settings icon
share icon
Swali

Je, Biblia inasema nini kuhusu kupata utulifu na amani ya kiakili?

Jibu


Watu wengi huelezea "utulifu na amani ya kiakili" kuwa kukosa mawazo ya kiakili na kutokuwa na utulifu. Nyakati tu ilio sawa na "utulifu na amani ya kiakili" inapatikana katika Biblia kwenye 2 Wakorintho 2:13 ambapo Paulo anasema hakuwahi pata "utulifu na amani ya kiakili" kwa sababu hakumpata Tito katika mji wa Troas. Tafsiri kamilifu vifungu hivi ni "utulifu wa roho yangu."

Biblia inatumia neno amani kwa namna nyingi tofauti tofauti. Amani wakati mwingine inarejelea uhusiano baina ya Mungu na mwanadamu. Amani hii baina ya Mungu mtakatifu na mwanadamu mtenda dhambi imeathirika kwa dhabihu ya kifo ya Kristo, "kufanya amani kwa damu ya msalaba wake" (Wakolosai 1:20). licha ya hayo, kama Kuhani Mkuu Bwana Yesu anahimiza kwamba hali ya urafiki kwa niaba ya wote "wamjiao Mungu kwa yeye,maana yu hai sikuzote ili awaombee" (Waebrania 7:25). Hii hali ya urafiki na Mungu ni muhimu kwa aina nyingine ya amani, ambayo wakati mwingine inahusu akili tulivu. "Tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo" (Waroma 5: 1) wakati tu tunaweza kupata amani ya kweli ya akili ambayo ni zao ya Roho Mtakatifu, ina maana, mazao yake yaliyodhihirishwa ndani yetu (Wagalatia 5: 22-23).

Isaya 26: 3 inatuhimiza kuwa Mungu atatulinda katika "amani iliyo kamilifu" iwapo akili zetu zitazalia kwake, kumaanisha akili zetu zinamtegemee Yeye, zimlenge Yeye, na kumtumainia Yeye. Utulivu wa akili zetu ni "kamilifu" au pungufu kufikia kiwango ambacho akili inazalia kwa Mungu badala ya sisi wenyewe au kwa shida zetu. Amani inapatikana tunapoamini kile Biblia inachosema kuhusu jinsi Mungu alivyo karibu kama ilivyo katika Zaburi 139: 1-12, na kuhusu wema wake na uwezo, rehema na mapenzi yake kwa wanawe, na utawala wake kamili kwa hali zote za kimaisha. Ila hatutamwamini tusiyemjua, hivyo ni muhimu, tumjue vyema Mwana wa Amani, Yesu Kristo.

Amani inapatikana kwa mujibu wa maombi. "Msijisumbue kwa neno lolote bali katika kila neno kwa kusali na kuomba,pamoja na kushukuru,haja znu na zijulikane na Mungu; na amani ya Mungu ipitayo akili zote,itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu"(Wafilipi 4: 6-7).

Akili na moyo wa amani unapatikana kwa mujibu wa na kutambua kuwa Baba mwenye busara na mwenye upendo ana lengo la kipekee katika majaribio yetu. "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema wale walioitwa kwa kusudi lake" (Warumi 8:28).

Mungu huleta vitu vyema aina tofauti tofauti, kama vile amani, kutokana na matatizo tupatayo. Hata nidhamu na hukumu ya Bwana "itatoa mazao ya amani ya haki" katika maisha yetu (Waebrania 12:11). Wanatoa fursa mpya kwa "kumtumainia Mungu" na hatimaye "kumtukuza" (Zaburi 43: 5). Wanatusaidia "kuwafariji" wengine wanapojaribiwa vile vile (2 Wakorintho 1: 4), na "hufikia utukufu wa milele kwa niaba yetu ambao unawazidi wote" (2 Wakorintho 4:17).

Amani ya akili na utulivu wa roho inayoambatana nayo hupatikana tu pindi tunapokuwa na amani ya kweli na Mungu kwa njia ya dhabihu ya Kristo msalabani kwa malipo ya dhambi zetu. Wale wanaojaribu kupata amani katika vitendo vya kidunia watajipata wamekwisha danganywa. Kwa Wakristo, hata hivyo, amani ya akili inapatikana kupitia kwa ujuzi wa kipekee, na kumwamini kikamilifu, Mungu ambaye "atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu" (Wafilipi 4:19).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Biblia inasema nini kuhusu kupata utulifu na amani ya kiakili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries