settings icon
share icon
Swali

Waamoni walikuwa kina nani?

Jibu


Katika historia ya awali ya Israeli, tunaona kumbukumbu ya watu wa Amoni. Walikuwa kina nani, walitoka wapi, na ni nini kilichowafanyikia? Waamoni walikuwa watu wa Kisemiti, wanaohusiana sana na Waisraeli. Licha ya uhusiano huo, mara nyingi walihesabiwa kuwa adui kuliko marafiki.

Loti, mpwa wa Ibrahimu, alikuwa kutoka uzao wa Waamoni. Baada ya Ibrahimu na Loti kutenganishwa (Mwanzo 13), Loti aliishi katika jiji la Sodoma. Wakati Mungu aliharibu Sodoma na Gomora kwa sababu ya uovu wao, Loti na binti zake walikimbilia nchi ya kilima kwenye mwisho wa kusini wa Bahari ya Ufu. Labda walifikiri walikuwa watu pekee walioachwa duniani, binti za Loti walimnywesha mvinyo na wakawa na uhusiano wa ngono na yeye ili kuzalisha watoto (Mwanzo 19: 30-38).Binti wa kwanza akawa na mwana mmoja aitwaye Moabu ("kutoka kwa baba yangu"), na binti mdogo alimzaa Ben-Ammi ("mwana wa watu wangu"). Waamoni, wana wa Ben-Ammi, walikuwa watu wahamaji ambao waliishi katika eneo la Yordani ya leo, na jina la mji mkuu, Amman, linaonyesha jina la wenyeji wa kale.

Wakati wa Musa, ardhi tambarare za rutuba za mto wa Yordani zilikuwa zimechukuliwa na Waamori, Waamoni na Wamoabu. Waisraeli walipotoka Misri, Waamoni walikataa kuwasaidia kwa namna yoyote, na Mungu akawaadhibu kwa kukosa kuwasaidia (Kumbukumbu la Torati 23: 3-4). Baadaye, hata hivyo, Waisraeli walipoingia katika Nchi ya Ahadi, Mungu aliwaagiza, "Utakaposongea kuwaelekea wana wa Amoni, usiwasumbue wana wa Amoni, wala usishindane nao; kwa kuwa sitakupa katika nchi ya hao wana wa Amoni kuwa milki yako; kwa sababu nimewapa wana wa Lutu iwe milki yao."(Kumbukumbu la Torati 2:19). Makabila ya Waisraeli ya Gadi, Reubeni, na nusu ya kabila ya Manase walichukua eneo la Waamori lililopakana na Waamoni.

Waamoni walikuwa watu wa kipagani ambao waliabudu miungu ya Milcom na Moleki. Mungu aliwaagiza Waisraeli wasiolewe na wapagani hawa, kwa sababu ingefanya Waisraeli kuabudu miungu ya uwongo. Sulemani hakutii, alimwoa Naama Mwamoni (1 Wafalme 14:21), pamoja na wanawake wengi wa kipagani, na, kama Mungu alivyoonya, alivutiwa na ibada ya sanamu (1 Wafalme 11: 1-8). Moleki alikuwa mungu wa moto na alikuwa na uso wa ndama; picha zake zilikuwa na mikono iliyonyooshwa ili kupokea watoto ambao walikuwa wametolewa dhabihu kwake. Kama vili mungu wao, Waamoni walikuwa wakaidi. Wakati Nahashi, Mwamoni alipoulizwa kuhusu makubaliano ya mkataba (1 Samweli 11: 2), alipendekeza kutolewa kwa jicho la kulia la kila mtu wa Kiisraeli. Amosi 1:13 inasema kwamba Waamoni waliwapasua wanawake wajawazito katika wilaya walizochukua.

Chini ya uongozi wa Mfalme Sauli, Israeli waliwashinda Waamoni na wakawafanya watumwa. Daudi aliendelea kutawala Amoni na baadaye akazingira mji mkuu ili kuimarisha udhibiti wake. Baada ya kugawanyika kwa Israeli na Yuda, Waamoni walianza kujiunga na maadui wa Israeli. Amoni alipata utawala kiasi tena katika karne ya saba kabla ya Yesu kuzaliwa, mpaka Nebukadineza akawashinda miaka mia moja baadaye. Tobia ambaye ni Mwamoni (Nehemiya 2:19) inaonekana alikuwa gavana wa eneo chini ya utawala wa Kiajemi, lakini wenyeji walikuwa mchanganyiko wa Waamoni, Waarabu, na wengine. Katika nyakati za Agano Jipya, Wayahudi walikuwa wameishi eneo hilo, na ilikuwa inajulikana kama Perea. Waamoni wametajwa mara ya mwisho kama watu tofauti katika karne ya pili na Justin Martyr, ambaye alisema walikuwa wengi sana. Wakati mwingine wakati wa Kirumi, Waamoni wanaonekana kuwa wamejumuika katika jamii ya Kiarabu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Waamoni walikuwa kina nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries