyewe – ingawa wakiwa na utukufu - na walitambuliwa naa Petro, Yakobo na Yohana.

Katika 1 Wathesalonike 4:13-18, Paulo anatuambia kwamba waumini katika Kristo wamelala katika Yesu, yaani, miili yao ni imekufa, bali roho zao ni hai. Kifungu hiki kinatuambia kwamba wakati Kristo atakaporudi, ataleta pamoja naye walio lala katika Yesu, na kisha miili yao itafufuliwa, watafanywa upya kama mwili wa Kristo uliofufuka, kwa kuwa alijiunga na roho zao ambazo Yeye huleta pamoja naye. Waumini wote ambao wanaishi katika kurudi kwa Kristo, wapata miili yao kubadilishwa na kuwa kama ya Kristo, na watakuwa wapya kabisa katika roho zao, bila tena kuwa na asili ya dhambi.

Waumini wote katika Kristo watatambuana na kuishi pamoja na Bwana milele. Sisi tutamtumikia katika milele yote, si kama malaika, lakini pamoja na malaika. Mshukuru Bwana kwa tumaini lililo hai Yeye huwapa muumini katika Yesu Kristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, sisi huwa malaika baada ya kufa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries