settings icon
share icon
Swali

Jinsi gani tutajiwasilisha kwa Mungu?

Jibu


Katika matukio yote ya Agano Jipya ambapo neno wasilisha hutokea, neno linatafsiriwa kutoka kwa neno la Kigiriki hupotasso. Hupo ina maana "chini" na tasso inamaanisha "kupanga." Neno hili na mzizi wake pia hutafsiriwa kwa maneno kutii na kugandamizwa. Maana kamili ya neno ni "kutii, kuweka chini, kupaswa kutii, kujiwasilisha mwenyewe, kuweka katika chini ya kugandamizwa au kuwa chini ya utii au utiifu." Neno lilitumiwa kama neno la kijeshi linalomaanisha "kupanga mgawanyiko wa vikosi vya wanajeshi kwa njia ya kijeshi chini ya amri ya kiongozi." Neno hili ni ufafanuzi wa ajabu wa nini maana ya "kuwasilisha" kwa Mungu. Ina maana ya kujipanga mwenyewe chini ya amri ya mtazamo wa Mungu badala ya kuishi kulingana na njia ya mtu ya zamani kulingana na mtazamo wa kibinadamu. Ni mchakato wa kusalimisha mapenzi yetu yenyewe kwa yale ya Baba wetu.

Maandiko ina mengi ya kusema juu ya kujiwasilisha kwa "mamlaka ya juu." Hii ina maana ya kanuni zilizoanzishwa ambazo Mungu ameamuru katika ulimwengu wetu-serikali na viongozi, katika nafasi yoyote, ambayo Mungu ameweka mamlaka juu yetu hapa duniani. Vifungu vinavyofundisha kanuni hii ni Warumi 13:1-7; Waebrania 13:17; 1 Petro 2:13-14; na Tito 3:1. Kanuni ni kwamba kuwa katika utii kwa mamlaka juu yetu, chochote kile mamlaka hayo iko, italeta baraka za muda kwa wakati halisi hapa na sasa na, kwa ajili ya muumini, thawabu baadaye. Mamlaka ya juu ni Mungu, na huwapa mamlaka kwa wengine; hivyo, ili kujiwasilisha kwa Mungu, tunajiwasilisha kwa mamlaka aliyoweka juu yetu. Utaona kuwa hakuna tahadhari ambayo inatofautisha kati ya mamlaka mema au mabaya au hata mamlaka ya haki au yasiyo ya haki. Sisi tu ni kunyenyekea wenyewe na kutii kama "kwa Bwana."

Tunaambiwa pia kujiwasilisha wenyewe kwa Mungu (Yakobo 4:7). Katika Waefeso tunasoma kwamba Wakristo wanapaswa kuwasilisha "hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo" (Waefeso 5:21). Pia tunasoma kwamba mke anapaswa kujiwasilisha kwa mumewe kama kwa Bwana na mume anapaswa "kumpenda" mkewe (Waefeso 5:22-25). Mtume Petro anaandika, "Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema" (1) Petro 5:5). Dhamira hapa ni moja ya unyenyekevu. Mtu hawezi kujiwasilisha kwa Mungu bila unyenyekevu. Utii unahitaji sisi kujinyenyekeza wenyewe kujisalimisha kwa mamlaka ya mwingine, na tunaambiwa kwamba Mungu anakataa kiburi-kinyume cha unyenyekevu-na majisifu ambayo yanakuza kiburi.

Kwa hivyo, kuwa na moyo mnyenyekevu na wa kutii ni chaguo tunalofanya. Hiyo ina maana kama waumini wazaliwa tena kila siku tunafanya uchaguzi wa kujiwasilisha wenyewe kwa Mungu kwa kazi ambayo Roho Mtakatifu hufanya ndani yetu "kutupatanisha na sura ya Kristo." Mungu atatumia hali ya maisha yetu kutuletea fursa ya kujiwasilisha Kwake (Warumi 8:28-29). Muumini basi anakubali neema Yake na utoaji wa kutembea katika Roho na si kwa njia ya asili ya zamani. Kazi hiyo imekamilika kwa kuchagua kujitumia wenyewe kwa Neno la Mungu na kujifunza kuhusu masharti ambayo Mungu ametufanyia katika Kristo Yesu. Kutoka wakati tunazaliwa tena, tuna masharti yote tunayohitaji, katika Kristo, kuwa muumini amekomaa, lakini tunapaswa kufanya uchaguzi wa kujifunza juu ya masharti hayo kwa kujifunza Neno na kutumia maagizo hayo kwa matembezi yetu ya kila siku.

Tunapaswa kuchagua kujiwasilisha kwa Mungu kwa mchakato wa kujifunza ili kukua kiroho. Ni mchakato unaoanza katika wokovu na kuendelea na kila chaguo tunayofanya ili kujiwasilisha wenyewe kwa Mungu. Utaratibu huu utaendelea mpaka Bwana atakaporudi tena au Kutuita nyumbani. Jambo la ajabu juu ya hili ni kwamba, kama vile Mtume Paulo anasema vizuri, "Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho"(2 Wakorintho 3:18).

Mungu hahitaji sisi kujiwasilisha kwa sababu yeye ni mudhalimu, lakini kwa sababu Yeye ni Baba mwenye upendo na anajua kile kinachofaa kwetu. Baraka na amani tunayopata kutokana na kujisalimisha kwa unyenyekevu na kujiwasilisha wenyewe Kwake kila siku ni zawadi ya neema ambayo ulimwengu huu unaweza kulinganisha.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Jinsi gani tutajiwasilisha kwa Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries