settings icon
share icon
Swali

Wazee ishirini na wanne (24) katika Ufunuo wao ni nani?

Jibu


Ufunuo 4: 4 inasema, "Kulikuwa na duara la viti ishirini na vine kukizunguka kiti cha enzi, na juu ya viti hivyo wazee ishirini na wane walikua wameketi wamevaa mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani." Hakuna mahali ambapo Kitabu cha Ufunuo hufafanua hasa wale wazee ishirini na wane ndio nani. Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa wao kuwawakilisha Kanisa. Haiwezekani kwamba wao ni malaika viumbe, kama wengine wanavyopendekeza. Ukweli kwamba wao wanaketi katika viti vya enzi inaonyesha kwamba wao wanatawala pamoja na Kristo. Hakuna katika Maandiko ambapo Malaika wanatawala au kukaa katika viti vya enzi. Kanisa, hata hivyo, linasemwa mara kwa mara kutawala na kutawala na Kristo (Ufunuo 2: 26-27, 5:10, 20: 4, Mathayo 19:28, Luka 22:30).

Kwa kuongeza, neno la Kiyunani lililotafsiriwa hapa kama "wazee" halitumiwi kamwe likirejelea malaika, bali kwa wanadamu peke yake, hasa kwa wanaume wa umri fulani ambao wamekomaa na wanaoweza kusimamia/kuongoza Kanisa. Kwa hivyo neon mzee itakua makosa likirejelea malaika, ambao hawazwwki. Mfumo wao wa mavazi pia unaonyesha kuwa hawa ni wanadamu. Huku malaika wakionekana katika mavazi meupe, nguo nyeupe hupatikana kwa waumini pia, ikiashiria haki ya Kristo inayohesabiwa kwetu wakati wa wokovu (Ufunuo 3: 5,18; 19: 8).

Taji za dhahabu zinazovaliwa na hawa wazee pia zinaonyesha kuwa hawa ni wanadamu, si malaika. Malaika hawajahaidiwaahidi kamwe taji, wala malaika hawajawahi onekana wakiwa wamevaa taji. Neno lililotafsiriwa "taji" hapa linamaanisha taji ya mshindi, huvaliwa na wale ambao wamefanikiwa kushinda na kushinda ushindi, kama Kristo alivyoahidi (Ufunuo 2:10, 2 Timotheo 4: 8, Yakobo 1:12).

Watu wengine wanaamini kwamba wazee ishirini na wanne wanawakilisha Waisraeli, lakini wakati wa maono haya, Israeli kama taifa zima halikuwa limekombolewa. Wazee hawawezi kuwakilisha watakatifu wa dhiki kwa sababu sawia-sio wote walikuwa wameokolewa wakati wa maono ya Yohana. Chaguo kubwa linalokisiwa ni kwamba wazee wanawakilisha Kanisa lililonykuliwa ambao huimba nyimbo za ukombozi (Ufunuo 5: 8-10). Wao wanavaa taji za ushindi na wameenda mahali walioandaliwa na Mwokozi wao (Yohana 14: 1-4).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Wazee ishirini na wanne (24) katika Ufunuo wao ni nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries