settings icon
share icon
Swali

Kwa nini kuna wakanamungu wengi sana?

Jibu


Kabla hatujaweza kujadili ukanaji Mungu, tunahitaji kuifafanua. Kwa mujibu wa tovuti ya ukanaji Mungu, wakanamungu wanajitambulisha wenyewe kwa njia hii: "Ukanaji Mungu si kutoamini katika miungu au kukataa miungu; ni ukosefu wa imani katika miungu." Wale ambao wanatambua kama wakanamungu wanapendelea kusisitiza ukosefu wao wa imani badala ya kukataa kuamini. Wanazingatia ukanaji Mungu kuwa ya akili zaidi kuliko imani katika Mungu. Hata hivyo, ufafanuzi huu unapingana na mtazamo wa ulimwengu wa Biblia, ambao unasema, "Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu …" (Zaburi 14:1; 53:1). Kwa kuwa wakanamungu wanaweza kukubaliana na watu wa imani kwamba kila mwanadamu ana uhuru wa kuchagua kile anachofikiri au anachoamini, tutafafanua ukanaji Mungu hapa kama uchaguzi wa kutoamini katika aina yoyote ya Kiumbe Kikuu kwa kile wanadamu wanaajibikia.

Takwimu zinaonyesha kuwa ukanaji Mungu unaongezeka katika nchi ambazo kihistoria zimekuwa na ushawishi mkubwa wa Kikristo. Takwimu hizi ni pamoja na wale waliolelewa katika nyumba zisizo na Mungu, lakini pia huonyesha ongezeko la kutisha kati ya wale ambao mara moja walishikilia aina fulani ya imani ya kidini. Tunaposikia habari ya kiumbe maarufu katika Ukristo kukataa imani aliyokuwa akidai, tunaachwa tukistaajabu, "Kwa nini?" Kwa nini watu wengi wanaacha kuamini katika Mungu wakati kazi ya mikono yake iko kila mahali (Zaburi 19:1; 97:6; Warumi 1:20)? Kila utamaduni duniani unatambua aina fulani ya uungu, basi kwa nini watu wengi wanadai kuwa hawaamini katika mungu yoyote kabisa?

Kuna sababu kadhaa ambazo watu wanaweza kujitambua kuwa wakanamungu. Ya kwanza ni ujinga. Kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi, mtu anaweza kuamua kwamba hakuna chochote kipo zaidi ya ulimwengu huu na uzoefu wa mwanadamu kwake. Kwa kuwa bado kuna mpango mkubwa hatujui, ujinga mara nyingi huvumbua mawazo kujaza mapengo. Hii mara nyingi husababisha labda dini za uongo au ukanaji Mungu. Habari hafifu kuhusu Mungu mara nyingi hutiwa doa na visasili au usihiri wa kidini kwa kiasi kwamba chochote kinaonekana si cha kawaida kama hadithi za vichimbakazi. Ilionyeshwa kwa shaghalabaghala ya madai ya kuchanganya, watu wengine huamua hakuna ukweli kwa kila kitu na kumtupa mtoto nje na maji ya kuoga.

Kuishiwa na imani ni sababu nyingine ya watu wengine kuwa wakanamungu. Kutokana na uzoefu usiofaa, kama vile sala kutojibiwa au kuona tabia ya unafiki kwa wengine, mtu anaweza kusema kwamba Mungu hayupo. Jibu hili mara nyingi linachochewa na hasira au maumivu. Watu hawa wanafikiri kwamba, kama Mungu alikuwepo, angeweza kutenda kwa njia ambazo wanaweza kuelewa au kukubaliana nazo. Kwa kuwa hakuwajibu kwa njia ambayo walitaka Yeye ajibu, wanahitimisha kwamba hapaswi kuwepo kabisa. Wanaweza kujikwaa juu ya dhana ngumu kama vile kuzimu, mauaji ya Agano la Kale, au milele, na kuhitimisha Mungu wa Biblia ni mchanganyiko sana kuwa halisi. Kuishiwa na imani huwashawishi watu kupata faraja katika kile kinachoonekana na kinachojulikana, badala ya Mungu asiyeonekana. Ili kuepuka uwezekano wa masikitiko zaidi, wanaacha jaribio lolote kwa imani na kupata kipimo cha faraja katika kuamua kwamba Mungu hayupo tu.

Wanaohusishwa kwa karibu sana na wale walioishiwa na imani ni wale wanaojiita wenyewe "wakanamungu" wakati, kwa kweli, ni wapinga Mungu. Mkanamungu ni kitambulisho ambacho baadhi hujificha nyuma ili kuficha chuki kubwa kwa Mungu. Mara nyingi kutokana na kiwewe au unyanyasaji ya utoto kwa jina la dini, watu hawa wanaharibiwa na uhasama kuelekea mambo yote ya kidini. Njia pekee ambayo wanaweza kulipiza kisasi dhidi ya Mungu wanaofikiria katili ni kumkataa Yeye kwa nguvu. Matukio ya zamani yameacha majeraha kwa kina kwamba ni rahisi kukana ukweli wa Mungu kuliko kukubali kwamba wanamchukia. Wakanamungu wa kweli hawawezi kujumuisha kundi hili kwa idadi yao, kwa vile wanatambua kwamba kuwa na hasira na Mungu ni kukubali kuwepo Kwake. Lakini watu wengi, kwa kweli, hujiita wenyewe wakanamungu wakati huo huo wakionyesha vitendo vya ujeuri kwa Mungu ambaye uwepo wake wanakataa.

Bado wengine wanakataa wazo la Mungu kwa sababu wanamtaka Yeye kuwa rahisi kupatikana. Wakati mkanamungu anayejulikana vizuri, Richard Dawkins aliulizwa, "Ungeweza kusema nini ikiwa unakabiliwa na Mungu baada ya kifo?" Akajibu, "Ningeweza kumwambia, 'Mbona ulichukua maumivu makubwa sana kujificha mwenyewe?'" Watu wengine wana chuki kwa ukweli kwamba Mungu ni Roho, asiyeonekana, na anapatikana tu kupitia imani (Waebrania 11:6; Yeremia 29:13). Wanachukua mtazamo kwamba Muumba wa ulimwengu ana deni lao la ushahidi wa kuwepo Kwake zaidi ya kile ambacho tayari ametoa kwa hiari (Zaburi 19:1, 102:25; Warumi 1:20). Yesu alikabiliana na mawazo haya wakati alipokuwa akitembea duniani. Katika Marko 8, Yesu alikuwa amewalisha watu elfu nne na mikate saba na samaki wachache, lakini wasomi wa akili walimwendea wakiomba kwamba atende ishara ya "kuthibitisha" Yeye alikuwa Masihi (mstari wa 11). Yesu alionyesha ugumu huu wa moyo katika fumbo Lake juu ya mtu tajiri katika Jahannamu ambaye alitamani kuwaonya ndugu zake juu ya kile kilichokusudiwa baada ya kifo (Luka 16:19-31). Ibrahimu akajibu kutoka mbinguni, "Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu" (Luka 16:31).

Maelezo ya uwezekano wa kuongezeka kwa ukanaji Mungu haijabadilika tangu Bustani ya Edeni (Mwanzo 3:6; Warumi 3:23). Kiini cha dhambi zote ni kujitegemea. Kwa kukataa uwepo wa Muumba, wakanamungu wanaweza kufanya chochote wanachopenda bila kujali hukumu ya baadaye au matokeo ya milele (Mathayo 12:36, Warumi 14:12, 1 Petro 4:5; Waebrania 4:13). Katika karne ya ishirini na moja, ibada ya kujitegemea imekuwa ya kukubalika kitamaduni. Ukanaji Mungu unavutia kwa kizazi kilicholelewa juu ya nadharia ya mageuzi na maadili ya Imani kwamba maarifa na maadili ni mambo ya mpito yanayotawaliwa na uwezo wa ubongo na wakati. Yohana 3:19 inasema, "… Ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu." Ikiwa wanadamu wanajiumba, kujitegemea, na ubinafsi, basi hakuna sheria ya kimaadili au mtoa sheria ambaye wanapaswa kujiwasilisha. Hakuna uhalisi na hakuna mtu ambaye hatimaye wanaajibikia. Kwa kuasili mawazo kama hayo, wakanamungu wanaweza kuzingatia kutafuta anasa katika maisha haya pekee.

Almradi wanasayansi, maprofesa, na wanafalsafa wanaeneza maoni yao ya uknaji Mungu kama ukweli na hekima, watu wataendelea kuiunua kwa sababu wazo la kujitegemea linavutia asili yetu ya uasi. Mtazamo sio kitu mpya, lakini kanuni za utamaduni zinazobadilika zimeifanya kukubalika kwa wazi zaidi. Warumi 1:18-31 inaelezea matokeo ya kukataliwa huu kwa mamlaka ya Mungu. Mstari wa 28 unasema, "Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa." Dunia yetu inaona matokeo ya uharibifu huo. Kile wakanamungu wanaita "kuelimika," Mungu huita upumbavu. Warumi 1:22 inasema, "Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika." Kwa kuwa "kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima" (Zaburi 111:10; Mithali 1:7; 9:10), basi kukataa Bwana (ukanaji Mungu) ni mwanzo wa upumbavu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini kuna wakanamungu wengi sana?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries