settings icon
share icon
Swali

Je! Kuna uhusiano gani kakit ya wokovu na msamaha?

Jibu


Wakati tunamkubali Yesu kama Mwokozi, tunapokea wokovu na msamaha. Lakini hiyo si mwisho. Pia Biblia inasema tumepokea uthibitisho, ukombozi, upatanisho, fidia, msamaha na uhuisho. Kila mojawapo ya maneno haya ya kitheolojia hudhirisha ukweli madhumuni kuhusu baraka ambayo tunaipokea wakati Yesu anakuwa Mwokozi wetu. Wokovu na msamaha, huku yakiwa wamekaribiana, sio maneno sawia.

Neno wokovu hutoka kwa neno la Kigiriki sozo, ambalo linamaana kuwa "kukombolewa, kuokolewa." Wokovu ni kukombolewa kutoka kwa adhabu ya dhambi, ambayo ni utengano na Mungu milele (Warumi 6:23; Mathayo 25:46). Wokovu ni Mungu kutuokoa kutoka kwa hukumu tunayostahili. Wokovu pia humuisha pia kukombolewa kwa dharura kutoka kwa nguvu za dhambi katika maisha haya. Dhambi imepoteza mamlaka yake juu ya wale wameokoka (Warumi 6:14). Imani katika Kristo inatuokoa kutoka kwa maisha tupu na yasiyo na maana vile imeelezwa katika Mhubiri na kutupa maisha ya utele na yenye matunda (Yohana 10:10; Wagalatia 5:22-23).

Neno msamaha linatokana na neno la Kigiriki aphiemi, ambalo linamaansiha "kuachilia, kukata tamaa, kutoshikilia tena." Wakati Yesu anasamehe dhambi zetu, makosa yetu, udhaifu, na uasi wetu umefutwa kutoka kwa rekodi. Msamaha wa dhambi unafanana na deni ya fedha ilifutiliwa mbali. Wakati Mungu anasamehe dhambi zetu, sisi tuko huru. Mungu hawezi yashikilia dhidi yetu tena (Zaburi 103:12).

Wokovu na msamaha zakaribiana sana. Hakuna wokovu bila msamaha. Wokovu ni njia ya Mungu kutokomboa toka kwa madhara ya dhambi. Msamaha ni Mungu kufutilia mbali deni yetu ya dhambi. Kwa kutumia kielelezo cha fedha, katika msamaha Mungu anararua stakabadhi zilizoorodhesha deni yetu, na sasa wokovu ni Mungu kutukomboa toka jela ya deni. Mungu asifiwe kwa wokovu na msamaha ambao ametupa. Hebu maisha yetu yaonyeshe shukrani kwa yaleo yote ametutendea (Warumi 12:1).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kuna uhusiano gani kakit ya wokovu na msamaha?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries