settings icon
share icon
Swali

Biblia inasemaje kuhusu kupanga wa uzazi?

Jibu


Mpango wa uzazi ni utaratibu wa kudhibiti idadi ya watoto watakaozaliwa katika familia, ikiwa ni pamoja na kudhibiti idadi ya miaka kati ya kuzaa, kwa njia ya mpango wa uzazi bandia, kutozaa kwa hiari, tiba ya utasa usio wa kujitakia, upangaji wa uzazi wa asili , au njia nyingine ya kuzuia au kuhamasisha mimba. Sababu za kutamani aina hizi ya udhibiti hutofautiana kutoka kwa familia moja hadi familia nyingine na inaweza kuathiriwa na sababu nyingi, kama vile uchaguzi wa kazi, masuala ya uhusiano, hali ya kifedha, ulemavu wa kimwili, hali ya maisha, nk.

Kwa kuwa upangaji wa uzazi wa kisasa haukuwepo wakati wa kibiblia, Biblia haijaguzia jambo hilo la kutumia mbinu hizi kuzuia au kuhamasisha mimba. Kuzuia mimba kwa madhumuni ya kupanga uzazi, iwe kwa muda au iwe ya kudumu, ni tendo ambalo haionekani kuwa ni dhambi. Uchaguzi wa matibabu ya uzazi vili vile sio dhambi. Hata hivyo, mume na mke wanapaswa kukubaliana juu ya maamuzi yoyote kuhusu watoto wa baadaye.

Ingawa hakuna chochote kibaya na wanandoa wanaopanga maisha ya baadaye ya familia zao, wanapaswa kukubali kwamba mapenzi ya Mungu hayawezi kuharibiwa. Hakuna chochote katika Biblia kinachosema kila wanandoa wanapaswa kuwa na watoto, lakini ukuu wa Mungu unapita mipango ya wanandoa, haijalishi tahadhari wanatakayochukua. Methali 16: 9 inasema, "Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake." Ikiwa mapenzi ya Mungu ni kumleta mtoto katika maisha ya wanandoa, jitihada za kuzuia mimba hazitazuia njia yake. Ikiwa wanandoa wanafanya ngono, bila mpango wa uzazi lazima wawe tayari kwa uwezekano wa ujauzito.

Ikiwa mwanamke anakuwa mjamzito bila kutarajia au bila kutaka, ujauzito unapaswa kuruhusiwa kutimia wakati wake. Utoaji mimba au Mipango ya Uzazi wa Dharura haikubaliki kama njia ya kupanga uzazi kwa sababu utoaji mimba na kidonge cha asubuhi hufanyakazi baada ya kushika mimba, na kusababisha kifo cha mwanadamu aliye hai. Mungu anajua kila mtu kabla ya uumbaji wake na kwa upendo anapanga mwili ndani ya tumbo (Yeremia 1: 5; Zaburi 139: 13-16). Chaguzi nyingi, ikiwa ni pamoja na kukabidhi mtoto kwa wazazi walezi, zinapatikana kwa wale ambao hawataki kuweka mtoto.

Watoto ni zawadi kutoka kwa Bwana (Zaburi 127: 3-4), lakini huwaletea wazazi wajibu mkubwa. Ikiwa wanandoa wanaamua kuwa hawako tayari kuwa na watoto au wangependa kudhibiti ushikaji mimba, huo ni uamuzi wao wa kufanya. Kwa njia ya maombi na majadiliano, mume na mke wanaweza kwa hekima kupanga mipango yao ya baadaye na watoto wa baadaye ambao Mungu atawabariki nao (Mithali 16: 3; 21: 5; Yakobo 1: 5).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasemaje kuhusu kupanga wa uzazi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries