settings icon
share icon
Swali

Je! Wachungaji wanapaswa kulipwa mshahara?

Jibu


Hakika kanisa linapaswa kukidhi mahitaji ya kifedha ya wachungaji wake na wahudumu wengine wa wakati wote. Wakorintho wa Kwanza 9:14 inalipa kanisa maagizo wazi: "Vivyo hivyo, Bwana ameamuru kwamba wale wanaohubiri Injili wapate riziki yao kutokana na Injili." Tunawalipa watu ili waandae na kutubakulia chakula chetu cha mwili; hatupaswi pia kuwa tayari kuwalipa wale wanaotulisha chakula chetu cha kiroho (Mathayo 4: 4)?

Timotheo wa Kwanza 5: 17-18 inasema, "Wazee wa kanisa wanaoongoza shughuli za kanisa vizuri wanastahili heshima mara mbili, hasa wale ambao kazi yao ni kuhubiri na kufundisha. 18Kwa maana Maandiko husema, "Usimfunge maksai kinywa apurapo nafaka," tena, "Mfanyakazi anastahili mshahara wake.'" Kunazo hoja kadhaa zilizotolewa katika kifungu hiki. Wazee wa kanisa wanapaswa kuheshimiwa, na heshima hii inajumuisha mshahara. Wale wazee wanaotumikia kanisa vizuri — haswa waalimu na wahubiri — wanapaswa kupokea heshima maradufu. Wahitimu kwa kazi hiyo. Itakuwa ukatili kufanyisha ndume kazi huku ukimnyima nafaka, na tunapaswa kuwa waangalifu tusiwatendee wachungaji wetu ukatili. Wacha washiriki katika baraka za kimwili za kanisa wanalolitumikia. Wachungaji wetu ni wa thamana kuu kuliko ndume.

Hakuna funzo lolote laa kiroho katika kumfanya mchungaji "kuteseka kwa ajili ya kumtumikia Bwana." Naam, mchungaji ameitwa na Mungu kwa huduma yake, lakini haimanishi kwamba kanisa linapaswa kusema, "Wacha Mungu amshugulikie." Mungu anasema kuwa kanisa lenyewe linawajibika katika kumtunza yeye na familia yake. Kutunza mahitaji ya kiroho ya kanisa ni kazi muhimu — labda muhimu zaidi kuliko vitu vingine vya kawaida ambavyo tunatumia pesa kuvinunua, kama vile kukidhi mahitaji yetu ya kimwili, kutunza magari yetu, na kujiburudisha. Angalia 1 Wakorintho 9: 7.

Ni kweli kwamba mtume Paulo alijisaidia mwenyewe wakati alihudumu huko Korintho (1 Wakorintho 9:12). Hakupata mshahara wowote kutoka kwa Wakorintho. Lakini aliweka wazi kuwa alifanya hivi kwa kujitolea kwa hiari kwa niaba yao, "Ya kwamba katika kuhubiri Injili niitoe bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili" (aya ya 18). Paulo alipokea mshahara kutoka kwa makanisa mengine (2 Wakorintho 11: 8). Mpangilio wake huko Korintho ulikuwa maalum, sio sheria.

Wakati mwingine kanisa haliwezi kutoa pesa za kutosha kumlipa mchungaji. Mchungaji katika hali kama hiyo analazimika kuwa mbunifu, bila kuwa na chaguo bali kufanya kazi nje ya kanisa ili kusaidia familia yake. Hii inasikitisha lakini wakati mwingine ni lazima. Kwa kawaida huwa bora mchungaji akilipwa ili ajitolee muda wake wote kikamilifu kwa kazi ya Bwana ya kuhudumia na kulichunga kanisa ambalo Mungu amemkabidhi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Wachungaji wanapaswa kulipwa mshahara?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries