settings icon
share icon
Swali

Je, vita mbinguni katika Ufunuo 12 vinaelezea asili ya kuanguka kwa Shetani au vita vya malaika vya nyakati za mwisho?

Jibu


Vita kuu vya mwisho vya malaika na hatima ya kufukuzwa kwa Shetani kutoka mbinguni vimeelezwa katika Ufunuo 12: 7-12. Katika kifungu hiki, Yohana anaona vita kubwa ambavyo vinamkabili Mikaeli na malaika wa Mungu dhidi ya joka (Shetani) na malaika wake walioanguka au mapepo. Haya yatafanyika wakati wa mwisho, wakati wa dhiki. Shetani, katika kiburi chake kikubwa na udanganyifu kwamba anaweza kuwa kama Mungu, ataongoza uasi wa mwisho dhidi ya Mungu. Itakuwa ni ukinzano. Joka na mapepo zake watapoteza vita na kutupwa kutoka mbinguni milele.

Tunajua vita hii bado ni vya baadaye kwa sababu ya muktadha wa Ufunuo 12. Mstari wa 6 unasema kwamba mwanamke (Israeli) akakimbia kutoka kwa joka (Shetani) " akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku 1,260." Mstari wa 7 huanza kwa maneno Na kisha. Waisraeli wanapokimbia, vita vinatokea katika ulimwengu wa mbinguni. Kukimbia kwa mwanamke katika Ufunuo 12: 6 kunaambatana na wito wa Yesu kwa Wayahudi wanaoishi Yudea kuwa "kukimbilia milimani" wakati wanapoona chukizo la uharibifu (Mathayo 24:16). Katikati mwa dhiki, Mpinga Kristo ataonyesha rangi zake za kweli, Shetani atazingirwa duniani, na Israeli itahifadhiwa kwa siku 1,260 (miaka mitatu na nusu, au nusu ya pili ya dhiki).

Dhana potovu ya kawaida ni kwamba Shetani na pepo zake walikuwa wamefungwa katika Jahanamu baada ya kuanguka kwa Shetani. Ni dhahiri kutoka kwenye vifungu vingi vya Biblia kuwa Shetani hakuzuiliwa kutoka mbinguni baada ya uasi wake wa kwanza. Katika Ayubu 1: 1-2: 8, anaonekana mbele ya Mungu kumshtaki Ayubu ya kuwa na nia za kusudi katika ibada yake ya Mungu. Katika Zekaria 3, Shetani anaonekana tena mbele ya Mungu kumshtaki Yoshua, kuhani mkuu. Pia, nabii Mikaya anaelezea maono ya roho mbaya iliyosimama mbele ya Mungu katika 1 Wafalme 22: 19-22. Kwa hivyo, hata baada ya kuanguka, Shetani bado alikuwa na uwezo wa kufika mbinguni.

Katika kisasi hiki, Shetani na malaika wake bado wana uwezo ingawa finyu wa kufika mbinguni na kuwapinga malaika wa Mungu (Danieli 10: 10-14). Lakini, katika vita viliyoandikwa katika Ufunuo 12, Shetani na vijana wake watapoteza uwezo wote wa kufika mbinguni (mstari wa 8) na kuwekwa kwenye sayari hii ya ulimwengu (mstari wa 9). Uhuru wake ukipunguzwa, Shetani atajazwa "ghadhabu, kwa sababu anajua kwamba muda wake ni mfupi" (mstari wa 12).

Kutakuwa na furaha kubwa mbinguni, kwa kuwa mshtakiwa wa kale atapiwa marufuku milele kwa kuwadharau wateule. Hata hivyo, wanaoishi duniani watateseka sana baada ya tukio hili, kwa sababu ya hasira za Shetani na hukumu Mungu iliyobaki duniani.

Vita kati ya Mikaeli na Shetani vitakuwa muhimu. Wakati malaika watakatifu wa Mungu wanashinda vikosi vya pepo, sauti kubwa mbinguni inasema, "Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu,

na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake "(Ufunuo 12:10). Watakatifu wa Mungu watashiriki katika ushindi huo pia: " Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao" (mstari wa 11).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, vita mbinguni katika Ufunuo 12 vinaelezea asili ya kuanguka kwa Shetani au vita vya malaika vya nyakati za mwisho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries