settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu vita?

Jibu


Watu wengi wanafanya makosa kwa kusoma chenye Bibilia inasema katika Kutoka 20:13, “Usiue” na wanatafuta kutumia amri hii katika vita. Ingawa, neno la Kiibrania katika maan ya juu juu lamaanisha, “ mauaji yaliyodhamiriwa kimataifa na mtu mwingine kwa uovu; uuaji.” Mungu kila mara aliamrisha Waisraeli kuenda vitani na mataifa meningine (1 Samweli 15:3; Yoshua 4:13). Mungu aliamrisha hukumu ya kifo kwa maovu mbali mbali (Kutoka 21:12; 15; 22:19; Mambo Ya Nyakati 20:11). Kwa hivyo Mungu hayuko kinyume na mauaji katika hali zote, lakini ile tu ya uuaji. Vita kamwe si kitu kizuri, lakini wakati mwingine ni jambo la lazima. Katika taifa ambalo limejawa na watu waovu (Warumi 3:10-18), vita ni lazima. Wakati mwingine njia peke ya kuwazuia watu waovu kutoka kuendelea kutenda uovu kwa wenye hawana habari ni kuenda vita.

Katika Agano La Kale, Mungu aliamrisha Waisraeli “walipize kisasi wana wa Israeli juu ya Wamidiani; kisha baadaye utakusanywa uwe pamoja na watu wako” (Hesabu 31:2). Kumbukumbu La Torati 20:16-17 yasema, “ Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo BWANA, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu cho chote kupumzikacho; lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperezi, na Mhivi, na Myebusi, kama alivokuamuru BWANA, Mungu wako.” Pia 1 Samweli 15: 18 yasema, “Kisha BWANA akakutuma safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hata watakapoangamia.” Kawaida Mungu hapingi vita vyote. Yesu kila mara amekubaliana kikamilifu na Baba (Yohana 10:30), kwa hivyo hatuwezi kupishana kuwa vita vilikuwa mapenzi ya Mungu peke katika Agano La Kale. Mungu habadiliki (Malaki 3:6; Yakobo 1:17).

Katika kurudi kwa Yesu mara ya pili kutakuwa kwa mchafuko. Ufunuo 19:11-21 waelezea vita vya mwisho na Kristo, amri jeshi mkuu ambaye atahukumu na kufanya vita “kwa haki” (aya ya 11). Kutakuwa na umwagikaji wa damu (aya ya 13) na ukatili. Ndege wa anga watakula miili ya wale waliompinga (aya ya 17-18). Hatakuwa na huruma kwa maadui wake, ambao atawashinda kabisa na kuwatupa katika “ siwa la moto uchomao” (aya ya 20).

Ni makosa kusema kuwa Mungu kamwe haungi vita mkono. Yesu si mpinzani vita. Katika ulimwengu umejaa watu waovu, wakati mwingine vita vinahitajika ili uzuie maovu zaidi. Kama Hitler hangeshindwa katika vita vya dunia vya II, ni mamilioni ngapi ya watu wangeuwawa? Kama vita vya kimarekani vya raia havikupiganwa, ni muda mgani Wamarekani-Waafrika wangetezeka katika utumwa?

Ni kitu kiovu namna gani. Vita vingine ni vya “ haki” kuliko vingine, lakini vita kawaida ni kwa mjibu wa dhambi (Warumi 3:10-18). Kwa wakati huo huo, Mhubiri 3:8 yasema, “Kuna wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.” Katika ulimwengu ambao umejawa na dhambi, chuki na uovu (Warumi 3:10-18), vita ni lazima. Wakristo wasithami vita, vilevile Wakristo hawastahili kupinga serikali ambayo Mungu ameiweka madarakani juu yao (Warumi 13:1-4; 1 Petero 2:17). Kitu cha maana tunaweza kufanya kwa kufanya wakati wa vita ni kuomba kwa hekima ya Mungu kwa viongozi wetu, kuombea usalama kwa wanajeshi wetu, kuombea suluhisho la haraka kwa mgogoro, na kuombea majeraha kwa raia wa pande zote mbili (Wafilipi 4:6-7).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu vita?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries