settings icon
share icon
Swali

Je! Tunapaswa kutii wachungaji wetu?

Jibu


Mstari unaozungumzia moja kwa moja swali hili ni Waebrania 13:17, "Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea, maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi. "

Wachungaji wanaumia kwa undani kuona watu wanapuuza shauri la Mungu wanayoshiriki. Wakati watu wanapuuza Neno la Mungu, hufanya hivyo sio tu kwa madhara yao wenyewe bali pia kwa kuvunja desturi za wale walio karibu nao. Vijana wana tabia ya kupuuza shauri la wazee wao, wakifanya kosa la kuamini hekima zao wenyewe na shauri la moyo wao wenyewe. Mchungaji wa kimungu anashiriki maagizo kutoka kwa Neno la Mungu kwa sababu anatamani kumtumikia Mungu na kulisha kundi chakula cha kiroho ambacho kitasababisha maisha yao mengi ambayo Yesu aliahidi (Yohana 10: 10b).

Kinyume cha mchungaji wa kimungu ni "mchungaji wa uongo" ambaye hana maslahi ya kundi kwa moyo lakini ana hamu zaidi ya kudumisha udhibiti au kutumia utawala juu ya wengine, au ambaye amefeli kujifunza Neno la Mungu na kwa hivyo hufundisha amri za wanadamu badala za Mungu. Mafarisayo wa wakati wa Yesu walikuwa na hatia ya kuwa "viongozi vipofu" (Mathayo 15:14). Na kuna maonyo mara kwa mara juu ya walimu wa uongo katika Matendo, Mabarua, na Ufunuo. Kwa sababu ya kuwepo kwa viongozi hawa wa kujitafuta wenyewe, kunaweza kuwa na wakati ambapo tunakosa kumtii mwanadamu ili kumtii Mungu (Matendo 4: 18-20). Hata hivyo, mashtaka dhidi ya kiongozi wa kanisa haipaswi kufanywa kwa urahisi na inahitaji kuthibitishwa na shahidi zaidi ya mmoja (1 Timotheo 5:19).

Wachungaji wa Mungu wana thamani ya uzito wao katika dhahabu. Kwa kawaida huwa na kazi nyingi na hulipwa kwa kiwango cha chini. Wao hubeba wajibu mkubwa, kama Waebrania 13:17 inasema — lazima siku moja watatoa hesabu ya huduma zao mbele za Mungu. 1 Petro 5: 1-4 inasema kwamba hawapaswi kutawala kimabavu, bali wanapaswa kuongoza kwa mfano wao na mafundisho mazuri (1 Timotheo 4:16) kwa unyenyekevu wa moyo. Kama Paulo, wanapaswa kuwa kama mama wauguzi ambao wanawapenda watoto wao kweli. Wachungaji wa kimungu wana nia ya kujitoa kwa kundi lao na kutawala kwa upole (1 Wathesalonike 2: 7-12; Yohana 10:11). Wana sifa ya kujitolea kwa kweli kwa Neno na kwa sala (Matendo 6: 4) ili waweze kutawala kwa nguvu na hekima ya Mungu na kupa kanisa nyama ya kiroho ili kuzalisha Wakristo wenye afya na wenye nguvu. Ikiwa haya ndiyo maelezo ya mchungaji wako, au yanakaribia (hakuna mtu hapa duniani ni mkamilifu), anastahili "heshima maradufu" na utii kama anavyotangaza mafundisho wazi ya Mungu (1 Timotheo 5:17).

Hivyo jibu la swali ni, ndiyo, tunapaswa kutii wachungaji wetu. Pia tunapaswa kuwaombea daima, tukimwomba Mungu awape hekima, unyenyekevu, upendo wa kundi, na ulinzi wakati wanawalinda wale wanaowajali.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tunapaswa kutii wachungaji wetu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries