settings icon
share icon
Swali

Je, wanyama rafiki pia huenda mbinguni? Je, wanyama rafiki wana roho?

Jibu


Biblia haitufundishi juu ya wanyama kama wana roho ama wataenda mbinguni.lakini tunaweza kutumia kanuni za biblia kuangazia swala hili. Biblia inasema kuwa wanadamu (mwanzo 2:7) na wanyama (mwanzo 1:30; 6:17; 7:15,22) wote wana pumzi ya uhai. Wanyama wakuumbwa katika mfano wa Mungu. Kwa kuumbwa kwa mfano wa Mungu, inamaana ya kuwa wanadamu ni kama Mungu, wana roho, akili, hisia, na uamuzi na pia wana hali ya kudumu hata baada ya kifo. Kama wanyama wana roho basi lazima iwe ni duni kuliko ya wanadamu. Na kwa sababu hii basi wanyama hawana hali ya kudumu hata baada ya kifo.

Jambo lengine la kutazama ni kwamba wanyama Mungu aliwaumba sawa na viumbe vyengine katyika kitabu cha mwanzo. Mungu aliwaumba wanyama na akasema ni wazuri (mwanzo 1:25). Kwa hivyo hakuna sababu ya kusiweko na wanyama katika dunia mpya (ufunuo wa Yohana 21:1). Kutakuwako na wanyama katika miaka elfu moja ya kutawala kwake kristo (Isaya 11:6; 65:25). Ni vigumu kujua kama wanyama hawa tutakaowaona watakuwa ni hawa tuliokuwa nao katika nyakati hizi tunazoishi. Tunajua Mungu ni wa haki na tutakapofika huko tutajipata katika hali ya kuridhika na mipango yake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, wanyama rafiki pia huenda mbinguni? Je, wanyama rafiki wana roho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries