settings icon
share icon
Swali

Je, wanawake wahudumu kama wachungaji/wahubiri? Je, Biblia inasemaje juu ya wanawake katika huduma?

Jibu


Yaonekana hakuna jambo lengine lenye kujadiliwa sana juu ya kanisa leo kama swala la wanawake wanao hudumu katika nyadhifa za uchungaji na uhubiri. Kwa hivyo si vyema kulitazama jambo hili kwa msingi wa waume kupinga wanawake. Kuna wanawake wanaoamini kuwa si vyema wanawake wawe wachungaji na Biblia inatoa vikwazo juu ya huduma ya wanawake – na kuna wanaume wanaoamini kuwa wanawake wanafaa kuhudumu kama wahubiri na hakuna vizuizi vyovyote juu ya huduma ya wanawake. Hili si swala la ubaguzi wa kijinsia ila la ufafanuzi wa maandiko ya Biblia.

Timotheo wa kwanza 2:11-12 inasema, “mwanamke na ajifunze katika utulivu akitii kwa kila namna. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha wala kumtawala mwanamume bali awe katika utulivu.” Katika kanisa Mungu hugawanya wajibu kwa wanaume na wanawake. Hii ni kwa sababu ya vile wanadamu walivyoumbwa (Timotheo wa kwanza 2:13) na pia kwa jinsi ile dhambi ilivyoingia duniani (Timotho wa pili 2:14). Mungu, kupitia nyaraka za Mtume Paulo akataza wanawake kuhudumu katika nyadhifa zenye kuwapa mamlaka ya kiroho juu ya wanaume. Hii inajumuisha huduma ya uchungaji, uhubiri, walimu na mamlaka ya kiroho juu ya wanaume.

Kuna upinzani mwingi juu ya wanawake kuhudumu katika uchungaji. La kwanza, Paulo awazuia wanawake wasifundishe kwa kuwa katika karne ya kwanza wanawake hawakusoma. Ijapokuwa katika Timotheo wa kwanza 2:11-14 hawakutaja swala la elimu. Kama kusoma kungekuwa kigezo cha mtu kuhudumu basi wanafunzi wengi wa Yesu hawangehudumu. La pili ni kwamba Paulo aliwakataza wanawake wa kiefeso wasifundishe (Timotheo wa kwanza ni waraka kwa ajili ya Timotheo aliyekuwa mchungaji wa kanisa la efeso). Mji wa efeso ulijulikana sana kwa hekalu lake la Artemi, Mungu bandia wa kiyunani na kirumi. Wanawake walikuwa ndio wenye mamlaka katika ibaada ya Artemi, ambayo ndiyo sababu ya kukatazwa huku katika Timotheo wa kwanza 2:11-12.

La tatu ni kuwa Paulo azungumzia juu ya wake na waume zao wala si wanawake kwa wanaume kwa jumla. Neno la kiyunani katika Timotheo wa kwanza 2:11-14 yaweza kumaanisha waume kwa wake zao. Katika aya za 8-10 pia neno hilo limetumika tena. Je, ni Wanaume pekee ambao niwainue mikono yao mitakatifu katika sala bila hasira wala kulazimishwa (aya 8)? Je, ni wanawake tu ndio ni wavae mavazi ya kujisitiri, wawe na matendo mema na wamwabudu Mungu (aya 9 - 10)? La hasha. Aya za 8 – 10 zazungumzia juu ya wanaume na wanawake kwa jumla swala sio waume kwa wake zao. Hakuna chochote ambacho kingethibitisha kusimama mahali pa waume na wake katika aya 11-14.

Pingamizi kwa tafsiri hii ya wanawake wachungaji/wahubiri ni kwa kuwatazama Miriam, Deborah, Huldah, Prisilla,Fibi na kadhalika, waliokuwa na nyadhifa za uongozi katika Biblia. Deborah alikuwa mwanamke peke yake aliyekuwa mwamuzi katika waamuzi 13. Huldah alikuwa peke yake nabii wa kike kati ya manabii wote waliotajwa katika Biblia. Miriam aliunganihwa na huduma ya ndugu zake wakina Musa na Haruni. Wanawake maarufu katika nyakati za wafalme ni Athaliah na Yezebeli – ambao hawawezi kufaa kama mifano ya wanawake waliokuwa na uongozi wa kimungu.

Katika kitabu cha Matendo ya mitume 18, Prisila na Akwila wanatambulishwa kama watumishi wa kristo waaminifu. Jina la prisila linatajwa kwanza,kuashiria alikuwa maarufu zaidi katika huduma kuliko mumewe.hakuna mahali alipoelezwa kufanya huduma yoyote ambayo ni kinyume na Timotheo wa kwanza 2: 11-14. walimleta kwa pamoja Apolo nyumbani mwao na kumfanya mwanafunzi kwa kumfundisha neno la Mungu kwa uhakika (matendo 18:26).

ika Warumi 16:1 hata Fibi pia atambuliwa kama shemasi wala si mtumishi kama vile mwalimu katika kanisa ajulikanavyo. “mwenye uwezo wa kufundisha “ ni kigezo cha wazee lakini kwa shemasi hakitumiki. Timotheo wa kwanza 3:1-13; Tito 1:6-9). Wazee/ makasisi/ mashemasi wanatajwa kama “waume wa mke mmoja” “mume ambayo watoto wake wanaamini,” na “ waume wanostahili heshima.”

Mpangilio wa maandiko katika Timotheo wa kwanza 2:11-14 inafafanua vizuri. Aya 13 inaeleza kwa nini Paulo alisema yale ayliymo katika aya za 11-12. kwa nini wanawake wasifundishe na wasiwe na mamlaka juu ya waume? Kwa sababu,- “kwa kuwa Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.” Hii ndiyo sababu. Mungu alimuumba Adamu kwanza na Hawa baadaye ili awe msaidizi wa Adamu. Hivyo ndivyo ilivyo katika jamii zetu nyumbani (waefeso 5:22-33) na kanisani. Wengi huamini kuwa wanawake ni rahisi kudanganywa.hivyo ni sawa na kusema wanawake wasiwe walimu. Mbona basi huachiwa watoto wawafunze? Ujumbe huo haukulenga tafsiri hiyo. Kwa sababu hiyo basi, Mungu amewapa wanaume jukumu na mamlaka ya kufundisha katika kanisa.

Wanawake ni bora katika vipawa vya ukarimu,huruma walimu na misaada. Huduma nyingi za kanisa hutegemea wanawake wanawake kanisani hawakatazwi kuomba kwa sauti au kutoa unabii (wakorintho wa kwanza 11:5), lakini wamekatazwa kuwa na mamlaka ya kiroho juu ya wanaume. Biblia haikatazi wanawake wasitumie vipawa vya Roho Mtakatifu (wakorintho wa kwanza 12). Wanawake, kama vile wanaume, huitwa kuhudumiana ili wadhihirisha matunda ya Roho Mtakatifu (wagalatia 5:22-23), na klitangaza injili kwa waliopotea (Mathayo 28:18-20; matendo 1:8; petro wa kwanza 3:15).

Mungu ameidhinisha waume wahudumu katika nyadhifa za mafundisho yenye mamlaka ya kiroho katika kanisa.hii si kwa sababu wanaume ni walimu bora au kuwa wanawake ni watu duni. Ni kwa sababu Mungu mwenyewe alitaka kanisa liwe hivyo. Wanaume ni wawe mifano katika uongozi wa kiroho- katika maisha yao na pia katika matamshi yao. Wanawake wanasisitizwa kufundisha wanawake wengine (Tito 2:3-5). Biblia pia haiwazuii wanawake kuwafundisha watoto. Kila wanachozuia kufanya ni kufundisha au kuwa na mamlaka ya kiroho juu ya wanaume. Hili linawajumuisha wanawake katika huduma ya uchungaji/uhubiri. Hili haliwafanyi wanawake kuwa si wa muhimu sana ila kuwapa mtazamo katika huduma ambao una kubalika mbele za Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, wanawake wahudumu kama wachungaji/wahubiri? Je, Biblia inasemaje juu ya wanawake katika huduma?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries