settings icon
share icon
Swali

Je, ni nini wiki sabini/sabini saba ya Daniel?

Jibu


Unabii wa "Wiki sabini" au "sabini saba" ni mojawapo ya unabii muhimu na wa kina wa Kimasihi wa Agano la Kale. Inapatikana katika Danieli 9. Sura huanza na Danieli kuombea Israeli, akikubali dhambi za taifa dhidi ya Mungu na kuomba huruma ya Mungu. Vile Danieli alipoomba, malaika Gabrieli alimtokea na akampa maono ya baadaye ya Israeli.

Mgawanyiko wa wiki 70
Katika mstari wa 24, Gabriel anasema, "Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu." Karibu wasemaji wote wanakubali kwamba sabini "saba" ni lazima ieleweke kama "wiki" sabini za miaka, kwa maneno mengine, kipindi cha miaka 490. Aya hizi hutoa aina fulani ya "saa" ambayo inatoa wazo la wakati Masihi angekuja na baadhi ya matukio ambayo yataambatana na muonekano Wake.

Unabii unaendelea kugawanya miaka 490 katika vitengo vidogo vitatu: moja ya miaka 49, moja ya miaka 434, na moja ya miaka saba. "Wiki" ya mwisho ya miaka saba inagawanywa zaidi nusu nusu. Mstari wa 25 unasema, "Tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili." "Saba "saba" ni miaka 49 , na sitini na mawili "saba" ni miaka mingane 434: miaka 49 + miaka 434 = miaka 483.

Kusudi la Wiki 70
Unabii una taarifa juu ya kusudi la mara sita ya Mungu kwa kuleta matukio haya kupita. Mstari wa 24 unasema kuwa kusudi hili ni 1) "kukamilisha makosa," 2) "kukomesha dhambi," 3) "kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu," 4) "kuleta haki ya milele," 5) "kutia muhuri maono na unabii," na 6)" kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu sana."

Tazama matokeo haya yanashughulikia ufutaji wa dhambi na uanzishwaji wa haki. Unabii wa wiki 70 unafupisha kile kinachotokea kabla ya Yesu kuanzisha ufalme wake wa milenia. Kwa kuzingatia maalum ni ya tatu katika orodha ya matokeo: "kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu." Yesu alitimiza upatanisho wa dhambi kwa kifo Chake msalabani (Warumi 3:25; Waebrania 2:17).

Ukamilishaji wa Wiki 70
Gabriel alisema saa ya unabii itaanza wakati amri ilitolewa ili kujenga upya Yerusalemu. Kuanzia tarehe ya amri hiyo hadi wakati wa Masihi itakuwa miaka 483. Tunajua kutoka kwa historia kuwa amri ya "kurejesha na kujenga upya Yerusalemu" ilitolewa na Mfalme Artashasta wa Uajemi c. 445 Kabla ya Kristo (angalia Nehemia 2:1-8).

Kitengo cha kwanza cha miaka 49 (saba "saba") kinashughulikia muda uliotakiwa kujenga upya Yerusalemu, "pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu" (Danieli 9:25). Ujengaji upya huu umeandikwa katika kitabu cha Nehemia.

Kutumia desturi ya Kiyahudi ya mwaka wa siku 360, miaka 483 baada ya 445 kabla ya Kristo inatuweka katika 30 baada ya Kristo, ambayo ingefanana na kuingia kwa Yesu kwa ushindi Yerusalemu (Mathayo 21:1-9). Unabii katika Danieli 9 unasema kwamba baada ya kukamilika kwa miaka 483, "Masihi atakatiliwa mbali" (mstari wa 26). Hii ilitimizwa wakati Yesu alisulubiwa.

Danieli 9:26 inaendelea na utabiri kwamba, baada ya Masihi kuuawa, "watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu." Hii ilitimizwa na uharibifu wa Yerusalemu katika 70 Baada ya Kristo. "Mkuu atakayekuja" ni kumbukumbu ya Mpinga Kristo, ambaye, inaonekana, atakuwa na uhusiano na Rumi, kwani ilikuwa ni Warumi ambao waliangamiza Yerusalemu.

Wiki ya mwisho ya wiki 70
Kati ya 70 "saba," 69 yametimizwa katika historia. Hii inaacha moja zaidi ya "saba" bado kutimizwa. Wasomi wengi wanaamini kwamba sasa tunaishi katika pengo kubwa kati ya wiki ya 69 na wiki ya 70. Saa ya unabii imesimamishwa, kama ilivyokuwa. "Saba" ya mwisho ya Danieli ni kile tunachoita kuwa kipindi cha dhiki.

Unabii wa Danieli unaonyesha baadhi ya matendo ya Mpinga Kristo, "mtawala atakayekuja." Mstari wa 27 inasema, "Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja". Hata hivyo, "na kwa nusu ya juma hiyo ... litasimama chukizo la uharibifu" katika hekalu. Yesu alionya juu ya tukio hili katika Mathayo 24:15. Baada ya Mpinga Kristo kuvunja agano na Israeli, wakati wa "dhiki kuu" huanza (Mathayo 24:21).

Danieli pia anatabiri kwamba Mpinga Kristo atakabiliana na hukumu. Yeye anatawala tu "na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu" (Danieli 9:27). Mungu ataruhusu tu uovu kwenda mbali sana, na hukumu ambayo Mpinga Kristo atakabiliwa tayari imepangwa.

Hitimisho
Unabii wa wiki 70 ni ngumu na kuelezwa ajabu sana, na mengi imeandikwa juu yake. Bila shaka, kuna tafsiri mbalimbali, lakini kile tulichowasilisha hapa ni maoni ya mgawo, ya kabla ya milenia. Jambo moja ni hakika: Mungu ana ratiba, na anaweka vitu kwa wakati. Anajua mwisho tangu mwanzo (Isaya 46:10), na tunapaswa daima kutafuta kurudi kwa ushindi wa Bwana wetu (Ufunuo 22:7).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni nini wiki sabini/sabini saba ya Daniel?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries