settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu Wakristo kutumikia jeshi?

Jibu


Bibilia inabeba wingi wa habari kuhusu kutumikia jeshi. Huku wingi wa Bibilia ukirejelea jeshi kama analojia, aya nyingi moja kwa moja zahuzisha swali hili. Bibilia hasa haitaji kama mtu anastahili kutumikia jeshi. Kwa wakati huo huo, Wakristo wanakua na uakikisho ya kwamba kuwa mwanajeshi ni jambo ambalo limeeshimika sana katika maandiko yote na jua kwamba huduma kam hiyo inaenda sambamba na mtazamo wa Bibilia.

Mfano wa kwanza wa huduma ya jeshi unapatikana katika Agano La Kale (Mwanzo 14), wakati Loti mpwa Abrahamu alitekwa nyara na mfalme Kedorlaoma wa Elamu, na walioshirikiana nao. Abrahamu aliungana na Loti kusaidia kwa kuwaweka pamoja wanaume 318 wa nyumba yake walijifunza vita na wakawashinda Waalamu. Hapa tunaona jeshi ambalo limejiami na kujuhuzisha katika jukumu muimu-kuokoa na kulinda wasio na hatia.

Baadaye katika historia, taifa la Israeli lilianzisha jeshi la kudumu. Dhana kuwa Mungu alikuwa mpiganaji wao wa uungu na kuwalinda watu wake mbali na ugumu wa jeshi lao huenda ndio ilikuwa sababu ya kuwafanya Waisraeli kuwa na haraka ya kuunda jeshi. Uanzishaji wa jeshi la muda katika Israeli ulitokea baada ya mfumo mgumu wa pamoja ulianzishwa na Saulo, Daudi na Suleimani. Saulo likuwa wa kwanza kuanzisha jeshi la kudumu (1 Samweli 13:2; 24:2; 26:2).

Chenye Saulo alianzisha, Daudi aliendeleza. Akaongeza idadi ya wanajeshi, na akaleta makundu makuu kutoka sehemu zingine ambao walikuwa waaminifu kwake (2 Samweli 15:19-22) na akabadilisha uongozi wa moja kwa moja wa jeshi lake na kuwa wa ule wa amri jeshi mkuu, Yoabu. Chini ya uongozi wa Daudi, Israeli ikawa yenye sheria kali katika sera za kijeshi, ilikubali nchi kama Amoni (2 Samweli 11:1; 1 Mambo Ya Nyakati 20:1-3). Daudi alianzisha mfumo wa kubadilisha vikozi kwa makundi kumi na mawili ya wanaume 24,000 watumikia mwezi mmoja wa mwaka (1 Mambo Ya Nyakati 27). Ingawa uongozi wa Suleimani ulikuwa wa amani, naye pia alilipanua jeshi, akaongeza farasi na wapanda farasi (1 Wafalme 10:26). Jeshi lilisimama liliendela (ingawa liligagwanyika kwa kugwagwanyikwa kwa ufalme baada ya kifo cha Suleimani) hadi mwaka 586 B.C., wakati Israeli (Yuda) ziliangamizwa kama taifa huru kisiasa.

Katika Agano Jipya, Yesu alishangashwa na afisa wa Rumi (afisa aliyesimamia askali mia moja) alimwendea. Jibu la afisa kwa Yesu lilionyesha kuwa alielewa maana ya mamlaka vile vile na Imani yake kwa Yesu (Mathayo 8:5-13). Yesu hakuishutumu kazi yake. Wengi wa wanajeshi ambo wametajwa katika Agano Jipya wanasifiwa kuwa Wakristo, wamcha Mungu, na wanaume wenye maadili mema (Mathayo 8:5; 27:54; Mariko 15:39-45; Luka 7:2; 23:47; Matendo Ya Mitume 10:1; 21:32; 28:16).

Mahali na cheo huenda vimebadilika, lakini jeshi letu lichukuliwe kuwa la maana kama lile la Bibilia. Che cha afisa kilieheshimiwa. Kwa mfano Paulo anamwelezea Epafrodito kama Mkristo mpendwa “asikari pamoja name” (Wafilipi 2:25). Bibilia pia yatumia matamshi ya jeshi kwa kuelezea kuwa mwenye nguvu katika Bwana kwa kuifaa silaha yote ya Mungu (Waefeso 6:10-20), ikijumlisha silaha zote za askari- dirii, ngao, na kisu.

Naam, Bibilia inazungumzia kutumikia jeshi, njia ya moja kwa moja na njia ya pempeni. Wakristo wanaume na wanawake ambao wanatumia nchi kwa maadili mema, ukakamavu, na kwa heshima wakaa kwa amani wakiwa wameakikishiwa kuwa utumishi kwa wote ambao watekeleza imekubalika na kuheshimika na Mungu wetu mkuu. Wale kwa heshima yote watumikia jeshi wastahili heshima na pongezi.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu Wakristo kutumikia jeshi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries