settings icon
share icon
Swali

Kwa nini fundisho la Kristo pekee ni muhimu?

Jibu


Kristo pekee (Solo Christo au solus Christus katika Kilatini) ni mojawapo wa solae ambazo hujumlisha maswala muhimu ya Matengenezo ya Kiprotestanti. Solo Christo inamaanisha Kristo pekee katika Kilatini. Solae zingine nne ni sola scriptura ("Mafundisho pekee"), sola fide ("imani pekee"), sola gratia ("Neema pekee"), na sola Deo gloria ("kwa utukufu wa Mungu peke yake"). Kila moja ya mafundisho haya ni muhimu sana. Kuondoa yoyote kutasababisha makosa na ijili ya uongo ambayo haina uwezo wa kuokoa.

Wakati Wanamatengenezo walisistiza kuhusu solo Christo (Kristo pekee), walithibitisha kwamba tunaokolewa na Kristo peke yake, na sio kwa ustahili wa mtu yeyote. Yesu pekee ndiye Mfalme wa Wafalme (Ufunuo 19:16). Yeye pekee ndiye Kuhani Mkuu (Waebrania 4:14). Yeye pekee ndiye Mkombozi wetu (Wagalatia 3:13) na Mpatanishi pekee kati ya Mungu na mwanadamu (1 Timotheo 2:5). Jaribio la kujitwalia au kushiriki katika vyeo hivyo ni majigambo ya kukufuru. Kumpa mtu mwingine majukumu hayo (kama vile Mariamu) haifai. Ni Kristo peke yake ambaye huokoa.

Hatuokolewi na haki yetu; ni Kristo pekee anayetuokoa. "Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake" (Tito 3:5). "Ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio" (Warumi 3:22). Haijalishi matendo mema tunayofanya na uaminifu wetu, "sisi ni watumishi tusio na faida" (Luka 17:10). Kristo pekee ndiye anayestahili (Ufunuo 5:9). Solo Christo (Kristo pekee).

Kuanzia mwanzo hadi mwisho, injili inainua Kristo peke yake. Yeye ndiye alitoka mbinguni na kuja kuwatafuta waliopotea (Luka 19:10). Yeye ndiye aliyetii sheria kikamilifu. Yeye ndiye aliyesulubiswa na ndiye aliyefufuka. Sisi ni wapokeaji wenye shukrani wa ukarimu wake. Sisi ni ombaomba nay eye ndiye Mfadhili. Sisi ndio wenye ukoma, na Yeye Ndiye Mponyaji. Tumefadhaika, naye Ndiye Amani. Solo Christo (Kristo pekee).

Injili sio ujumbe kuhusu kile tunapaswa kumfanyia Mungu; injili ni Habari njema ya kile Mungu ametufanyia. Kimsingi, wokovu sio juu yetu; ni kuhusu Yesu. Solo Christo. Katika mambo yote, Kristo lazima awe mtangulizi katika yote (Wakolosai 1:18), na Wanamatengenezo walirudisha mafundisho hayo ya Kiblia kwa kanisa. Kama Luther alivyoandika, "Lazima nisikize Injili. Hainiambii ninacholazimika kufanya, lakini inaniambia kuhusu ambacho Kristo, Mwana wa Mungu amenitendea" (Martin Luther, Ufafanuzi juu ya Wagalatia, Sura ya 2, Mistari 4-5).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini fundisho la Kristo pekee ni muhimu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries