settings icon
share icon
Swali

Kwanini kuna vurumai nyingi katika Agano la Kale?

Jibu


Ukweli kwamba Mungu aliamuru kuuawa kwa mataifa katika Agano la Kale imekuwa mada ya kukosoa kwa ukali kutoka kwa wapinzani wa Ukristo kwa muda mrefu. Hatuwezi kukana vita katika Agano la kale. Swali ibuka ni ikiwa vurumai katika Agano ya Kale ilikuwa halali na ikiwa iliruhusiwa na Mungu. Richard Dawkings asiyemwamini Mungu, katika kitabu chake The God Delusion, anarejelea Mungu kama mwenye kulipiza kisasi, mwenye kiu ya mauaji ya kikabila. Mwana habari Christopher Hitchens analalamika kwamba Agano la Kale lina kibali cha mauaji "yasiyokuwa ya ubaguzi." Wakosoaji wengine wa Ukristo wana mashtaka kama hayo, wakimshtaki Yahweh kwa "uhalifu dhidi ya binadamu."

Je, Ukosoaji huu ni halali? Mungu wa Agano la Kale ni "mkatili" ambaye anaamuru mauaji ya jinai dhidi ya wanaume, wanawake, na watoto wasio na hatia? Je, majibu yake kwa dhambi za Wakanaani na Wamaleki yalikuwa ya "kuangamiza makabila"? Au inawezekana kuwa Mungu alikuwa na sababu nzuri za kutosha za kuamuru kuangamizwa kwa mataifa haya?

Ujuzi wa kimsingi wa tamaduni ya Wakanaani hufunua uovu wa maadili yake. Wakanaani walikuwa wakatili, wenye ujeuri ambao walijishughulisha na matendo ya kinyama, zinaa ya maharimu na kutoa dhabihu ya watoto. Vitendo vya ngono haramu vilikuwa kama kawaida. Dhambi ya Wakanaani ilikua mbaya hata Mungu akasema, "Hiyo nchi yatapika wenyeji wake kuwatoa" (Mambo ya Walawi 18:25). Hata hivyo, uharibifu huo ulielekezwa zaidi kwa dini ya Kanaani ( Kumbukumbu la Torati 7:3-5, 12:2-3) kuliko kwa Wakanaani wenyewe. Hukumu hio haukuchochewa na ukabila. Wakanaani binafsi kama vile Rahabu huko Yeriko walipata rehema baada ya toba (Yoshua 2). Mungu anatamani kwamba waovu wageuke kutoka kwa dhambi badala ya kufa (Ezekieli 18:31-32, 33:11).

Mbali na kushughulikia dhambi za kitaifa, Mungu alitumia ushinde wa Kanaani kuunda mukhtadha wa kidini/Kihistoria ambayo mwishowe angemtambulisha Masihi ulimwenguni. Masihi huyu angeleta wokovu sio tu kwa Israeli bali pia kwa maadui wa Israeli, ikiwepo Kanaani (Zaburi 87:4-6; Marko 7:25-30).

Itakumbukwa kwamba Mungu aliwapa watu wa Kanaani muda zaidi wa kutosha kutubu dhambi zao -zaidi ya miaka 400! Kitabu cha Waebrania kinatuambia kwamba Wakanaani walikuwa "wasiotii," kumaanisha walikosa maadili (Waebrania 11:31). Wakanaani walikua wanajua nguvu za Mungu (Yoshua 2:10-11; 9:9) na wangetafuta toba. Isipokuwa tu katika hali adimu, wao waliendelea na uasi wao dhidi ya Mungu hadi mwisho wenye majonzi.

Lakini je, Mungu pia aliamuru Waisraeli kuuwa wasio washambulizi? Rekodi katika Biblia ni wazi kwamba alifanya hivyo. Itakumbukwa kwamba ingawa wanawake Wakanaani hawakupigana vita, hii haimaanishi kuwa hawakuwa na hatia, kama vile tabia yao ya utongozi inavyoonekana katika (Hesabu 25:1-3).Hata hivyo, swali ibuka ni, je, na watoto pia? Hili sio swali rahisi lakini tunapaswa kujua kwamba, hakuna mtu ambaye hana hatia (wakiwepo watoto wachanga). Maandiko yanatufundisha kuwa sisi sote tumezaliwa katika dhambi (Zaburi 51:5; 58:3). Hii inamaanisha kwamba watu wote wana hatia ya Adamu kwa njia fulani. Watoto pia wamehukumiwa kutoka kwa dhambi kama vile watu wazima.

Pili, Mungu ni mwenye enzi juu ya maisha yote na anaweza kuyachukua wakati wowote. Ni Mungu pekee anayepatiana uhai, na ni yeye pekee ambaye ana haki ya kuuchukua wakati wowote atakapochagua. Kwa kweli, Yeye hatimaye huchukua maisha ya kila mtu wakati wa kifo. Maisha sio yetu lakini ni ya Mungu. Ni hatia kwa mwanadamu kuchukua uhai, isipokuwa katika visa vya adhabu, vita, na hali ya kujitetea lakini hii haimaanishi kwamba Mungu huwa na hatia anapofanya hivyo. Kihisia asili tunatambu hili wakati tunatuhumia watu wengine au mamlaka ambayo yanachukua maisha ya mtu kuwa "kumchezea Mungu." Mungu hayuko chini lazimisho lolote kurefusha maisha ya kila mmoja hata kwa siku moja. Jinsi na wakati tutakufa yote ni juu yake.

Tatu, bishano linaeza fanywa kuwa ingekuwa ukatili kwa Mungu kuyachukua maisha ya Wakanaani wote na kuacha Watoto. Bila ulinzi wa wazazi wao na utunzaji, watoto wachanga na watoto wa makamu wangekumbana n amauti kwa sababu ya njaa. Fursa ya kuwa hai kwa yatima katika karne ya kale haikuwa nzuri.

Mwisho, Watoto wa Kanaani wangekuwa watu wazima wakiwa na huruma kwa dini mbaya za wazazi wao. Ilifika wakati utamaduni wa kuabudu sanamu na upotovu kuisha Kanaani, na Mungu alitaka kuwatumia Waisraeli kuumaliza. Pia, watoto waliobaki yatima wa Kanaani kiasili wangekuwa watu wazima wakiwa na chuki na Waisraeli. Pengine, wengine wangetafuta baadaye kulipisa "mabaya" wazazi wao walitendewa na kuirudisha Kanaani na kuwa nchi isiyo amini Mungu.

Pia ni jambo la muhimu kusingatia hali ya milele ya wale watoto wachanga waliouawa Kanaani. Ikiwa Mungu aliwachukua kablia wafikie umri wa uwajibikaji, basi moja kwa moja walienda mbinguni (vile tunavyo amini). Hao Watoto wako mahali pazuri kuliko ikiwa wangeishi na kuwa watu wazima kama Wakanaani.

Hakika, suala la Mungu kuamrisha vurumai katika Agano la Kale ni ngumu sana. Walakini, tunafaa kukumbuka kwamba Mungu anaona mambo kutoka kwa mtazamo wa milele, na njia zake sio kama njia zetu (Isaya 55:8-9). Mtume Paulo anatuambia kwamba Mungu ni mpole na pia mkali (Warumi 11:22). Huku ikiwa kweli kuwa siha takatifu ya Mungu hudai kuwa dhambi iadhibiwe, lakini neema yake na huruma huendele kuwepo kwa wale wako tayari kutubu na kuokolewa. Kuangamizwa kwa Wakanaani hutupa ukumbusho tulivu kwamba, huku ikiwa Mungu wetu ni wa neema na mkarimu, pia ni Mungu wa utakatifu na ghadhabu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwanini kuna vurumai nyingi katika Agano la Kale?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries