settings icon
share icon
Swali

Kwanini inaonekana kwamba Mungu hajali kuhusu watoto walio na njaa ulimwenguni?

Jibu


Watu wengine humlaumu Mungu kwa sababu ya idadi ya watoto walio na njaa ulimwenguni, huku wakimtuhumu kwa kukosa uwezo au utunzaji ambao anapaswa kuwa nao. Ni ukweli kwamba njaa ni tatizo kwa wengi ulimwenguni na watoto wengi wanakabiliwa na utapiamlo. Shirika la Compasion International inaripoti kuwa zaidi ya watoto milioni tatu hufa kila mwaka kutokana na utapiamlo. Katika nchi zinazoendela , asilimia 25 ya watoto wana uzito duni na wako katika hatari ya kuwa na athari za muda mrefu kutokana na ukosaji wa lishe bora. Shida hili ni halisi lakini Biblia inatufunza kwamba upendo wa mungu ni halisi pia.

Mungu ametupatia maarifa, kidokozi na majibu tayari katika neno lake, Biblia, kwa kila swali tunaweza kuwa nalo kumuhusu. Yesu alifunza kwamba watoto ni wa muhimu kwake Mungu. "Na yeyote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi; bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.(Mathayo 18:5-6). Halafu katika mstari wa 10, Yesu alisema, "Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote hutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni."

Ukweli ni kwamba Mungu anajali.

Shirika za msaada na watenda kazi wa serikali wanakubali kwamba kuna chakula kingi duniani cha kulisha kila mtu. Shida sio ukosefu wa chakula lakini ni kukosa uwezo wa kukipata chakula. Basi kwa hivyo kuna chakula cha kutosha kulisha idadi ya watu duniani basi makosa sio ya Mungu. Badala yake, kosa liko katika asili ya ufisadi ya mwanadamu. Badala ya kuwa wasimamizi wa kuaminika wa rasilimali za ulimwengu, mataifa na watu binafsi mara nyingi huweka akiba ya chakula kwa uchoyo, hutumia rasilimali vibaya, na kutumia pesa vibaya badala ya kuhakikisha kwamba watu wanapata chakula.

Mungu hawajibiki kwa sababu ya ujinga wa mwanadamu. Wala sio yeye anayehusika kwa uchoyo, ubinafsi, chuki, kiburi, uvivu, kuweka akiba kwa uchoyo, ukatili, ukorofi, kukosa huruma, ama dhambi zinginezo ambazo huchangia kuwepo kwa njaa ulimwenguni. Ndani yake Mungu hamna udhalimu (Zaburi 92:15). Watu wote ni wenye dhambi(Warumi 3:23), na "mshahara wa dhambi ni mauti" (Warumi 6:23). Majanga ya ulimwengu- haswa yanayoweza kuzuiwa kama vile njaa duniani- ni matokeo ya dhambi (ona Warumi 8:28).

Mungu huwajali watoto kote ulimwenguni. Alithibitisha utunzaji wake kwa vile alimtuma Mwanawe duniani ili atukomboe kutoka kwa laana ya dhambi. "Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa njia yake" (1 Yohana 4:9).

Mungu pia anaonyesha utunzaji wake kwa kuwa anawahimiza wafuasi wa Kristo kusaidia kumaliza njaa ulimwenguni. Mungu anafanya kazi kulisha walio na njaa ulimwenguni kupitia mashirika mengi ya Kikristo — Compassion International, World Vision, World Help, Feed the Hungry, Samaritan's Purse- na mengineo. Wamishonari Wakristo ulimwenguni kote wanasaidia watu na mahitaji yao ya msingi na wakati huo huo wanawafunza Neno la Mungu. Wanfanya hivyo kwa upendo wao kwa Mungu na kwa watu pia. Wanafanya hivyo kwa maana "tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema" (Waefeso 2:10).

Mungu ni mwema wakati wote. Lakini mara nyingi inashusha moyo kuona uovu na mateso ulimwenguni. Tunajua kwamba uovu haupo kwa sababu yake Mungu lakini kwa sababu ya shetani, dhambi na hali ya kuanguka kwa mwanadamu. Hatuachi kutumaini. Tunapata kuweza "kushinda siku ya uovu" (Waefeso 6:13). Tunapenda majirani wetu jinsi tunavyojipenda, kwa sababu yake Yeye "aliyependa ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee" (Yohana 3:16). Siku moja, Bwana wetu atafanya mambo kuwa sawa, na "wala hapatakuwa na laana yoyote tena" (Ufunuo 22:3)

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwanini inaonekana kwamba Mungu hajali kuhusu watoto walio na njaa ulimwenguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries