settings icon
share icon
Swali

Je! Inamaanisha nini kuwa Wakristo wametwaliwa na Mungu?

Jibu


Kuasili mtu ni kumfanya mtu huyo kuwa mwana au binti kisheria. Uasili/utwalizi ni moja wapo ya sitiari zilitumika katika Biblia kuelezea jinsi Wakristo wameletwa katika familia ya Mungu. Yesu alikuja "ili tupate kupokea zile haki kamili za kufanywa watoto wa Mungu" (Wagalatia 4:5), na alifanikiwa kufanya hivyo: "mlipokea roho ya kufanywa wana" (Warumi 8:15).

Biblia pia inatuma sitiari ya "kuzaliwa mara ya pili" kwa familia ya Mungu (Yohana 3:3), ambayo inaonekana kuitilafiana na dhana ya utwalizi kwa sababu, kawaida, aidha mtu amezaliwa kwa familia au kuasiliwa na sio zote mbili kwa wakati mmoja. Hatupaswi kusema mengi juu ya tofauti zao, walakini, kwa sababu ya dhana hizi ni sitiari na hasipazwi kutumika moja dhidi ya nyingine.

Uasili haukuwa jambo la kawaida katika ulimwengu wa Wayahudi. Hadhi ya mtu ilikuwa kwa misingi ya uzao. Hii ndiyo sababu, iwapo mme amekufa, kakaye mdogo angemrithi mjane. Kijana wa kwanza wa kiume angezaliwa katika ndoa hiyo mpya kisheria angechukuliwa mwana wa hayati ili kizazi chake kiendelee. Hakukuwa na wazo la mjane kuasili mwana wa kiume ili aendeleze uzao wa familia. Katika Yohana 3, Yesu anazungumza naye Nikodemu, kiongozi wa Kiyahudi, na alitumia dhana ya Kiyahudi ya kuzaliwa upya (uzao wa mbinguni) kuelezea jinsi mtu analetwa katika familia ya Mungu.

Katika ulimwengu wa Kirumi, kuasili kulikuwa muhimu na utamaduni wa kawaida. Hii leo tunaweza kuandika wosia na kuacha utajiri na mali yetu kwa mtu yeyote tunayempendelea awe wa kiume au kike. Katika ulimwengu wa Kirumi, kukiwa na upekee chache, mwanaume angerithisha mali yake kwa wanawe wa kiume. Ikiwa mtu hakuwa na wana wa kiume, au kuhisi wanawe wakiume hawakuwa na uwezo kusimami mali yake vyema au hawakufaa, angeweza kumwasili mwana ambaye atakuwa wa kufaa. Uasili huu haukuwa wa watoto wachanga vile ilivyo kawaida hii leo. Watoto wa makamu na watu wazima mara nyingi walikuwa wanaasiliwa. Wakati uasili ulikuwa umekubalika kisheria, aliyeasiliwa madeni yake yote yangefutwa na kupewa jina mpya. Na sasa angekuwa mwana kamili wa kisheria wa baba aliyemwasili na kupokea haki zote faida za kuwa mwana. Baba angemkana mwanawe wa uzao, lakini uasili haungebatilizwa baada ya kufanyika.

Paulo akiwaandikia Warumi, anatumia sitiari ya uasili, ambayo wasikilizaji wangeelewa. Wagalatia 4:3-7 inasema, "Vivyo hivyo na sisi, tulipokuwa bado watoto wadogo, tulikuwa utumwani chini ya taratibu za kawaida za ulimwengu. Lakini ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe, ambaye alizaliwa na mwanamke, akazaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, ili tupate kupokea zile haki kamili za kufanywa watoto wa Mungu. Kwa sababu ninyi ni watoto wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, anayelia, "Abba, Baba." Kwa hiyo, wewe si mtumwa tena, bali ni mtoto, kwa kuwa wewe ni mtoto, Mungu amekufanya wewe pia kuwa mrithi kwa kupitia Kristo." Katika kifungu hiki, Wakristo wamezaliwa wakiwa watumwa, lakini Yesu anawanunua toka utumwani na kuasiliwa na Baba na kujazwa Roho na sasa wao ni warithi.

Wengi wamepinga lugha ambayo inatumia "wana wa kiume" katika kurejelea utwalizi wetu. Je! sembuze binti? Katika ulimwengu wa Kirumi, binti hawangepokea urithi. Paulo akiwaandikia waumini waume na wanawake, anasema kuwa jinsia zote zimeasiliwa na kupokea haki zote za kisheria wana wa kiume wamepokea. Badala ya kudunisha hadhi ya wanawake, maneno haya yanainua. Mwanamke huenda asiweze kuwa mrithi wa baba wa Kirumi, lakini mwanamke muumini ni mrithi wa Mungu.

Tunapokuja kwa Imani katika Kristo, deni zetu zinafutiliwa mbali, tunapewa jina mpya, na tunapewa haki zote ambazo warithi wa Mungu wanamiliki. Tofauti moja kutoka uasili wa Kirumi ni kwamba Wakristo hawatwaliwi kwa sababu Mungu anafikiria kuwa hawatakuwa warithi wema. Mungu anaasili watu ambao sio wa dhamani, kwa sababu Anaasili kwa misingi ya neema Yake.

Kwa hivyo, Wakristo wamezaliwa kwa familia ya Mungu (akitumia sitiari ya Kiyahudi) na kuasiliwa kwa familia ya Mungu (akitumia sitiari ya Kirumi). Matokeo ya mwisho ni sawia; Wakristo kamwe ni sehemu ya familia ya Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Inamaanisha nini kuwa Wakristo wametwaliwa na Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries