settings icon
share icon
Swali

Je, ina maana gani kuwa kutakua na vita na fununu za vita kabla ya nyakati za mwisho?

Jibu


Katika jibu lake kwa kile wanafunzi walimuuliza, "Tuambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonesha kuja kwako na mwisho wa nyakati?" (Mathayo 24:3), Yesu alijibu, "Mtasikia juu ya vita na fununu za vita" (Matahayo 24:6). Kwa sababu ya maneno ya Yesu katika kifungu hiki, kunapotokea mgogoro haswa karibu na mji wa Israeli, watu wengi huingiwa na wasiwasi wakidhani vita hizo mpya ni ishara ya nyakati za mwisho. Ikiwa tu watu watasoma Mathayo 24:6- " oneni kuwa hamjapewa onyo kwa kuwa hili ni lazima litokee, lakini mwisho wenyewe ungali bado".
Kuelewa ujumbe wa Yesu kuhusu "vita na fununu za vita" kwa kumaanisha kwamba vita ni ishara ya nyakati za mwisho ni kinyume kamili na kile ambacho anatarajia. Yesu alikua anatufundisha kwamba tusikubali vita ama fununu za vita kutupea wasiwasi, kwa sababu ' mwisho ungali bado.' Vilevile, Yesu aliongea kuhusu Wakristo wa uongo (Mathayo 24:5), njaa, na mitetemeko ya ardhi (Mathayo 24:7), na kuonya kwamba, " Yote hayo ni kama mwanzo wa maumivu ya kujifungua mtoto" (Mathayo 24:8).

Cha kusikitisha, ni kuwa kwa zile vitu zote ambazo Yesu alisema kuwa zitakua ishara ya nyakati za mwisho ndizo watu wengi haswa huchukulia kama ishara ya nyakati za mwisho. Basi, hii si kusema kwamba vita na fununu za vita hazina uhusiano na nyakati za mwisho. Wakati Biblia inazungumzia nyakati za mwisho, inaelezea kuhusu vita vikali sana. Lakini ujumbe wa Yesu unajaribu kuonyesha kwamba kumekua na vita,ipo, na itakua hadi pale atakapoleta amani katika ufalme wa milenia, kutakua na vita kila mar. Kwa hivyo, vita na fununu za vita si utabiri wa kuamini kuhusu nyakati za mwisho.

Hata ikiwa ni vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Afrika, ugomvi baina ya Israeli na majirani wake, ama vita dhidi ya ugaidi, siku hizi hakuna mgogoro ambao unaeza tabiri kuwa nyakati za mwisho ziko karibu. Hata ikue vita gani ama fununu gani za vita zinazoendelea kati yetu, huduma yetu ni moja, na inaonekana kuwa huduma hiyo ndio Yesu anasema itakua ishara halisi ya nyakati za mwisho, "Ila, kabla ya mwisho kufika, hii habari Njema ya ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote, na mwisho utawadia" ( Mathayo 24:14, inasisitiza).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ina maana gani kuwa kutakua na vita na fununu za vita kabla ya nyakati za mwisho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries