settings icon
share icon
Swali

Kwa kuwa wahubiri wanawake wanaweza kuwa bora sawa na wanaume, je, haimaanishi kwamba wameitwa kuhubiri?

Jibu


Kwa sabau ya zama za kale ambapo wanawake walidunishwa katika kila Nyanja, wengi hudhani kuwa vizuizi vya kibiblia juu ya majukumu ya wanawake kanisani ni sehemu ya mawazo hayo ya kijinsia. Wengine wanadai kwamba, kwa kuwa utamaduni umeondoa tofauti nyingi za kijinsia, kanisa linapaswa kufanya hivyo pia. Wengine wanasema kuwa mwanamke anaweza kuwa na kipawa kama vile mwanaume -au bora kuliko mwanaume katika kutoa hotuba hadharani na ufahamu wa Biblia, kwa hivyo mwanamke anaweza kuhubiri kama vile mwanaume anavyofanya. Ni suala linalogawanya na tunahitaji kuangalia kile Biblia inasema.

Biblia ina miongozo ya Mungu ya majukumu ya kijinsia katika dunia yake iliyo na mpangilio. Majukumu hayo ni tofauti lakini sio kubwa ama ndogo. Rangi nyekundu na kijani kibichi ni tofauti. Sio kwamba moja ni kuu kuliko nyingine lakini zinatumika kwa madhumuni tofauti. Zinakamilishana pamoja, huku zikijaza ulimwengu wetu na rangi nzuri. Ikiwa kila kitu kingekuwa chekundu au kijani kibichi, hatungethamini uzuri wa chochote. Ndivyo ilivyo katika ukamilishaji wa kijinsia. Wakati wanaume na wanawake wanapofanya kazi pamoja katika kazi zao zilizoteuliwa na Mungu, ufalme wa Mungu unastawi.

Wanawake wameitwa katika nyanja mabimbali za huduma na wanapokea karama kutoka kwa Roho Mtakatifu kama vile wanaume. Wanapaswa kutimiza wito huo na kutumia karama hizo kama vile wanaume. Wanawake walio na karama ya kufundisha wanapaswa kutumia karama hio, lakini kwa mwongozo wa Biblia. Mwongozo huo unaweza kupatikana katika 1 Timotheo 2:12. Mkazo umewekwa wazi: Mungu aliteua uongozi wa wanaume kanisani huku wanawake wakisaidia katika majukumu. Hii haimaanishi wanaume hawawezi au hawapaswi kujifunza kutoka kwa wanawake; ina maana ya kuwa wanawake hawapaswi kuwa na mamlaka ya kiroho juu ya wanaume. Nafasi ya mchungaji au mzee ni jukumu ambalo limetengwa ya wanaume-ambao pia lazima wawe na sifa fulani (ona Tito 1:5-9).

Mwanamke aliye na karama ya kufundisha au uinjilisti ana njia nyingi za kutumia karama yake kanisani, maadamu asitumie mamlaka ya kiroho ya wanaume waliyopewa na Mungu. Katika makanisa mengi yanayofundisha kwamba wanaume na wanawake wana majukumu tofauti lakini yanayokamilishana, wanawake hufundisha wanawake wengine na watoto huku madarasa ya watu wazima yanaongozwa na wanaume. Mwanamke anaweza kuwa msemaji mzuri na mhubiri shupavu lakini ustadi wake haupaswi kukanusha mfano wa Biblia. Hapaswi kuwahubiria wanaume, kana kwamba yeye ndiye kiongozi wao wa kiroho, haijalishi karama yake. Amri ya Biblia dhidi ya mwanamke kuchukua mamlaka ya kiroho kanisani inamaanisha kuwa, angalau wanawake hawapaswi kuwa wafafanuzi wa mafundisho kanisani. Watafsiri wenye mamlaka wa maandiko- wanaoongoza kiroho-wanapaswa kuwa wanawake.

Matendo ya Mitume 18:24–26 inaelezea hadithi ya Apolo aliyekuwa akifundishwa na timu ya mume na mke walioitwa Prisila na Akila. Apolo alipokea mafundisho hayo, akajifunza utimilifu wa ujumbe wa injili na akawa mwinjikisti shupavu. Je, Prisila alikuwa mfano wa "wanawake wahubiri wa kisasa"? Hapana, kifungu hiki ni wazi kwamba maagizo aliyopata Apolo hayakuwa ya kirasmi, yalikuwa ya faragha na yalifanywa na Prilisa na mumewe: "wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi" (mstari wa 26). Prisila kushiriki injili na Apolo; hakuwahi kuonekana kama mamlaka ya kiroho kanisani. Paulo baadaye anawaita Prisila na mumewe "wafanyikazi wenzake" (Warumi 16:3).

Wanawake wengine ambao wana karama ya mawasiliano wanajihisi kwamba wameitwa kuhubiri, na mara nyingi wanaweza kufanya kazi bora kuliko wanaume kwenye mimbara. Lakini ni muhimu watazame suala hilo kulingana na Biblia na wajitolee kufanya majukumu ambayo Mungu ameteua. Kuchukua jukumu la uchungaji, kuamua mwelekeo wa kanisa wa kiroho na njia zingine za kuwa na mamlaka juu ya wanaume kanisani inapita mpango wa Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa kuwa wahubiri wanawake wanaweza kuwa bora sawa na wanaume, je, haimaanishi kwamba wameitwa kuhubiri?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries