settings icon
share icon
Swali

Je! Wanawake wanapaswa kukoma kuwafunza wavulana kanisani?

Jibu


Kupata historia kamili, tafadhali soma nakala zetu juu ya wachungaji wanawake na wanawake katika huduma. Ikiwa hitimisho ni kwamba wanawake hawapaswi kufundisha, kuwa na mamlaka ya kiroho juu ya wanaume, au kuwachunga kanisani ni jambo sahihi kibiblia, na tunaamini ni hivyo ndivyo ilivyo, swali basi linaibuka: Je! Ni katika umri gani mtu wa kiume anachukuliwa kuwa mwanamume?

Je! wanawake wanaweza kutumika kama viongozi wa makundi ya vijana? Wanawake wanaweza kufundisha somo la Biblia au darasa la Jumapili ambalo linajumuisha vijana wanaume? Je! sembuse darasa hilo analiongoza na mwanaume akiwa na mwanamke? Haya ni maswali ambayo kwamba Biblia haitupi jibu kamili.

Biblia haizungumzi moja kwa moja swali la mwanamke kuwafundisha vijana wavulana au ni lini kijana anakuwa mwanamume. Katika Agano la Kale, umri wa miaka 20 ulionekana kuwa wa kutosha kutumika katika jeshi na kuhesabiwa katika hesabu ya idadi ya watu (Hesabu 1: 3) —kwa hivyo, vijana wadogo wa miaka 20 walichukuliwa kuwa watu wazima. Katika Mishnah, umri wa uwajibikaji wa maadili na kidini uliwekwa kuanzia miaka 13. Lakini hakuna mahali popote ambapo Biblia inataja miaka 20 au 18 au 13 au umri wowote kuwa umri ambao mvulana anakuwa mwanamume.

Biblia ii wazi kuwa nafasi ya kawaida ya "mwalimu" katika kanisa lazima uchukuliwa na mwanaume hasa ikiwa mwanamume huyo yu miongoni mwa wanafunzi. Kuzungumza kwa ujumla, makanisa mengi ambayo yanashikilia dhana ya ukamilishaji wana walimu ambao ni wanaume katika madarasa ambayo vijana wanaume ni wanafunzi. Hii inaonekana kuwa sera nzuri ya kufata, kwa kuwa inajaribu kukwepa uasi wowote wa sheria za Mungu kuhusu wanawake kuwa walizing wa wanaume katika kanisa. Kwa wakati huo huo, sio jambo la Kibiblia kusema hasa kuwa hakuna nafasi mwafaka ya wanawake kufunza wanaume kati ya umri wa 13-18. Fauka ya hayo, wanawake hawajazuiliwa kutokana na kufanya wanafunzi, kuhimiza, kukemea na kutoa mwelekeo kwa wanaume wadogo. "Nifuate vile ninamfuata Kristo" ni kitu ambacho kila Mkristo anapaswa kuiga (1 Wakorintho 11:1).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Wanawake wanapaswa kukoma kuwafunza wavulana kanisani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries