settings icon
share icon
Swali

Mtazamo wa Wakristo ni upi kuhusu uvutaji? Uvutaji ni dhambi?

Jibu


Bibilia moja kwa moja hiataji uvutaji sigara. Kuna misimamo, hata hivyo inayoweza kutumika kwa uvutaji. Kwanza, Bibilia inatuamuru kuwa tusihiruhusu miili yetu “itawaliwe” na kitu cho chote. “Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote” (1 Wakorintho 6:12). Uvutaji bila kukana ni mazoea. Baadaye kwa ujumbe huo huo tumeambiwa, “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu” (1 Wakorintho 6:19-20). Uvutaji bila shaka unadhuru afya yako. Uvutaji umethibitishwa kuwa unaharibu mapafu na moyo.

Uvutaji unaweza kuhesibiwa kuwa wa “manufaa” (1 Wakorintho 6:12)? Inawezwa semwa kuwa uvutaji ni kumheshimu Mungu na mwili wako (1 Wakorontho 6:20)? Mtu anaweza kuvuta kwa kweli “kwa utufuku wa Mungu” (1 Wakorintho 10:31)? Tunaamini kuwa jawabu kwa maswali haya matatu ni “la.” Kwa sababu hiyo, tunaamini kuwa uvutaji ni dhambi na kwa hivyo husiwahi fanywa na wafuasi wa Yesu Kristo.

Wengine hushindana na mtazamo huu kwa kuelekezea hoja kuwa watu wengi hula vyakula ambavyo si vizuri kwa afya yao, ambayo inaweza kuwa mazoea na hivyo kuwa mbaya kwa mwili. Kwa mfano, watu wengi bila uwezo wa kujisaidia wamevutwa na mazoea ya uvutaji kafeini hadi hawawezi fanya kazi bila kikombe cha kahawa asubuhi. Hii ikiwa kweli, ni namna gani uvutaji unaweza kuwa sawa? Ni ushindani wetu kuwa Wakristo lazima wajiepushe na ulafi na ulaji kupita kiasi ambacho unadhuru afya. Naam, Wakristo mara nyingi ni wanafiki kwa kushutumu dhambi moja na kuikubali nyingine, lakini tena hii haifanyi uvutaji kumweshimu Mungu.

Hoja nyingine kinyume na mtazamo wa uvutaji ni kwamba watu wengi wa Mungu wamekuwa wavutaji wakati mmoja kama vile mhubiri mashuhuri wa Uingereza C.H. Spurgeon, aliyejulikana kwa kuvuta sigara. Pia hatuamini hoja hii kuwa inabeba uzito wowote. Tunaamini Spurgeon alifanya makosa kwa kuvuta. Vinginevyo alikuwa mtu wa Mungu na mwalimu mzuri wa neno la Mungu? Kamwe! Hiyo inayafanya matendo yake na mazoea yake kumweshimiu Mungu? La.

Kwa kutaja kuwa uvutaji ni dhambi, hatumaanishi kuwa wavutaji wote hawajaokoka. Kuna waumini wengi wa kweli katika Kristo ambao huvuta. Uvutaji haumzui mtu kuokoka. Ama kumfanya mtu kuupoteza wokovu wake. Uvutaji unasemehewa sawa na vile dhambi zingine, hata kama mtu atakuwa Mkristo au Mkristo akiri dhambi zake kwa Mungu (1 Yohana 1:9). Wakati huo huo, tunaamini kwa udi na ufumba kwamba uvutaji ni dhambi ambayo tunastahili kuiacha na kwa usaidizi wa Mungu tuushinde.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mtazamo wa Wakristo ni upi kuhusu uvutaji? Uvutaji ni dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries