settings icon
share icon
Swali

Utume wa kanisa unafaa kuwa upi?

Jibu


Kanisa ni uumbaji wa Mungu ( Matendo ya mitume 20:28; 1Wakorintho 3:9,17; 15:9), iliyojengwa na kumilikiwa na Yesu Kristo- "Nitalijenga kanisa langu" (Mathayo 16:18) ambalo litaongozwa na kupewa nguvu kupitia na Roho Mtakatifu (1Wakorintho 10:17; 12:5-27; Warumi 12:4-5).Kwa hivyo, ni furaha ya kanisa kumtegemea Mungu ili kuonyesha mpango na utumwa kwa kanisa. Utume wa Mungu kwa kanisa unadhibitisha kuwa na sehemu mbalimbali.

1. Utume wa kanisa ni kutengeneza wanafunzi: Kabla ya Yesu kuenda mbinguni, aliambia wanafunzi wake hivi: " Nendeni basi mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote, naam, mpaka mwisho wa nyakati" ( Mathayo 28:19-20). Mwanafunzi ni mfuasi ambaye amejitolea kwa mkuu wake. Kwa hivyo huwa tunafikiria kwamba Yesu alituma kanisa lijulishe watu kumhusu kila mahali. Jinsi kanisa linatengeneza wanafunzi, watu wanaeza tamani kumuabudu, kumwamini,kumfuata na kumheshimu Yesu kama Mwokozi na Bwana wao. Wanachama wa kanisa wakiwa wamependezwa na Yesu Kristo huwa wanamzunguka kama Bwana, Kiongozi, Mwokozi na Rafiki yao. Utumwa wetu ni kumtambulisha kwa kila taifa.

2. Utume wa kanisa ni kumtukuza Kristo. Paulo aliandika, " na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake, nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu ( Waefeso 1:11-12). Lengo la Mungu kwa kanisa ni kumuinua Yesu Kristo kupitia jinsi kanisa linaishi na kenye linafanya. Kristo alijenga kanisa lake liwakileshe miuujiza, na kazi yake ya kuokoa maisha kwa ulimwengu. Katika kanisa lake, Kristo anaonyesha ulimwengu jinsi watu ambao wako huru na wamesamehewa vile wako, yani watu ambao wametosheka na Mungu kwa sababu ya furaha ya Kristo na ushindi kwa kujitoa kama dhabihu. Amepanga maadili ya kanisa kuwa maadili yake na anatarajia mienendo yake ionyeshe tabia yake( 2Wakorintho 6:14-7:1; Waefeso 5:23-32; Wakolosai 1:13, 18; 1Timotheo 3:15). Jinsi vile mwezi huonyesha jua, hivyo hivyo kanisa linafaa kuonyesha utukufu wa Mungu kwa dunia iliyo kwenye giza.

3. Utume wa kanisa ni kutengeneza walio watakatifu: Kanisa linafaa kuwahimiza na kuwatia moyo wanachama wake (1Wathesoloniki 5: 11; 2Wakorintho 13:11). "kusiweko na utengano katika mwili, bali viuongo vyote vishughulikiane" (1 Wakorintho 12:25). Yesu ndiye jiwe la pembeni kuu, na kanisa limefananishwa na nyumba " katika yeye ninyi pia mnajengwa pamoja ili mpate kuwa makao ambamo Mungu anaisi kwa njia ya Roho wake" ( Waefeso 2;19-22; pia soma 4:4-25). Yesu Kristo alijenga kanisa lake lionyeshe familia ya Mungu duniani ili wale ambao hawajampata Mungu waone jinsi Mungu anajenga familia yake ndani ya Yesu Kristo na jinsi familia iyo inahudumiana ( Mariko 3:35 na Yohana 13:35).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Utume wa kanisa unafaa kuwa upi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries