settings icon
share icon
Swali

Je, Biblia inasema nini kuhusu uzinzi? Je, Mungu atasamehe mzinzi?

Jibu


Uzinzi mara nyingi hujulikana kama "taaluma ya kale zaidi." Hakika, daima imekuwa njia ya wanawake kupata pesa, hata wakati wa Biblia. Biblia inatuambia kwamba uzinzi ni usherati. Methali 23: 27-28 inasema, "Kwa maana kahaba ni shimo refu, na Malaya ni rima jembamba. Naam, huotea kama mnyang'anyi ; na kuwaongeza wenye hila katika wanadamu."

Mungu anakataza kushirikiana na makahaba kwa sababu anajua kuhusika kama hiyo kuna madhara kwa wanaume na wanawake. "Kwa maana midomo ya mwanamke mwovu hudondoza asali, na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; lakini mwisho wake huwa machungu kuliko pakanga, ni mkali kama upanga wa makali kuwili. Miguu yake inateremkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu"(Mithali 5: 3-5 NKJV).

Uzinzi h uharibu ndoa, familia, na maisha tu, lakini huharibu roho na roho kwa njia inayosababisha kifo cha kimwili na kiroho. Mungu anatamani kwamba tuwe bila hatia na tutumie miili yetu kama zana za matumizi na utukufu wake (Warumi 6:13). Wakorintho wa kwanza 6:13 inasema, "Mwili sio kwa uzinzi bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili."

Ingawa uzinzi ni dhambi, makahaba hawajazidi upeo wa Mungu wa msamaha. Biblia inaonyesha matumizi yake ya kahaba aitwaye Rahabu ili kuendelea na kutimiza mpango wake. Kwa sababu yakutii kwake, yeye na familia yake walitunukiwa na kupewa baraka (Yoshua 2: 1; 6: 17-25). Katika Agano Jipya, mwanamke ambaye alikuwa anajulikana kwa kufanya izinzi-kabla ya Yesu kumsamehe na kumtakasa kutoka kwa dhambi-alipata nafasi ya kumtumikia Yesu wakati alipokuwa akitembelea nyumbani mwa Mfarisayo. Mwanamke, alipomtambua Kristo,yeye alileta chupa ya mafuta ya gharama kubwa kwake. Kwa kusikitisha na toba, mwanamke alilia na akamwaga ubani juu ya miguu Yake, akaifuta kwa nywele zake. Wakati ambapo Mafarisayo alimshtumu Yesu kwa kukubali tendo hili la upendo kutoka kwa "mwanamke" wa kiasherati, aliwaonya na kukubali ibada ya mwanamke. Kwa sababu ya imani yake, Kristo alikuwa amesamehe dhambi zake zote, naye akapokewa katika ufalme Wake (Luka 7: 36-50).

Akizungumzia na wale waliokataa kuamini ukweli kuhusu Yeye mwenyewe, Yesu Kristo alisema, "Nawaambieni kweli, watoza ushuru na makahaba wanaingia katika ufalme wa Mungu mbele yenu.Kwa kuwa Yohana alikuja kwenu kuwaonyesha njia ya haki, lakini hamkumwamini, lakini watoza ushuru na makahaba walifanya hivyo, na hata baada ya kuona hayo, hamkutubu na kumwamini "(Mathayo 21: 31-32).

Kama vile mtu mwingine yeyote, makahaba wana nafasi ya kupokea wokovu na uzima wa milele kutoka kwa Mungu, kutakaswa kwa uovu wao wote na kupewa maisha mapya! Wanayopaswa kufanya ni kugeuka kutoka kwa maisha yao ya dhambi na kugeuka kwa Mungu aliye hai, ambaye neema yake na huruma hazina kipimo. "Kwa hiyo, ikiwa mtu yupo ndani ya Kristo, yeye ni kiumbe kipya, ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya!" (2 Wakorintho 5:17).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Biblia inasema nini kuhusu uzinzi? Je, Mungu atasamehe mzinzi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries