settings icon
share icon
Swali

Je! Watu wengi wataenda mbinguni au kuzimu?

Jibu


Swali la kuwa ikiwa kuna watu wengi mbinguni au Jahannamu linajibiwa na Yesu mwenyewe katika kifungu kimoja kifupi na dhahiri: "Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimuni, nao waionao ni wachache"(Mathayo 7: 13-14).

Ni wale tu wanaompokea Yesu Kristo na ambao wanaamini ndani yake wanapewa haki ya kuwa watoto wa Mungu (Yohana 1:12). Kama hivyo, zawadi ya uzima wa milele inakuja tu kwa njia ya Yesu Kristo kwa wote wanaoamini. Alisema, "Mimi ndimi njia, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi"(Yohana 14: 6). Si kupitia Mohammed, Budha, au miungu mingine ya uongo ya kufanywa na mtu. Sio kwa wale wanaotaka njia rahisi kuenda mbinguni wakati wanaendelea kuishi maisha ya kidunia ulimwenguni. Yesu anaokoa tu wale wanaomwamini kikamilifu kama Mwokozi (Matendo 4:12).

Kwa hivyo, malango haya mawili katika Mathayo 7: 13-14 ni nini? Ni malango ya kuingia "njia" mbili tofauti. Lango pana linaelekeza kwa njia pana. Na ndogo, lango nyembamba linaelekeza kwa njia ambayo ni nyembamba. Njia nyembamba ni njia ya wacha Mungu, na njia pana ni njia ya wasiomcha Mungu. Njia pana ni njia rahisi. Ni ya kuvutia na inakuza kujipendeza. Na inaruhusu. Ni njia ya umoja ya ulimwengu, yenye sheria chache, vikwazo vichache, na mahitaji machache. Stahamala ya dhambi huendelezwa, na Neno la Mungu halifunzwi na viwango vyake havifuatwi. Njia hii haihitaji ukomavu wa kiroho, hakuna tabia ya maadili, hakuna kujitolea, na hakuna dhabihu. Ni njia rahisi kufuata "ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi" (Waefeso 2: 2). Ni njia hiyo pana ambayo "Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti" (Methali 14:12).

Wale wanaohubiri injili ya pamoja ambako "njia zote huelekea mbinguni" huhubiri injili tofauti kabisa kuliko ile ambayo Yesu alihubiri. Lango la kujifikiria mwenyewe, kujifyonza mwenyewe, na mwenye kiburi, mtazamo wa mtakatifu-kuliko-wote ni lango kubwa la ulimwengu linaloongoza kwenye kuzimu, sio lango nyembamba linaloongoza kwa uzima wa milele. Watu wengi hutumia maisha yao kufuata umati ambao wako katika barabara pana, kufanya kile ambacho kila mtu mwingine anafanya na kuamini kile kila mtu anaamini.

Njia nyembamba ni njia ngumu, njia inayohitaji. Ni njia ya kutambua kwamba huwezi kujiokoa mwenyewe na lazima utegemee Yesu Kristo pekee ili akuokoe. Ni njia ya kujikana mwenyewe na msalaba. Ukweli kwamba watu wachache hupata njia ya Mungu inamaanisha kuwa ni lazima itafutwe kwa bidii. "Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote" (Yeremia 29:13). Hatua ni hii kwamba hakuna mtu atakayejikwaa ndani ya ufalme au kuzurura kupitia lango nyembamba kwa ajali. Mtu mmoja alimwuliza Yesu, "je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akamwaambia, jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze" (Luka 13:23-24).

Wengi watatafuta kuingia huo mlango mwembamba, mlango wa wokovu, lakini "hawataweza." Hawataki kumwamini Yesu pekee. Hawataki kulipa thamani. Itawagharamu vikubwa sana kwao kuacha dunia. Njia ya Kristo ni njia ya msalaba, na njia ya msalaba ndiyo njia ya kujikana mwenyewe. Yesu alisema, "Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha" (Luka 9: 23-24).

Yesu anajua kwamba wengi watachagua lango pana na njia pana inayoongoza kwenye uharibifu na kuzimu. Vile vile, alisema kuwa ni wachache pekee watakaochagua lango nyembamba. Kulingana na Mathayo 7: 13-14, hakuna shaka kwamba zaidi wataenda kuzimu kuliko mbinguni. Swali kwako ni, basi, ni barabara gani uko?

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Watu wengi wataenda mbinguni au kuzimu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries