settings icon
share icon
Swali

Je, uumbaji na mageuzi huathiri jinsi mtu anavyoutizama ulimwengu?

Jibu


Tofauti muhimu kati ya uumbaji na mageuzi huja chini ya uhakika wetu juu ya kila kitu tunachofikiri tunajua. Fikiria juu yake: kama hisia zetu tano na akili zetu ni mageuzi tu ya ghafla, yasiyo na maana, tunawezaje kuwa na hakika kwamba zinatupa taarifa ya kuaminika? Kitu ambacho jicho langu na ubongo unaona kama "nyekundu" kinaweza kuonekana kwa jicho lako na ubongo kuwa cha rangi ya "samawati," lakini unakiita "chekundu" kwa sababu ndivyo ulivyofundishwa. (Rangi zenyewe hazitabadilika, kwa kuwa zinajumuisha mizunguko fulani, isiyobadilika ya wigo wa umeme.) Hatuna njia ya uhakika ya kujua kama tunaongea juu ya kitu kimoja.

Au tuseme umeona mwamba ambao ulionekana kuwa na mchoro juu yake unaosomeka "Chicago: maili 50." Sasa pia tuseme unaamini kuwa alama hizo sio kweli lakini matokeo ya mmomonyoko wa ghafula kutoka kwa upepo na mvua ambazo huonekana kueneza na kuchora ujumbe huu. Je, unaweza kuwa na imani yoyote kwamba Chicago kweli ii mbaili maili 50?

Lakini sembuze kama ulijua kwamba kila seti ya kawaida ya macho na akili imeundwa kutambua mzunguko fulani wa wigo wa umeme kama "nyekundu"? Kisha unaweza kuwa na ujasiri katika kujua kwamba kile ninachokiona kama nyekundu ni kile unachokiona kama chekundu. Na sembuze ungejua kwamba mtu alikuwa amepima umbali wa maili 50 kutoka Chicago na kisha akaweka alama hapa ili kuonyesha hiyo? Basi, unaweza kuwa na uhakika kwamba alama hiyo inakupa maelezo sahihi.

Tofauti nyingine katika jinsi uumbaji na mageuzi huathiri mtazamo wa mtu wa ulimwengu ni katika hali ya maadili. Ikiwa sisi ni bidhaa tu za mageuzi ya ghafula, isiyo na maana, ni nini hasa maana usahihi ya maneno "nzuri" na "mabaya"? "Nzuri" ikilinganishwa na nini? "Uovu" ukilinganishwa na nini? Hakika, bila mizani ya kupimia (k.m., hali ya Mungu), hatuna msingi wa kusema kwamba kitu ni nzuri au mabaya; ni maoni tu, ambayo haina uzito wa kuhukumu jinsi ninavyofanya au jinsi ninavyohukumu matendo ya wengine. Mama Teresa na Stalin walifanya tu uchaguzi tofauti katika ulimwengu kama huo. Hakuna jibu adilifu "Fulani alisema?" tunapokuja kwa suala la kuamua haki na mbaya. Na wakati watu wasiokuwa na imani na wasioamini wanaweza kuongoza maisha maadili — ikiwa ni kweli kwa imani zao hawana sababu — wala hawana msingi wowote wa kuhukumu hatua za wale wanaoamua kuwa wamefanya kitu "kibaya."

Lakini kama kuna Mungu ambaye alituumba kwa mfano wake, basi hatujaumbwa na hisia tu pekee ya kile kilicho sawa au kibaya, lakini pia tuna jibu la kusema ni "nani?" Nzuri ni kile kinachohusiana na asili ya Mungu, na uovu ni chochote ambacho hakifai.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, uumbaji na mageuzi huathiri jinsi mtu anavyoutizama ulimwengu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries