settings icon
share icon
Swali

Je, "kutendea wengine kama ungependa wakutendee" ni kauli ya kibiblia?

Jibu


"Watendee wengine kama unavyotaka wakutendee," inayojulikana kama "Kanuni ya kuu," ni kwa kweli kanuni ya kibiblia. Luka 6:31 Yesu anasema, "Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo." Maneno haya ni katika maudhui ya somo kutoka kwa Yesu kuhusu kupenda adui wetu. Yesu kwa kiasi kikubwa alibadili njia ya kawaida ya njia ya kushiriki na watu (tazama Mathayo 5: 38-48). Badala ya kuwafanyia wengine yale waliyotutendea au kuwapa yale wanayostahili, tunapaswa kuwafanyia yale tunayotaka watutendee.

Katika Mathayo 7:12 Yesu anasema, "Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii." Hivyo basi kanuni hii bora imekuwa daima sehemu ya msingi ya ujumbe wa Biblia. Baadaye katika Mathayo, alipoulizwa amri kuu zaidi, Yesu alijibu, "'Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.' Hii ndiyo amri ya kwanza na kuu zaidi. Na ya pili ni hii: "Mpende jirani yako kama nafsi yako." Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.

"(Mathayo 22: 37-40). Usiku wa kukamatwa kwake, Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Amri mpya nawapa: Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi."(Yohana 13: 34-35). Upendo wa Yesu kwetu ni kamilifu, haubadiliki, na niwakujitolea. Uwezo wetu wa kupenda wengine jinsi Yesu anavyoamuru huja tu kutokana na uzoefu wetu wa upendo Wake na kutoka kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Njia moja ya vitendo ya kupenda wengine vizuri ni kujiweka wenyewe katika hali yao. Tunapofikiria jinsi tunavyopenda kutendewa katika hali fulani, tunawajali wale wanaoishi katika hali hiyo. Je! Tunapenda kutendewa kwa upendo na heshima? Basi tunapaswa kuwapa wengine zawadi hiyo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, "kutendea wengine kama ungependa wakutendee" ni kauli ya kibiblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries