settings icon
share icon
Swali

Je! Watoto wanapaswa kubatizwa katika umri gani na / au kuruhusiwa kushiriki Meza ya Bwana?

Jibu


Huku makanisa mengine yakiwahitaji watoto darasa za Biblia kwa maagizo ya kanuni na maana ya amri kabla waruhusiwe kushiriki, mengine mengi hawaitaji. Iwe hali yoyote, ni vyema kwa wazazi kuwaelekeza na kuwatayarisha watoto wao kwa ubatizo na meza ya Bwana. Hatimaye mafundisho ya watoto katika njia za Mungu ni jukumu la wazazi, na kanisa liko kusaidia tu.

Kabla ya kushiriki meza ya Bwana, sharti kuu kwa watoto (kama ilivyo kwa watu wakubwa) ni kwamba wamempokea Bwana Yesu Kristo kama Mwokozi wao. Hata kama watoto wengine wanafanya uamuzi huu wa wokovu wakiwa na umri mchanga, ubatizo na kushiriki meza ya Bwana havifai kuharakishiwa. Mto anapokomaa katika imani ni imedhihirika kwamba amezaliwa mara ya pili, baba/mama yake anapaswa kuwa mwangalifu kujua ni lini mtoto ako tayari kuelewa na kushiriki meza ya Bwana. Kiwango cha ukomavu wa kiroho cha mtoto mmoja kinatofautiana na kile cha mtoto mwingine, hata katika familia moja.

Katika makanisa mengi, wakati wazazi wa mtoto wanamjulisha mchungaji kuwa mtoto wao anataka kubatizwa, mchungaji anasungumza na mtoto mwenyewe kuamua ikiwa kweli mtoto huyo yuko tayari. Hili ni tendo bora na la busara. Ni muhimu sana mtoto akumbuke kuwa ubatizo au meza ya Bwana havimwokoi, badala yake hizi ni hatua za utiifu na ukumbusho wa kile Yesu alitufanyia katika kutoa wokovu wetu (Luka 22:19).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Watoto wanapaswa kubatizwa katika umri gani na / au kuruhusiwa kushiriki Meza ya Bwana?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries