settings icon
share icon
Swali

Ni akina nani walikuwa waandishi wa vitabu vya Biblia?

Jibu


Hatimaye, zaidi ya waandishi wa binadamu, Biblia iliandikwa na Mungu. Timotheo wa pili 3:16 inatuambia kwamba Biblia ni "pumzi" ya Mungu. Mungu aliwaongoza waandishi wa binadamu wa Biblia ili, huku wakitumia mitindo wa uandishi na wenyewe wa haiba, wao bado walinakili kile hasa ni lengo la Mungu. Biblia haikuimliwa na Mungu, lakini iliongozwa kikamilifu na Mungu.

Kwa kusungumza kiubinadamu, Biblia iliandikwa na takriban watu 40 wa kada mbalimbali katika kipindi cha miaka 1500. Isaya alikuwa nabii, Ezra alikuwa kuhani, Mathayo alikuwa mtoza ushuru, Hoyana alikuwa mvuvi, Paulo alikuwa mtengeza ema, Musa alikuwa mchungaji, Luka alikuwa daktari. Licha ya kuandikwa na waandishi mbalimbali juu ya karne 15, Biblia haijichanganyi yenyewe na haina makosa yoyote. Waandishi wote waonyesha mitazamo yao mbalimbali, lakini wao wote wanamtangaza yule Mungu mmoja wa kweli, na hiyo njia moja ya wokovu ya Yesu (Yohana 14:6, Matendo 4:12). Chache ya vitabu vya Biblia hasa hutaja majina ya waandishi. Hapa kuna vitabu vya Biblia pamoja na majina ya wale ambao wemedhaniwa na wasomi wa Biblia kuwa waandishi, pamoja na tarehe ya uandishi :

Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu, Kumbukumbu = Musa - 1400 BC (Kabla Yesu azaliwe)
Joshua = Joshua - 1350 BC
Waamuzi, Ruthu, 1 Samweli, 2 Samweli = Samuel / Nathan / Gadi - 1000-900 BC
1 Wafalme, 2 Wafalme = Jeremiah - 600 B.C.
1 Mambo ya Nyakati, 2 Mambo ya Nyakati, Ezra, Nehemia = Ezra - 450 BC
Esther = Mordekai - 400 BC
Kazi = Musa - 1400 BC
Zaburi = baadhi ya waandishi mbalimbali, wengi wao wakiwa David - 1000 - 400 BC
Mithali, Mhubiri, Wimbo wa Sulemani = Solomon - 900 BC
Isaya = Isaya - 700 BC
Yeremia, Maombolezo = Jeremiah - 600 BC
Ezekieli = Ezekieli - 550 BC
Danieli = Danieli - 550 BC
Hosea = Hosea - 750 BC
Yoeli = Yoeli - 850 BC
Amosi = Amosi - 750 BC
Obadia = Obadia - 600 BC
Yona = Yona - 700 BC
Mika = Mika - 700 BC
Nahumu = Nahumu - 650 BC
Habakuki = Habakuki - 600 BC
Sefania = Sefania - 650 BC
Hagai = Hagai - 520 BC
Zakaria = Zakaria - 500 BC
Malaki = Malaki - 430 BC
Mathayo = Mathayo - A.D. 55
Marko=Yohona Marko A.D 50
Luka = Luka - A.D. 60
Yohana= Yohana - A.D. 90
Matendo = Luke - A.D. 65
Warumi, 1 Wakorintho, 2 Wakorintho, Wagalatia, Waefeso, Wafilipi, Wakolosai, 1 Wathesalonike, 2 Wathesalonike, 1 Timotheo, 2 Timotheo, Tito, Philemon = Paul - AD 50-70
Waebrania = haijulikani, kuna uwezekano kzaidi kuwa ni Paulo, Luka , Barnabas , au Apolo - AD 65
Yakobo = Yakobo- A.D. 45
1 Petro, 2 Petro = Petro - A.D. 60
1 Yohana, 2 Yohana, 3 Yohana = Yohana - A.D. 90
Yuda= Yuda - A.D. 60
Ufunuo = Yohana- A.D. 90

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni akina nani walikuwa waandishi wa vitabu vya Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries