settings icon
share icon
Swali

Mwanamke anastahili kumtii mume wake?

Jibu


Kutii ni jambo la muimu sana kwa mjibu wa ndoa. Hata kabla ya dhambi kuingia katika ulimwengu, kulikuwa na kanuni ya ukubwa/uongozi (1 Timotheo 2:13). Adamu aliumbwa kwanza, na Hawa akaumbwa kuwa “msaidizi” wa Adamu (Mwanzo 2:18-20). Kwa wakati huo huo, kwa vile hakukuwa na dhambi, hakukuwa na utawala mwanadamu kutii ila tu ni utawala wa Mungu. Wakati Adamu na Hawa walimuasi Mungu, dhambi ikaingia ulimwengu, na hapo mamlaka yakahitajika ili yatekeleze sheria za nchi na pia kutupa kinga tunayohitaji. Kwanza, tunastahili kumtii Mungu, ambayo ndio njia pekee tutakayo mtii (Yakobo 1:21; 4:7). Katika 1 Wakorintho 11:2-3, tunapata kuwa, mwanamume anastahili kumtii Kristo, vile Kristo alivyo mtii Mungu. Tena aya hii yasema kuwa mke anastahili kufuata mfano wake na kumtii mume wake.

Kutii ni jukumu la kimaumbile kwa uongozi wa kupendeza. Wakati mume anampenda mke wake vile Kristo analipenda kanisa (Waefeso 5:25-33), kwa hivyo kutii ni jukumu la kimaumbile kutoka kwa mke hadi kwa mume wake. Neno la Kiyunani ambalo limefasiriwa “kutii,” hupotasso, ni uendelezo wa kitenzi. Hii yamaanisha kumtii Mungu, serikali, au mume si tendo la mara moja. Ni nia inayoendelea, ambayo itakuwa mtindo wa tabia. Utiifu unaozungumziwa katika Waefeso 5 sio wa sehemu moja kunyenyekea kwa mtu mchoyo anayetaka kutawala. Utiifu wa Kibibilia umepangwa kuwa Wakristo wawili wamejazwa kwa Roho Mtakatifu ambao wamejitolea kwa wao wenyewe na kwa Mungu. Utiifu ni wa namna mbili, kupokea na kupatiana. Utiifu ni hali ya heshima na ukamilifu. Wakati mwanamke amependwa vile Kristo alivyolipenda Kanisa, utiifu sio jambo ngumu. Waefeso 5:24 yasema, “Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.” Aya yasema kuwa mke anastahili kumtii mume wake kwa kila jambo ambalo ni njema na la kisheria. Kwa hivyo, mwanamke kwa vyovyote vile hana chaguo lingine la kutomtii sheria au Mungu kwa kisingizio kuwa anatii.

Matthew Henry aliandika: “Mwanamke aliumbwa kutoka kwa ubafu wa Adamu. Hakuumbwa kutoka kwa kichwa chake ili amtawale, au kutoka kwa miguu yake ili akanyagigwe chini, lakini kutoka kwa ubafu wake ili awe kiwango kimoja naye, chini ya mabawa zake ilie akingwe, na karibu na moyo wake ili apendwe.” Wakristo wanastahili kuwa na utiifu kwa wao wenyewe kwa kumcha Kristo (Waefeso 5:21). Katika mkudhata huo kila kitu katika Waefeso 5:19-33 ni kwa mjibu wa kujazwa kwa Roho. Wakristo waliojazwa kwa Roho wanastahili kuwa watu wa kuabudu (Waefeso 5:19), wenye shukrani (Waefeso 5:20) na watiifu (Waefeso 5:21). Paulo baadaye anayafuatisha mawazo yake kuwa katika kuisha maisha ya kujazwa kwa Roho yanawapasa mume na mke katika aya ya 22-23. Mke lazima amtii mume wake, sio kwa sababu hivyo ndivyo Mungu alipanga uhusiano wa ndoa uwe ukifanya kazi hivyo. Utiifu sio mwanamke “kushinda kwa nyumba” kwa sababu ya mume wake. Ile hali kwa usaidizi wa Roho Mtakatifu, mwanamke anamtii mume wake na mwanamume kwa juhudi zote anampenda mke wake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mwanamke anastahili kumtii mume wake?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries