settings icon
share icon
Swali

Je, kuna watu weusi waliotajwa katika Biblia?

Jibu


Tunaweza kusema kwa kiwango cha uhakika ya kwamba, ndiyo, Biblia inataja watu weusi, ingawa Biblia haitambui wazi mtu yeyote kuwa mwenye ngozi nyeusi. Pia, Biblia haitambui mtu yeyote kama mwenye ngozi nyeupe. Rangi ya ngozi ya mtu haijatajwa sana katika Biblia; rangi ya ngozi ya mtu haina maana kwa ujumbe wa msingi wa Biblia.

Hadithi nyingi za Biblia zinafanyika katika Mashariki ya Kati, ndani na karibu na Israeli. Watu "weusi" na "weupe" sio wengi katika mikoa hii. Watu wengi katika Biblia ni wa Kisemiti na wangekuwa rangi ya maji ya kunde. Hatimaye, haijalishi rangi ya ngozi watu wa Biblia walikuwa na nayo.

Wasomi wengine wanadhani kwamba mke wa Musa, Zippora, alikuwa mweusi kwa sababu alikuwa Mkushi (Hesabu 12: 1). Kushi ni jina la kale la eneo la Afrika. Shulammite inawezakana alikuwa mweusi (Wimbo Ulio bora wa Sulemani 1: 5), ingawa muktahdha unaonyesha kwamba ngozi yake ilikuwa nyeusi kutokana na kufanya kazi kwenye jua. Wengine hupendekeza kwamba Bathsheba (2 Samweli 11: 3) alikuwa mwenye ngozi nyeusi. Wengine wanaamini kwamba Malkia wa Sheba aliyemtembelea Sulemani (1 Wafalme 10: 1) alikuwamwenye ngozi nyeusi. Simoni wa Kurene (Mathayo 27:32) inawezekana ali kuwa mwenye ngozi nyeusi, na pia "Simeoni aitwaye Nigeri" katika Matendo 13: 1. Mtumwa wa Ethiopia huko Matendo 8:37 alikuwa wa ngozi nyeusi. Waethiopia wanatajwa mara 40 katika Biblia, na tunaweza kudhani kwamba haya ni marejeleoo kwa watu weusi, kwa kuwa Waethiopia ni watu wa ngozi nyeusi. Nabii Yeremia aliuliza, "Je! Mtiopiya anaweza kubadili ngozi yake?" (Yeremia 13:23) — Dhana ya asili ni kwamba Yeremia anaelezea ngozi nyeusi.

Wengi wa walimu wa Biblia wanaamini kwamba watu wa rangi nyeusi ni wazao wa Nuhu, mwana wa Hamu (Mwanzo 10: 6-20), lakini hatuwezi kuwa na hakika kwa kuwa Biblia haswa haielezei, Biblia mara kwa mara iko kimya kwa mambo ya rangi ya ngozi. Rangi ya ngozi si muhimu kwa Mungu kama hali ya moyo. Injili ni habari njema ya ulimwengu wote. Watu wenye ngozi nyeusi, watu wenye ngozi nyeupe, na walio kati ya rangi hizi mbili wanaalikwa kuja kwa Kristo kwa ajili ya wokovu. Kwa neema ya Mungu tunaweza kuchukua macho yetu mbali na ngozi na kuzingatia roho.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kuna watu weusi waliotajwa katika Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries