settings icon
share icon
Swali

Je! Mungu anaahidi kutotupatia zaidi kuliko tunayoweza kustahimil?

Jibu


Wakorintho 10:13 inasema, "Jaribio halikuwapta nyinyi, isipokua lililo kawaida kwa wanadamu. Na Mungu ni mwaminifu; yeye hatawaacha mjaribiiwe kupita mwezavyo;. Lakini unapojaribiwa, atakupa njia ya kutokea ili uweze kustahimili. "Maandiko haya yanatufundisha kanuni nzuri. Ikiwa sisi ni wake, Mungu hataruhusu shida yoyote kuingia katika maisha yetu ambayo hatuwezi kustahimili. Kwa kila jaribio linalokuja njiani yetu, Mungu atabaki kuwa mwaminifu kwetu; Atatoa njia ya kustahimili jaribio. Hatupaswi kuingia kwenye dhambi. Tunaweza kumtii Mungu katika kila hali.

Kwa hivyo, tuna moti nasha kutoka kwa Mungu katika kutembea kwetu kwa Kikristo. Sala "Tuokoe na uovu" (Mathayo 6:13) itajibiwa. Hata hivyo, ahadi hizi hazimaanishi sisi hatutawahi kuwa na shida; Kwa kinyume chake, Yesu alisema, "Katika ulimwengu huu utakuwa na shida" (Yohana 16: 33a). Jambo la maana linapatikana katika maneno yafuatayo ya Yesu, "Lakini usife moyo! Nimeshinda ulimwengu "(Yohana 16: 33b).

Paulo na wenzake walijaribsiwa sana waliokua wakitangaza Injili katika maeneo mapya. Huu ndio ushuhuda wake: "Sisi tulikuwa chini ya shinikizo kubwa, mbali na uwezo wetu wa kustahimili, ili tufadhaike kwa maisha yenyewe. Hakika, tulihisi kana kwamba tulipokea hukumu ya kifo "(2 Wakorintho 1: 8-9). Inaonekana kama Paulo alijaribiwa zaidi ya kile angeweza kustahimili- "mbali zaidi." Ukweli huu unatuongoza kwenye ukweli mwingine: nguvu zetu za kuvumilia majaribio hazitoki kwetu; inatoka kwa Mungu. Hiyo ndivyo Paulo anasema hapo mbeleni: "Hili lilitokea ili tusijitegemee ila tu Mungu" (2 Wakorintho 1: 9). Paulo anaendelea na sifa kwa Bwana kwa ajili ya ukombozi Wake (mstari wa 10) na kusisitiza juu ya ufanisi wa maombi ya kanisa (mstari wa 11).

Kitu chochote kinachokuja kwa njiani yetu, chochote kinachotushutumu, msiba wowote unaotufikia, tuna uwezo, kwa nguvu za Mungu, ya kushinda. Katika vitu vyote tunaweza kufikia ushindi wa kiroho, kupitia Kristo. Maisha si rahisi. Ukweli ni kwamba mara nyingi tunahitaji "njia ya kukimbia." Maisha ni ngumu, lakini tunaweza kukabiliana nayo kwa ujasiri katika ahadi za neema za Mungu.

Sisi ni "zaidi ya washindi" katika Kristo (Warumi 8:37). "Kila mtu aliyezaliwa na Mungu anashinda ulimwengu. Hii ni ushindi ambao umeshinda ulimwengu, hata imani yetu "(1 Yohana 5: 4). "kushinda" majaribio ya ulimwengu ni kuibwaga kabisa, kama Daudi, kwa nguvu za Mungu, alishinda Goliathi. Mipango mbaya na hali zisizokubalika hazitafanikiwa. "Wameninyanyasa sana tangu ujana wangu, lakini hawajapata ushindi juu yangu" (Zaburi 129: 2). Majaribio yetu ni kwa madhumuni, tuna silaha za Mungu na fursa ya maombi, na Mungu atahakikisha kuwa majaribu yetu hayatashinda imani yetu. Msimamo wetu kama watoto wa Mungu ni salama; Tutapitia majaribio na kubaki salama "Ninaamini kwamba. . . hakuna chochote katika viumbe vyote, ambacho kitatweza kututenga na upendo wa Mungu ulio ndani ya Kristo Yesu Bwana wetu "(Waroma 8: 38-39).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mungu anaahidi kutotupatia zaidi kuliko tunayoweza kustahimil?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries