settings icon
share icon
Swali

Je, nitajua aje ikiwa nimepata wito kwa huduma?

Jibu


Kwa mawazo ya kawaida kila Mkristo ako na wito wa huduma. Tume kuu ( Mathayo 28:18-20) inaashiria waumini wote na wakristo wanajumuisha mwili wa Kristo. Ili kutimiza jukumu lako katika mwili wa Kristo bila kujali jukumu lenyewe ni lazima uhudumie wengine. Hata hivyo, watu wengi wenye huuliza swali hili huwa wanataka kujua ikiwa wameitwa kwa huduma ya ufundi kama ya uchangaji. Ni swali nzuri ilo,sazingine huduma ya ufundi iko na mahitaji ya kipekee.

Ili kudhibitisha wito wowote,ni muhimu kuchunguza moyo wako na motisha(Yeremia 17:9).Una uhakika huu wito umetoka kwa Mungu au ni wa kujinufaisha?au ni majaribu ya kuishi kulingana na matarajio ya mtu kukuhusu?Ikiwa motisha ni ya kiburi au ya kufurahisha watu,basi unafaa kusitisha.Unahisi "kuitwa"kwa sababu unafikiri ya kuwa ili uwe mkristo mkuu"ni lazima ufanye kazi kidhahiri kwa huduma ya mkristo? Wakristo ndio manukato ya Kristo(2wakorintho2:15) haijalishi penye unafanya huduma,unaweza kuwa mwangaza na chumvi na ufanye huduma nje ya kanisa au kwa kazi ya kidunia jinsi tu ufanyavyo katika kanisa au kwa wito dhahiri wa mkristo.

Kujishuku sazingine inaeza chukuliwa kama wito kwa huduma. Wakristo wengi husikia kuwa kumhudumia Mungu ni lazima utoe dhabihu na si kweli. Hii haina maana kuwa Mungu anaita kila mkristo kwa huduma geni ama huduma yenye haina furaha. Ni ukweli kuishi kikristo lazima ujitolee lakini si kujitesa, kwa sababu kuna furaha kuishi na wito wetu. Paulo ni mfano kamili wa maneno haya, kwa sababu aliteseka sana katika huduma yake lakini aliishi akiwa na furaha kwa Kristo( soma ujumbe wa Paulo kwa wafilipi).

Ukihakikisha kuwa moyo wako umepata motisha ya kutosha,unafaa kuangazia talanta zako za kimwili(pamoja na za kiroho) na uwezo wako. Je, hii inakaa kuambatana na wito wako wa huduma ambao umechagua? Ndio, Mungu ameonyesha uwezo penye kuna udhaifu wetu na anatuita kwa huduma tufanye kazi kwa uwezo wake bali si kwa uwezo wetu, pia ametupea talanta na zawadi mbalimbali ili tuweze kumtumkia kikamilifu. Haiwezekani Mungu kuita mtu ambaye hana ujuzi wowote wa kifundi kurekebisha kitu. Je, uko na talanta kwa huduma ambayo umepata wito?

Kitu ingine ya muhimu ya kuangazia ni mwelekeo wako wa asili. Mtu ambaye ameimarishwa na ukweli Fulani,mfano, mtu kama uyo haendi kuwa na furaha kwenye nafasi yeyote katika uchungaji. Unaeza pata majaribu ya talanta ama ata majaribu ya kibnafsi ili kubaini mwelekeo wako wa talanta .

Mahala pengine pa kuangazia ni ujuzi wako. Mungu hutueka tayari kabla ya kututuma kwa huduma yetu, kwa mfano, kwa Biblia tunaona Daudi akipata mafunzo kutoka kwa Saulo ata kama alifaa kuwa mfalme ama zile nyakati za Musa uko misri na wakiwa jangwani na jinsi aliongoza waisraeli kutoka kwa utumwa. Je, kuna vitu au mafunzo fulani yako ambayo Mungu anaeza tumia katika kazi yako ya huduma?

Pia unaeza tafuta mawaidha( angalia Methali 11:14 na 15:22 ). Udhaifu wetu na uwezo wetu unaeza onwa na watu wengine lakini si sisi wenyewe. Ina manufaa ukipata mawaidha kutoka kwa marafiki wa kuaminika na ambao wameokoka na ni vizuri kuzingatia maoni ya wengine kukuhusu. Je, watu huonekana wakifuata mienendo zako kwa hiari yao ama huwa unalazimisha uongozi wako? Je, watu wamefungua nyoyo zao kwako na kukuelezea mahitaji yao? Hata kama ni muhimu kutafuta mawaidha, haifai kuyategemea kikamilifu kwa sababu mara zingine marafiki na jamii hupotosha( angalia Samueli 16:7). Hata hivyo majibu yenye uaminifu kutoka kwa wale ambao wanakupenda yanafaa kusaidia wito wako.

Kila mtu ako na wito wa kipekee kutoka kwa Mungu. Wito kwenye huduma ya kifundi mara mingi huwa ya umma na wale ambao wako kwenye huduma hii ya umma huwa wametambulika ama kukosolewa. Yakobo 3:1 inasema, "Ndugu zangu, msiwe waalimuwengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi."Wale ambao wako katika nafasi za uongozi katika huduma huwa wanachukuliwa kuwa wa viwango vya juu kwa sababu wanaongoza wengine.Katika Timotheo ya kwanza na pili na kitabu cha Tito zinaelezea mahitaji ya viongozi kwenye kanisa.

Wakati unabaini kama umeitwa kwa huduma ama hujaitwa unafaa kuangazia kenye inajumuisha na ukue mjasiri na umwamini Mungu. Ikiwa Mungu amekuita atakuandaa na akujaze ili uweze kuhudumia wengine( Mathayo 6:33; Waebrania 13:20-21; Waefeso 3:20-21; Zaburi37:23; na Isaya 30:21)

Kitu ingine, ni muhimu kuenda mbele. Mara mingi huwa tunasita kusonga adi wakati tutadhibitisha wito wetu, lakini inaeza kuwa rahisi kurekebisha kitu yenye ishaanzaa kuliko kurekebisha yenye ijaanza. Tunapoanguka kutoka kwa imani yetu ata kama si kwa njia nzuri,Mungu ni mwaminifu na anatuongoza bado.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, nitajua aje ikiwa nimepata wito kwa huduma?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries