settings icon
share icon
Swali

Je! Waandishi wa Agano Jipya walichukulia uandishiw wao kuwa Maandiko?

Jibu


Timotheo wa Pili 3:16-17 yatangaza kwamba "Kila Andiko limevuviwa na Mungu na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe amekamilishwa, apate kutenda kila kazi njema." Ni wazi kwamba kanisa la kwanza lilichukulia Agano la Kale kuwa Maandiko yaliyovuviwa. Vile 2 Petro 1:20-21 inaeleza, "Kama wameukimbia upotovu wa dunia kwa kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo, kisha wakanaswa tena humo na kushindwa, hali yao ya mwisho ni mbaya zaidi kuliko ile ya kwanza. Ingelikuwa afadhali kwao kama wasingeliijua kamwe njia ya haki, kuliko kuijua kisha wakaiacha ile amri takatifu waliyokabidhiwa."

Je! Lakini hili linaweza kutumika sawia kwa uandisho ulioko katika Agano Jipya? Je! Waandishi wa Agano la Kale walijua hali ya maandiko ya nyaraka zao? Ijapokuwa hili haliwezi kuthibitishwa kwa hakika, kunayo kauli ngumu ya kufanya kuwa walikuwa wanajua. Katika 2 Petro 3:15-16, Petro anaandika, "Hesabuni uvumilivu wa Bwana kuwa ni wokovu, kama vile ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima ile aliyopewa na Mungu. Huandika vivyo hivyo katika nyaraka zake zote, akizungumzia ndani yake mambo haya. Katika nyaraka zake kuna mambo mengine ambayo ni vigumu kuyaelewa, ambayo watu wajinga na wasio thabiti huyapotosha kwa maangamizi yao wenyewe, kama wapotoshavyo pia Maandiko mengine." kwa wazi Petro alihesabu uandishi wa Paulo kuwa Maandiko yalivuviwa.

Ishara nyingine zaidi ya kuwa waandishi wa Agano Jipya walielewa uandishi wao kuwa Maandiko ni 1 Timotheo 5:18, wakati inatangazwa, "Kwa maana Maandiko husema, "Usimfunge maksai kinywa apurapo nafaka," tena, "Mfanyakazi anastahili mshahara wake." Huku rejeleo la kwanzwa limenukuliwa kutoka Kumbukumbu (25:4), la pili limetolewa katika Injili ya Luka (10:7). Kwa wazi, uandishi wa Luka unatazamiwa kuwa sawia kimamlaka na dhamani kama ule wa Torati. Uandishi wa Luka vile vile hapa unarejelewa kama "Maandiko."

Kwa kumalizia, kuna sababu nzuri za kuamini kwamba waandishi wa Agano Jipya waliona maandishi ya kila mmoja kama Maandiko matakatifu, yaliyovuviwa na Mungu – "na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe amekamilishwa, apate kutenda kila kazi njema" (2 Timotheo 3: 16-17).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Waandishi wa Agano Jipya walichukulia uandishiw wao kuwa Maandiko?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries