settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu wema dhidi ya uovu?

Jibu


Miongoni mwa imani za kilimwengu kwa wanadamu wote ni dhana ya “wema dhidi ya uovu.” Kila utamaduni katika kila zama umeshikilia toleo fulani la mapambano haya. Ufafanuzi wa maneno wema na uovu hutofautiana sana, vile vile maoni kuhusu jinsi maneno hayo yanavyohusiana. Hata hivyo, imani katika tofauti kati ya kile ambacho ni “chema” na kile ambacho ni “kibaya” imeenea kwa wanadamu wote. Wakati hiari zote na mawazo yote yanapolinganishwa, ni Biblia pekee ambayo inayotoa mtazamo juu ya wema na uovu ambao unashikamana kikamilifu na unaoweza kuishi kikamilifu (Zaburi 25:6-15).

Kulingana na Biblia, “wema dhidi ya uovu” sio jambo la maoni. Wala sio mapambano yanayolingana kati ya viumbe viwili au nguvu. Maandiko hayaonyeshi kwamba mipaka ya mema na mabaya hubadilika. Wala haidai mkinzano baina yao utadumu milele. La umuhimu wa kipekee ni kwamba Biblia haipendekezi baadhi ya watu ni wema, na huku wengine ni waovu.

Badala yake, Biblia inafunza kwamba wema na uovu vimefafanuliwa kwa mjibu wa Mungu mkamilifu na asiyebadilika. Kila mtu apigane kibinafsi na kuwepo kwa majaribu ya uovu. Maandiko yanabainisha kwamba uovu wote, bila ubaguzi, hatimaye utaadhibiwa na kushindwa. Na inatuambia kwamba kuna kiwango cha mwisho cha wema ambacho tunapaswa kutamani-kiwango kilichokuzwa ndani ya mtu, badala ya nadharia.

Kimakusudi mema na mabaya yanatofautiana
Kulingana na Biblia, kunayo tofauti kati ya wema na uovu. Baadhi ya mitazamo ya ulimwengu inadai kwamba tofauti zote za kimaadili zinategemea tu hiari. Kwa mfano, imani ya kutokuwepo kwa Mungu hairuhusu msingi wote wa kufafanua kitu chochote kama “chema” au “kibaya.” Katika ulimwengu usiomcha Mungu, kuna vitu tu ambavyo mtu anapendelea na vitu ambavyo mtu hapendi. Hii ndiyo sababu kuu ya ni kwa nini falsafa zinazokumbatia ukana Mungu daima huelekea kwenye vurugu na udhalimu: hakuna hisia ya mamlaka ya juu na hakuna sababu ya kudhibiti matakwa ya wale walio na mamlaka.

Dhana ambayo inafafanua mema na mabaya inategemea mapendeleo au hali kwa kawaida huitwa uwiano wa kimaadili. Maandiko yanalikataa wazo hili kwa kuwa ni la uongo. Biblia inafafanua baadhi ya mambo kuwa “mema” na mambo mengine kuwa “mabaya” (Isaya 5:20; Warumi 12:9). Mgawanyiko huu unaakisiwa katika matumizi thabiti ya mada kama vile mwanga dhidi ya giza (Isaya 9:2; Mathayo 4:16; Yohana 1:5; Waefeso 5:8). Hatima ya mwisho ya watu wote inategemea ikiwa wanamfuata Mungu mwema au wanampinga (1 Wakorintho 6:9-11; Ufunuo 21:8).

Kupambanua kati ya mema na mabaya inawezekana tu ikiwa inahusiana kiwango kimoja kisichobadilika: asili kamilifu ya Mungu. Mungu hayuko chini ya maadili, kwa kuwa Yeye ndiye chanzo na kipimo cha maadili. Wala maadili hayawezi kubadilika, kwa kuwa asili kamilifu ya Mungu ni ya milele na haibadiliki. Pingamizi kama lile la kuanguka kwa Euthyphro, tangu halibainishi kati ya Mungu wa milele na asiyebadilika na miungu ibadilikayo ya dini ya Kigiriki ya kale.

Mema na mabaya hayajasawazishwa
Sehemu ya mara kwa mara ya hadithi za uongo na uwezo wa kubuni taswira na dhana kwamba mema na mabaya yana usawa, nguvu zinazofanana. Kulingana na maoni haya, hakuna hata mmoja anayedhibiti. Aidha hatimaye inaweza kushinda. Hii ni dhana ya uwili, ambayo inaonyesha uwiano wa kudumu kati ya nguvu za mema na mabaya. Katika baadhi ya matukio, uwili unamaanisha kwamba viumbe vinavyopingana, kama vile Mungu na Shetani, wamekwama katika mapambano ya kutawala na kuwa na mamlaka.

Baadhi ya mitazamo hufunza kwamba wema wote na uovu hatimaye vitasawazishwa. Hii inahusiana na dhana ya Mashariki kama vile karma, ambayo ina maana kwamba mema na mabaya hayana usawa lakini siku moja yatasawazishwa.

Maandiko yanakataa uwili na kuichukulia kuwa uongo. Biblia inaonyesha kwamba Mungu ni mkuu kabisa na hayuko hatarini yoyote ya kushindwa (Ayubu 42:2; Zaburi 89:8; Wagalatia 6:7). Chenye Shetani hufanya, yeye “ameruhusiwa” kufanya hivyo, lakini hawezi kufanya amzidi Mungu nguvu (Ayubu 1:12; Ufunuo 9:1; 20:7). Kibiblia, uovu umekusudiwa kushindwa na uharibifu. Hakuna hata tendo moja la uovu litakaloepuka hukumu; kila dhambi italipiwa na Kristo msalabani (2 Wakorintho 5:21) au na wale wanaomkataa Kristo (Yohana 3:36) wanapoitumikia milele yao katika kuzimu (Ufunuo 20:11-15).

Mema na Mabaya sio vitu vya nje
Ushahidi kwamba ubinadamu unashikilia dhana ya msingi ya wema dhidi ya uovu ni dhahiri (Warumi 1:18-20). Hii inaelezea ni kwa nini mawazo ya kiadili-yanayobainisha “kilicho” kutoka kwa “kile kinachopaswa kuwa”-ni sehemu ya kilimwengu kote ya wanadamu. Bila shaka, hiyo haimaanishi kwamba watu wote wana maoni sawa juu ya mema na mabaya. Hatuchunguzi maadili kutoka nje, kama waangalizi wa upande wowote; mijadala yote ya kimaadili kwa ufafanuzi inahusisha mtu/watu wanaoyajadili pia.

Sehemu ya kipekee ya mafundisho ya Biblia juu ya mema na mabaya ni kwamba watu wote, bila ubaguzi, wako chini ya dhambi na uovu (Warumi 3:10; 3:23). Dhana ya kibiblia ya asili ya dhambi ina maana kwamba tofauti kati ya wema na uovu hauwezi kuletwa kati ya watu. Badala yake inavutiwa ndani na mtu binafsi. Ukweli huu wa asili ya mwanadamu ni muhimu kuelewa (Mathayo 15:19-20). Kama vile Aleksandr Solzhenitsyn alisema, “Laiti yote yangekuwa rahisi sana! Laiti kungekuwa na watu waovu mahali fulani wakifanya movu kwa hila, na ingehitajika tu kuwatenganisha na sisi wengine na kuwaangamiza. Lakini mstari unaogawanya mema na mabaya unakata moyo wa kila mwanadamu. Na ni nani aliye tayari kuharibu sehemu ya moyo wake mwenyewe?”

Kwa lugha rahisi zaidi C. S. Lewis alibainisha, “Kuwa Mkristo kunamaanisha kusamehe wasio na udhuru kwa sababu Mungu amekwisha samehe wasio na udhuru” (ona Mathayo 6:14-15).

Ukweli mmoja unaopatikana katika injili ni kwamba watu wote, bila ubaguzi, ni wenye dhambi na wanahitaji Mwokozi. Ukristo wa Kibiblia hauoni wema dhidi ya uovu kama vita vya kupiganwa duniani (Yohana 18:36), suala la kusuluhisha kwa kulipiza kisasi au kuadhibu (Warumi 12:20-21), au msimamo wa kifalsafa unaopaswa kuzingatiwa. Biblia inasema kila mtu ameumbwa kwa kusudi jema (Mwanzo 1:27; Wagalatia 3:28) lakini anateseka kutokana na moyo mbaya (Warumi 7:15-25), ambao unaweza tu kurekebishwa kwa imani katika Yesu Kristo (Yohana 14:6). Ukombozi unapatikana kwa mtu yeyote (Mathayo 7:7-8; Ufunuo 22:15), bila kujali maisha yake ya zamani au kina cha dhambi yake (1 Wakorintho 6:9-11).

Wema dhidi ya Uovu Wahitaji “Hukumu ya haki”
Sehemu nyingine kuu ya mafundisho ya Biblia kuhusu “wema na uovu” ni kwamba hakuna mtu asiyekosea, hata katika mambo ya kiroho. Wale wanaoongozwa na Roho Mtakatifu wameandaliwa vyema zaidi kuhukumu mambo ya kiroho (1 Wakorintho 2:14), na wanapaswa kufanya hivyo. Maandiko yako wazi kwamba watu wote wako chini ya dhambi, na vile vile ni wazi kuwa watu wote wako chini ya adhabu (Waebrania 12:5-11), kujifunza (2 Timotheo 2:15), na mapungufu (1 Samweli 16:7).

Katika Mathayo 7 Yesu anatoa maelezo ya kina ya jinsi ya kupambanua kati ya mema na mabaya ipasavyo: “Hukumu” njia inayostahili; hiyo ni kutumia “hukumu iliyo sawa” (Yohana 7:24). Biblia inahimiza kujihoji (Matendo 17:11), inaamrisha kuweka kila kitu katika jaribu (1 Yohana 4:1), na inakuza uwajibikaji (1 Petro 3:15) na kujitolea kwa ukweli (Wagalatia 1:8-9).

Maandiko hayamaanishi kwamba “wema dhidi ya uovu” ni rahisi na dhana jozi. Kwa kuwa ni Mungu tu pekee ambaye ndiye mkamilifu, biblia inaruhusu mpangilio wa “wema dhidi ya bora.” Mungu aliita uumbaji wake wa mwanzo kuwa “mzuri” (Mwanzo 1:24), kisha baada ya kuumba zaidi akasema ni “mzuri sana” (Mwanzo 1:28). Baadhi ya vitu vizuri ambavyo Mungu ametupa vina matumizi zaidi ya moja, na sio matumizi yote moja kwa moja ni mazuri au mabaya (1 Timotheo 4:4). Ufahamu wa kibiblia wa mema dhidi ya mouvu haumaanishi kwamba vitu vyote kikamilifu ni vitakatifu, au ni vya kishetani kabisa. Badala yake, kunaweza kuwa na mambo mazuri na mabaya ya uhuru mwingi ambao Mungu anatupa (1 Wakorintho 6:12). Vivyo hivyo, ingawa dhambi zote husababisha kutengana na Mungu, Maandiko yanazungumzia juu ya dhambi zingine kuwa mbaya zaidi kuliko zingine.

Biblia inakubali kwamba sio kila wakati katika maisha ya mwanadamu jibu litakua kwa njia ya wazi. Maandiko yanazingatia tu mambo muhimu zaidi tunayohitaji kujua, sio kila hali inayoweza kuwaziwa (Yohana 21:25). Hii ina maana hata Wakristo waaminifu zaidi, wanaoamini biblia, waliozaliwa mara ya pili wanaweza kutokubaliana juu ya swali la kimaadili (1 Wakorintho 10:23-33). Jibu la Biblia-wakati suala haliangaziwa kwa uwazi katika Neno la Mungu (1 Wakorintho 5:6)-ni kwa ajili ya uvumilivu na subira (Tito 3:9). Tumepewa dhamiri kwa madhumuni (Warumi 14:23).

Ukweli huwa na lengo; kwa maoni yoyote au tafsiri, mtu yuko sahihi, na mtu mwingine ana makosa. Lakini wanadamu wanakosa ukamilifu wa kimaadili wa Mungu; hili limeakisiwa katika fundisho la Biblia juu ya wema dhidi ya uovu na jukumu letu katika kutumia uamuzi mzuri.

Maandiko yanawahimiza waumini kutotumia maneno kama mema, uovu, dhambi na kadhalika kwa masuala ambayo kuna nafasi ya shauku (Warumi 14:1-12). Kinyume na vile wengine wanavyofikiri, Biblia inakubali kwamba hueanda wanadamu wasiwe sahihi nyakati zote katika maamuzi yetu ya kiadili. Hatupaswi kuepuka hukumu zote (Yohana 7: 24), lakini Biblia inatufundisha kwamba tuzingatie kwa makini wakati na jinsi tunavohukumu (Waefeso 5:10).

Wema na Uovu vinahitaji mwitikio
Mafundisho ya Biblia juu ya mema dhidi ya mabaya hutuongoza kuwa na hitimisho lenye changamoto: kwamba kila mtu ana wajibu wa kufanya chaguo la msingi kati ya hayo mawili. Chaguo hilo huamuliwa kabisa na mwitikio wetu kwa Mungu, ambaye ndiye ufafanuzi wa wema na Muumba wetu. Muda baada ya muda, hiyo ina maana kuwa tufuate mapenzi yake au tuasi na kuchagua kutenda dhambi (1 Wakorintho 10:13). Milele, hii inamaanisha tunachagua kumkubali Yeye na wokovu Wake (Yohana 3:16; 14:6) au kusimama dhidi yake (Yohana 3:36). Ingawa tunaweza kuwa si wakamilifu na wenye makosa, hatuwezi kuwa upande wowote katika mtazamo wetu wa wema dhidi ya uovu. Mioyo yetu inatafuta wema wa Mungu (Mathayo 7:7-8; Warumi 2:4) au ubinafsi wa uovu (1 Petro 3:10-12).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu wema dhidi ya uovu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries