settings icon
share icon
Swali

Wakati wa utulivu ni wakati gani?

Jibu


Muda wa utulivu ni sehemu muhimu ya maisha ya kila siku ya Mkristo, kwa maana ndio wakati anaenda kwenye pahali pa starehe na ya siri (kwa kawaida) nyumbani kwake ambako anaweza kumkaribia Mungu bila vurugu. Wakati wa utulivu ni sehemu ya kila siku inayotengwa kwa mkutano kati ya mwamini na Mungu. Inajumuisha kusoma sehemu ya Biblia anayechagua mwamini na kuomba.

Kila mwamini anahitaji wakati wa utulivu na Bwana. Ikiwa Yesu mwenyewe alihitaji hivyo, basi sisi tunahitaji Zaidi. Yesu mara nyingi alisonga mbali na wengine ili kuwasiliana na Baba Yake mara kwa mara, kama Maandiko yafuatayo yanavyotuambia: " Kisha Yesu akaenda pamoja nao mpaka bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa, hata niende kule nikaombe."(Mathayo 26:36). "Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko." (Marko 1:35). "Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba." (Luka 5:16).

Urefu wa muda wa utulivu haujalishi, lakini ni lazima uwe na muda wa kutosha wa kutafakari juu ya kile kilichosomwa na kisha kuomba juu yake au kitu kingine chochote ambacho huja akilini. Kumkaribia Mungu ni zoezi yenye manufaa, na mara moja zoezi ya muda wa utulivu unapotengenezwa, wakati maalum wa kujifunza na sala unakuwa ni wa kutarajia kwa hamu. Ikiwa ratiba zetu zimejaa sana na tunajisikia kwamba hatuwezi kuchukua muda wa kila siku kukutana na Baba yetu wa mbinguni, basi haina budi kurekebisha ratiba yetu na kuacha kujishugulisha.

Jihadharini: dini zingine za Mashariki ambazo zinafundisha kanuni za kutafakari zinajumuisha maagizo juu ya "kuondo mambo akilini" kwa kuzingatia kurudia sauti au neno fulani. Kufanya hivyo kunampa Shetani fursa ya kuingia na kuharibu mawazo yetu. Badala yake, Wakristo wanapaswa kufuata ushauri wa mtume Paulo katika Wafilipi 4: 8: "Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo."Kujaza akili ya mtu kwa mawazo haya mazuri husaidia kuleta amani na kumpendeza Mungu. Wakati wetu wa utulivu unapaswa kuwa wakati wa mabadiliko kupitia kufanya upya nia zetu (Waroma 12: 2), si kwa njia ya kufuta yaliyo akilini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Wakati wa utulivu ni wakati gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries