settings icon
share icon
Swali

Je! Dini ndio sababu ya vita nyingi?

Jibu


Kwa hakika, migogoro mingi katika historia imesababishwa na dini, na dini nyingi zinahusika. Kwa mfano, katika Ukristo, yalitokea haya (kwa kutaja machache tu):

• Vita vya Kikristo — Mfululizo wa kampeni kutoka karne ya 11 hadi 13 pamoja na lengo lililowekwa la kupatanisha Nchi Takatifu kutoka kwa wavamizi wa Kiislam na kusaidia wale wa Ufalme wa Byzantine

• Vita vya Ufaransa vya Dini — Mfululizo wa vita nchini Ufaransa wakati wa karne ya 16 kati ya Wakatoliki na Waprotestanti Huguenots.

Vita vya Miaka thelathini — Vita vingine kati ya Wakatoliki na Waprotestanti wakati wa karne ya 17 katika Ujerumani.

Orodha hii sio kamilifu kabisa. Mbali na hili, unaweza kuongeza Uasi wa Taiping na Matatizo katika Ireland ya Kaskazini. Ukristo kwa kweli imekuwa sababu katika migogoro mingi katika historia yake ya miaka 2,000.

Katika Uislam, tunaona dhana ya jihadi, au "vita takatifu". Jihadi, maanaanake ni "mapambano," lakini dhana imekuwa kutumika kuelezea vita katika upanuzi na ulinzi wa eneo la Kiislamu. Vita vya

Vita ambavyo vinaendelea katika Mashariki ya Kati, zaidi ya nusu karne iliyopita hakika imechangia wazo kwamba dini ndiyo sababu ya vita vingi. Mashambulizi ya Septemba 11 huko Marekani , yameonekana kama Jihadi dhidi ya Shetani Mkuu", Marekani " ambayo kwa macho ya Kiislamu ni sawa na Ukristo. Katika Kiyahudi, vita vya ushindi viliandikwa katika Agano la Kale (hasa kitabu cha Yoshua) kwa amri ya Mungu, alishinda Nchi ya Ahadi.

Ni jambo la dhahiri kuwa dini kwa hakika imechangia katika vita vingi katika historia ya mwanadamu. Hata hivyo, je,hii inathibitisha jambo lililosemwa na wakosoaji wa dini kwamba dini yenyewe ndiyo sababu ya vita? Jibu ni "ndiyo" na "hapana." "Ndiyo" kwa maana kwamba kama sababu ya pili, dini, angalau, imesababisha mgogoro mkubwa. Hata hivyo, jibu ni "hapana" kwa maana dini sio sababu kuu ya vita.

Ili kufafanua jambo hili, hebu tuangalie karne ya 20. Kwa akaunti zote, karne ya 20 ilikuwa moja ya karne ya mauaji mengi katika historia ya binadamu. Vita mbili kuu vya dunia, ambazo hakzikua na uhusiano wowote na dini, Ukatili wa Kiyahudi, na Mapinduzi ya Kikomunisti nchini Urusi, Uchina, Kusini Magharibi mwa Asia, Cuba, wamepata kuhesabu kati ya vifo vya watu milioni 50-70 (baadhi yao wanahesabu wastani wa milioni 100 ). Kitu kimoja hizi migogoro na mauaji ya kimbari yanafanana ni kwamba ni vita hivi visababiswa na mawazo tofauti na hazikua vita vya kidini. Tunaweza kusema kuwa watu wengi wamekufa katika historia ya wanadamu kutokana na mawazo tofauti kuliko dini. Dhana ya Ukomunisti unachochea uamuzi juu ya wengine. Ile dhana ya Nazi inachochea kuondolewa kwa jamii "duni". Mawazo haya mawili peke yake yalisababisha vifo vya mamilioni, na dini haikuwa na uhusiano wowote na hilo. Kwa kweli, ukomunisti ni ufafanuzi wa itikadi amabayo haimwaini Mungu.

Dini na mawazo tofauti zote huababisha vita. Hata hivyo, sababu kuu ya vita vyote ni dhambi. Fikiria Maandiko yafuatayo:

"Ni nini kinachosababisha mapigano na migongano kati yenu? Je, si hutoka kwa tamaa zenu zinazopigana ndani yenu? Unataka kitu lakini haukipati. Unaua na unatamaa, lakini huwezi kuwa na unachotaka. Unateta na kupigana. Hauna, kwa sababu humuombi Mungu. Unapouliza, huwa hupati kwa sababu unaomba kwa nia mbaya, ili uweze kutumia kile unachopata kwenye raha zako "(Yakobo 4: 1-3).

"Kwa maana ndani ya moyo huja mawazo mabaya, mauaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushuhuda wa uongo, kunena mabaya kwa wengine" (Mathayo 15:19).

"Moyo una udanganyifu juu ya vitu vyote na huwa zaidi ya tiba. Ni nani anayeweza kuelewa? "(Yeremia 17: 9).

"BWANA akaona jinsi uovu mkubwa wa mwanadamu duniani ulivyokuwa, na kwamba kila nia ya mawazo ya moyo wake ilikuwa mabaya tu wakati wote" (Mwanzo 6: 5).

Ushahidi wa Maandiko ni upi kuhusu sababu ya msingi wa vita? Ni nyoyo zetu mbaya. Dini na itikadi ni njia tu ambayo tunatumia kutekeleza uovu katika mioyo yetu. Kufikiria, kama watu wengi wasiokuwa na imani wanaoamini kwamba, ikiwa tunaweza kuondoa "mahitaji yetu ya dini isiyo ya kawaida," tunaweza kuunda jamii ya amani kwa namna fulani, ni kuwa na mtazamo usio sahihi wa asili ya kibinadamu. Ushuhuda wa historia ya mwanadamu ni kwamba ikiwa tunauondoa dini, kitu kingine kitachukua mahali pake, na kwamba kitu hicho si kizuri kamwe. Ukweli ni kwamba dini ya kweli inadhibiti ubinadamu ulioanguka; bila hayo, uovu na dhambi utawala.

Hata kwa ushawishi wa dini ya kweli yaani Ukristo, hatuwezi kamwe kuona amani katika ezi za kisasa. Hakuna siku bila mgogoro fulani mahali fulani duniani. Tiba ya vita ni Mkuu wa Amani, Yesu Kristo! Wakati Kristo atakaporudi kama alivyoahidi, ataufunga wakati huu wa kisasa na kuanzisha amani ya milele:

"Atahukumu kati ya mataifa, na ataamua migogoro kwa watu wengi; nao watapiga mapanga yao kuwa makasu, na mikuki yao kuwa makonde ya kupogoa; taifa halitainua upanga juu ya taifa, wala hawatajifunza vita tena "(Isaya 2: 4).

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Dini ndio sababu ya vita nyingi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries