settings icon
share icon
Swali

Nini kusudi ya zawadi za ishara za kibiblia?

Jibu


Tunapozungumzia zawadi za kibiblia, tunazungumzia miujiza kama kusema kwa lugha, maono, uponyaji, kufufua wafu, na kutabiri. Hakuna swali kati ya waumini kama zilikuwepo au hazikuwepo, kwa maana Bibilia inaelezea waziwazi. Ambapo kutokubaliana hutokea kati ya waumini ni kusudi lao, pamoja na swali la kuwa tunapaswa kupitia leo. Wengine wanasema kuwa zawadi hizi ni ishara ya wokovu wa mtu, wakati wengine wanasema ni ishara ya ubatizo wa Roho Mtakatifu, na wengine wanasema kusudi lao ni kuthibitisha ujumbe wa Injili. Tunawezaje kujua ukweli? Lazima tutafute Maandiko ili tutaelezea kusudi la Mungu kuhusu mambo haya.

Moja ya kumbukumbu za mwanzo za ishara za zawadi katika Biblia zinapatikana katika Kutoka 4, wakati Musa akifundishwa na Mungu kuhusu ukombozi uliokaribia kutoka Misri. Musa alikuwa na wasiwasi kwamba watu hawataamini kwamba Mungu alimtuma, hivyo Mungu akampa ishara ya fimbo kuwa nyoka na mkono wake kuwa na ukoma. Mungu alisema ishara hizi zilikuwa "ili kwamba wapate kusadiki ya kwamba Bwana, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo, amekutokea " (mstari wa 5).Kisha itakuwa wasipoamini hata ishara hizo mbili, wala kusikiliza sauti yako, basi, yatwae maji ya mtoni uyamwage juu ya nchi kavu, na yale maji uyatwaayo mtoni yatakuwa damu juu ya nchi kavu (mstari wa 9). Kusudi la watoto wa Israeli ni kwamba wangeamini mjumbe wa Mungu.

Mungu pia alimpa Musa ishara za ajabu kumwonyesha Farao, ili awaache watu waende. Katika Kutoka 7: 3-5, Mungu alimwambia Musa kwamba atazidisha ishara na maajabu yake Misri, kwa hivyo "Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, hapo nitakapounyosha mkono wangu juu ya Misri na kuwatoa wana wa Israeli watoke kati yao." Mungu alitaka watu wa Misri kujua kwamba Yeye ndiye aliyefanya kazi ya kuwakomboa Waisraeli. Katika Kutoka 10: 7, Musa alimwambia Farao kwamba dhiki ya mwisho, ambayo ingeua mzaliwa wa kwanza, ilikuwa kuonyesha kwamba Mungu alifautisha kati ya Wamisri na Waisraeli. Ishara na maajabu yalithibitisha ujumbe wa Mungu kwa Farao na Wamisri, hivyo wangejua kwamba Musa alitumwa na Mungu.

Wakati Eliya alipowakabili manabii wa uongo juu ya Mlima Karmeli (1 Wafalme 18), aliomba Mungu atume muujiza wa moto kutoka mbinguni ili watu waweze kujua "wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, nay a kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako ... ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, Ee Bwana, ndiwe Mungu "(mstari 36-37). Miujiza yeye na manabii wengine walifanya ni uthibitisho kwamba Mungu alikuwa amewatuma manabii na kwamba Mungu alikuwa akifanya kazi katikati ya Israeli.

Yoeli alipewa ujumbe wa hukumu ya Mungu juu ya Israeli, na ndani ya ujumbe huo ulikuwa unabii wa rehema na matumaini. Wakati hukumu ilikuja vile ilitabiriwa, na watu waliitikia kwa kutubu, Mungu alisema kuwa ataondoa hukumu na kurejesha baraka zake: "Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wanu, wala hakuna mwingine: Na watu wangu hawatatahayari kamwe"(Yoeli 2:27). Mara tu baada ya maneno hayo, Mungu alisema juu ya kumwaga Roho Wake juu ya watu, hivyo wangeweza kutabiri, kuona maono, na kuona maajabu yanayotokea. Wakati Wanafunzi walipoanza kuzungumza kwa lugha kwa siku ya Pentekoste (Matendo 2: 1-21), Petro akasema, "Haya ndiyo yale yaliyosemwa na nabii Yoeli." Ilikuwa na lengo gani? Ili watu waweze kujua ujumbe ulioletwa na Petro na wengine ulikuwa ujumbe wa Mungu.

Huduma ya Yesu ilikuwa imeambatana na ishara na maajabu mbalimbali. Nini kusudi la miujiza Yake? Katika Yohana 10: 37-38, Yesu alikuwa akiwajibu Wayahudi ambao walitaka kumpiga mawe kwa kumshutumu, na akasema, "Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini; lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini kazi zile: mpate kujua na kufahamu ya kuwa Baba yu ndani yangu, nani ni ndani ya Baba." Kama vile katika Agano la Kale, kusudi la miujiza ya Yesu ilikuwa kuthibitisha mkono wa Mungu juu ya Mtume Wake.

Mafarisayo walipomuuliza Yesu awaonyeshe ishara, Yesu alisema, "Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, ila ishara ya nabii Yona. Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi. Watu wa Niwani watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa: kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona: na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona "(Mathayo 12: 39-41). Yesu alikuwa wazi sana kwamba kusudi la ishara ilikuwa hivyo watu wangekubali ujumbe wa Mungu na kujibu kwa namna hiyo. Vivyo hivyo, katika Yohana 4:48, alimwambia mheshimiwa, "Basi Msipoona ishara na maajabu, humtaamini kabisa." Ishara hizo zilikuwa msaada kwa wale waliokuwa na shida ya kuamini, lakini ujumbe wa wokovu katika Kristo ulikuwa ndio lengo.

Ujumbe huu wa wokovu ulielezewa na Paulo katika 1 Wakorintho 1: 21-23: "Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neon linalohubiriwa. Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima: bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulubiwa: kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi." Ishara zina lengo lake, lakini ni njia ya mwisho mkuu-wokovu wa roho kupitia mahubiri ya injili. Katika 1 Wakorintho 14:22, Paulo anasema kwa wazi kwamba "lugha si ishara kwa waumini bali kwa wasioamini." Mungu alitumia ishara za ajabu kama kusema katika lugha ili kuwashawishi wasioamini kuwa ujumbe wa Kristo ulikuwa wa kweli, lakini kama sehemu yote ya mazingira inaonyesha, jambo muhimu zaidi lilikuwa ni tamko la wazi la ujumbe wa injili.

Jambo moja ambalo mara nyingi hupuuzwa katika majadiliano juu ya ishara na miujiza ni wakati na uwekaji wao katika Maandiko. Kinyume na imani maarufu, watu wa nyakati za Biblia hawakuona miujiza wakati wote. Kwa kweli, miujiza ya Biblia kwa ujumla inajumuisha kuzunguka matukio maalum katika Mungu kushughulika na wanadamu. Uokoaji wa Israeli kutoka Misri na hadi kuingia katika Nchi ya Ahadi ulifuatana na miujiza mingi, lakini miujiza ilinyauka haraka baadaye. Wakati wa miaka ya ufalme wa mwisho, wakati Mungu alikuwa karibu kuwaweka watu uhamishoni, Aliruhusu baadhi ya manabii Wake kufanya miujiza. Wakati Yesu alikuja kuishi kati yetu, alifanya miujiza, na katika huduma ya kwanza ya mitume, walifanya miujiza, lakini nje ya nyakati hizo, tunaona miujiza chache au ishara katika Biblia. Wengi wa watu ambao waliishi katika nyakati za Biblia hawakuona ishara na maajabu kwa macho yao wenyewe. Walipaswa kuishi kwa imani katika yale ambayo Mungu alikuwa amewafunulia tayari.

Katika kanisa la kwanza, ishara na maajabu zilizingatia hasa kwenye uwasilishaji wa kwanza wa injili kati ya makundi mbalimbali ya watu. Siku ya Pentekoste, tunasoma kwamba kulikuwa na "Wayahudi, watu waaminifu, kutoka kila taifa chini ya mbinguni" walikusanyika Yerusalemu (Matendo 2: 5). Ilikuwa kwa Wayahudi hawa, ambao walikuwa wamelelewa katika nchi nyingine na wakazungumza lugha hizo za kigeni (mstari wa 6-11), kwamba ishara ya lugha ilipeanwa kwanza. Walikubali kwamba walikuwa wakisikia kwa lugha zao za asili juu ya kazi za ajabu za Mungu, na Petro akawaambia kuwa majibu ya pekee yaliyofaa ni kutubu dhambi zao (mstari wa 38). Wakati injili ilipotolewa kwa mara ya kwanza kati ya Wasamaria, Filipo alifanya ishara na maajabu (Matendo 8:13).

Tena, wakati Petro alipopelekwa Kornelio, Mataifa, Mungu alitoa ishara ya miujiza kuthibitisha kazi Yake. "Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa,watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipwa cha Roho Mtakatifu. Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu "(Matendo 10: 45-46). Petro alipoulizwa na mitume wengine, alitoa hii kama ushahidi wa kuongoza kwa Mungu, na wengine "wakamtukuza Mungu, wakisema," Kwa hiyo, kwa Wayahudi pia Mungu ametoa toba inayoongoza kwa uzima "(Matendo 11:18).

Katika kila hali, zawadi za ishara zilikuwa uthibitisho wa ujumbe na mjumbe wa Mungu, ili watu waweze kusikia na kuamini. Mara baada ya ujumbe kuthibitishwa, ishara zilinyauka. Hatuitaji ishara hizo kurudia katika maisha yetu, lakini tunahitaji kupokea ujumbe huo wa injili.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nini kusudi ya zawadi za ishara za kibiblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries