settings icon
share icon
Swali

Je, viumbe wenye uhai katika Ufunuo ni kina nani?

Jibu


Viumbe wanne wenye uhai wanapatikana katika Ufunuo 4:6–9; 5:6–14; 6:1–8; 14:3; 15:7; na 19:4. Maandiko ambayo yanaelezea viumbe hawa hayaonyeshi kuwa ni viumbe hao niwa kitamathali -wao ni halisi. Viumbe wannne wenye uhai (“viumbe”kihalisi) ni maalum na wameinuliwa kwa kiwango cha kiumbe malaika au makerubi. Hii ni wazi kwa ukaribu wao na kiti cha enzi cha Mungu. Ezekieli 1:12–20 inadokeza kwamba wako daima katika mwendo wakizunguka kiti cha enzi.

Ufunuo 5:6-14 inaeleza majukumu na makusudi ya viumbe wanne wenye uhai. Wanaanguka chini na kumwabudu Mwana Kondoo, Yesu Kristo, wakimpa heshima ileile ambayo walimpa Bwana (Ufunuo 4:8), wakidhibitisha uungu wa Yesu Kristo. Wao pamoja na wazee ishirini na wanne wana “vinubi na mabakuli ya dhahabu, ambayo ni maombi ya watakatifu” (Ufunuo 5:8). Mara nyingi vinubi vinahusishwa na ibada katika Agano la Kale, pamoja na unabii (2 Wafalme 3:15; 1 Nyakati 25:1). Uvumba unawakilisha maombi ya watakatifu. Kwa hivyo viumbe wanne wenye uhai pamoja na wazee ishirini na wanne wanashikila mikononi mwao yale ambayo manabii wamewahi kutabiri na yale waumini wamewahi kuombea- yote yanakaribia kutimia.

Kusudi la viumbe wanne wenye uhai pia linahusiana na kutangaza utakatifu wa Mungu na kuongoza katika ibada na kumwabudu Mungu, na wanahusika kwa njia nyingine na haki ya Mungu, kwani wakati ile lakiri ya kwanza miongoni mwa zile saba inafunguliwa na kutuma wale wapanga farasi kuharibu, sauti zao zenye nguvu kama radi zinaamuru “njoo” (Ufunuo 6:1-8). Wale wapanda farasi wanaitikia mwito wa viumbe hao wanne wenye nguvu, huku wakionyesha nguvu wanayo viumbe hao. Nguvu hiyo inaonekana tena katika Ufunuo 15:7 wakati mmoja wa viumbe wale wanne anapoachilia mapigo saba ya Mungu juu ya binadamu.

Viumbe hao wanne wenye uhai wanafanana sana, ikiwa sio sawa na viumbe katika Ezekieli sura ya 1 na 10 na Isaya 6:1-3. Ni wanne, wana macho, na nyuso kama viumbe katika Ezekieli 1:10, na wana mabawa sita (Isaya 6:2), na wanaabudu kama vile viumbe katika Isaya 6:3, wakisema, “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana.” Huenda wasiwe viumbe sawa, lakini kwa hakika wanaweza kulinganishwa na pengine ni wa mpangilio sawa.

Kwa muhtasari, viumbe hawa ni wa mpangilio uliotukuka wa malaika ambao kusudi lao la msingi ni ibada (Ufunuo 19:4). Wanafanana sana na viumbe katika Ezekieli 1 na 10 na Isaya 6:1–3, na wanahusika kwa namna nyingine katika haki ya Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, viumbe wenye uhai katika Ufunuo ni kina nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries