settings icon
share icon
Swali

Je, waandishi waliobishana na Yesu walikuwa kina nani?

Jibu


Waandishi katika Israeli ya kale walikuwa watu ambao kazi yao ilikuwa kujifunza Sheria, kuitafsiri, na kuandika maoni kuhusu sheria. Walipata kuajiriwa pia wakati ambapo kulikuwa na haja ya kuandika hati au wakati tafsiri ya jambo la kisheria ilihitajika. Ezra ambaye alikuwa "mwalimu aliyefahamu sana Sheria ya Musa," alikuwa mwandishi (Ezra 7: 6).

Waandishi walichukulia kazi yao ya kuhifadhi Maandiko kwa uzito sana; wangepiga nakala ya Biblia na kuipitia kwa uangalifu, hata kuhesabu barua na nafasi katika nakala hizo ili kuhakikisha kila nakala ilikuwa sahihi. Tunaweza kuwashukuru waandishi wa Kiyahudi kwa kuhifadhi sehemu ya Agano la Kale ya Biblia zetu.

Wayahudi walizidi kujulikana kama "watu wa Kitabu" kwa sababu ya kujifunza kwao kwa Maandiko, hasa Sheria na jinsi ilifaa kufuatwa. Katika zama za Agano Jipya, mara nyingi waandishi walihusishwa na dhehebu la Mafarisayo, ingawa sio Mafarisayo wote walikuwa waandishi (tazama Mathayo 5:20, 12:38). Waandishi walikuwa walimu wa watu (Marko 1:22) na wakalimani wa Sheria. Waliheshimiwa sana na jamii kwa sababu ya ujuzi wao, kujitolea, na jinsi walivyoweka sheria.

Waandishi walifanya zaidi ya kutafsiri Maandiko, hata hivyo waliongezea mila nyingi zilizofanywa na wanadamu kwa kile Mungu alichosema. Wao wakawa wataalamu wa kusoma barua ya Sheria huku wakipuuza roho iliyoishawishi. Mambo yakawa mabaya sana kwamba kanuni na mila ambayo waandishi waliongeza kwa Sheria zilizingatiwa kuwa muhimu zaidi kuliko Sheria yenyewe. Jambo hili likasababisha mapambano mengi kati ya Yesu na Mafarisayo na waandishi. Mwanzoni mwa Mahubiri ya Mlimani, Yesu aliwashangaza wasikilizaji wake kwa kutangaza kuwa haki ya waandishi haingeweza kuwafanya waingie katika ufalme wa mbinguni (Mathayo 5:20). Sehemu kubwa ya mahubiri ya Yesu yalizungumzia yale watu waliyokuwa wamefundishwa (na waandishi) na kile ambacho Mungu alitaka (Mathayo 5: 21-48). Kuelekea mwisho wa huduma ya Yesu, aliwahukumu kabisa waandishi kwa unafiki wao (Mathayo 23). Walifahamu Sheria, na waliifundisha wengine, lakini hawakuitii.

Lengo la awali la waandishi lilikuwa kujua na kuhifadhi Sheria na kuhimiza wengine kuifuata. Lakini mambo yalienda mrama wakati mila iliyofanywa na wanadamu ilichukua nafasi ya Neno la Mungu na pia kujifanya kuwa watakatifu kulibadilisha maisha ya uungu wa kweli. Waandishi ambao walisema lengo lao ni kulinda Neno, kwa kweli waliibatilisha na mila waliyofundisha(Marko 7:13).

Je, Mambo yalipataje kuchukua mkondo tofauti? Pengine kwa sababu baada ya kuishi miaka mingi ya mateso na utumwa Wayahudi walikuwa na kiburi kwa kutunza ile Sheria na jinsi ilivyowafanya kuonekana kama watu waliochaguliwa na Mungu. Viongozi wa kidini katika siku za Yesu bila shaka walijiskia bora (Yohana 7:49), jambo ambalo Yesu alipinga (Mathayo 9:12). Tatizo kubwa ni kwamba waandishi walikuwa wanafiki mioyoni mwao. Walikuwa na nia ya kuonekana wazuri mbele ya watu kuliko walivyozingatia kumpendeza Mungu. Hatimaye, waandishi hao ndio walioshiriki katika kumfunga Yesu na kusulubiwa (Mathayo 26:57, Marko 15: 1; Luka 22: 1-2). Somo ambayo kila Mkristo anaweza kujifunza kutokana na unafiki wa waandishi ni kwamba Mungu anataka zaidi ya vitendo vya nje vya haki. Mungu anapendezwa na mabadiliko ya ndani ambayo huendelea kushawishiwa katika upendo na utii kwa Kristo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, waandishi waliobishana na Yesu walikuwa kina nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries