settings icon
share icon
Swali

Je! Vitabu vya Injili viliandikwa lini?

Jibu


Ni vyema kuelewa kwamba tarehe za kuandikwa kwa Injili na vitabu vingine vya Agano Jipya ni kisio la wasomi na katika hali mbaya ni dhanio la upumbavu. Kwa mfano, tarehe zilizopendekezwa za kuandikwa kwa Injili ya Mathayo zinaanzia mwanzo wa BK 40 hadi mwishoni mwa BK 140. Upana huu wa tarehe kutoka kwa wasomi unaonyesha hali ya kibinafsi ya mchakato wa ukadrio wa umri. Kwa ujumla, mtu atapata kwamba dhana za wasomi zinaathiri sana ukadirio wao wa kuandikwa kwa Injili.

Kwa mfano, hapo mbeleni wanatheolojia wengi wa mlengo huru wamehoji kuwa vitabu vya Agano Jipya viliandikwa tarehe ya baadaye kuliko vile inavyodhibitishwa au kuhalalishwa, kwa jaribio la kudhalilisha au kutia shaka juu ya yaliyomo na ukweli wa simlizi ya Injili. Kwa upande mwingine, kuna wasomi wengi ambao wanaangalia tarehe ya mbeleni ya uandishi wa vitabu vya Agano Jipya. Kuna wengine ambao wanaamini kuna ushahidi mzuri wa kuunga mkono maoni kwamba Agano Jipya lote, hii ikiwa ni pamoja na Ufunuo, kuwa liliandikwa kabla ya uharibifu wa Yerusalemu mnamo BK 70. Ni hoja yetu kwamba ushahidi unaunga mkono tarehe ya mbeleni zaidi kuliko kuwepo kwa Ushahidi wa tarehe ya baadaye.

Kunao wasomi ambao wanaamini kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa mapema kama miaka kumi hadi kumi na mbili baada ya kifo cha Kristo. Wale wanaoshikilia tarehe hii ya mapema ya Mathayo wanaamini aliandika Injili yake kwanza kwa Kiaramu, na baadaye ikatafsiriwa kwa Kiyunani. Mojawapo ya ushahidi wa tarehe hii ya mapema ya Injili ya Mathayo ni kwamba viongozi wa kanisa la kwanza kama vile Irenaeus, Origen, na Eusebius waliandika kwamba Mathayo aliandika Injili yake kwanza kwa waumini wa Kiyahudi wakati alikuwa bado yuko Palestina. Kwa kweli Eusebius (askofu wa Kaisaria na anayejulikana kama baba wa historia ya kanisa) alisimulia kwamba Mathayo aliandika Injili yake kabla ya kuondoka Palestina ili kuihubiri injili katika nchi zingine, ambayo Eusebius anasema kuwa ilitokea takribani miaka 12 baada ya kifo cha Kristo. Wasomi wengine wanaamini kwamba hii itaweka kuandikwa kwa Mathayo mapema kati yam waka wa BK 40-45 na baadaye BK 55.

Hata kama Injili hazikuwa zimeandikwa hadi baada ya miaka 30 baada ya kifo cha Kristo, hiyo bado itaweka kuandikiwa kwao kabla ya uharibifu wa Yerusalemu mnamo BK 70. Hii haileti shida kubwa kwa mamlaka yao au usahihi. Kupitisha mila na mafundisho ya mdomo ilikuwa kawaida katika utamaduni wa Kiyahudi wa siku hizo, na kukariri kulisisitizwa sana na kuweka katika matendo. Pia, ukweli kwamba hata wakati huo kungekuwa na idadi kubwa ya mashahidi waliokuwepo ili kupinga na kudharau madai yoyote ya uwongo, na ukweli kwamba hakuna "msemo mgumu" wa Yesu uliochukuliwa kutoka kwa simulizi ya Injili, inaunga mkono zaidi maoni yao kwa usahihi. Ingekuwa kuwa Injili ilisahihisshwa kabla ya kuandikwa, kama vile wasomi wengine huru wanavyosisitiza, basi hiyo ilikuwa kazi hafivu sana. Waandishi waliacha "misemo migumu" mingi sana, ambayo haikubaliki kitamaduni na sio simulizi sahihi kisiasa hiyo itahitaji kufafanuliwa. Mfano wa hii ni kwamba mashahidi wa kwanza wa ufufuo walikuwa wanawake, ambao hawakuchukuliwa kuwa mashahidi wa kuaminika katika utamaduni wa siku hizo.

Jambo kuu kwa Wakristo ni hili — iwe Injili iliandikwa pindi tu baada ya kifo cha Kristo, au hadi baada ya miaka 30 baada ya kifo chake, haijalishi sana, kwa sababu usahihi na mamlaka yao haitegemei wakati ziliandikwa bali juu ya kile zilivyo: Neno la Mungu lililovuviwa na Mungu (2 Timotheo 3:16). Tunapaswa pia kukumbuka kuwa moja wapo ya ahadi ambazo Yesu aliwapa wanafunzi wake ni kwamba atawatumia "msaidizi mwingine," Roho Mtakatifu, ambaye angewafundisha vitu vyote na "kuwakumbusha yote niliyowaambia" (Yohana 14: 26). Kwa hivyo, iwe ni miaka michache au mingi iliyopita baada ya kifo cha Yesu ndiposa Injili ikaandikwa, tunaweza kuwa na ujasiri kamili na imani katika ukamilifu wake na usahihi tukijua kwamba ziliandikwa na, "watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu" (2 Petro 1: 21), ambaye aliandika kwa usahihi maneno ya Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Vitabu vya Injili viliandikwa lini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries