settings icon
share icon
Swali

Je, Utukufu wa Shekinah ni nini?

Jibu


Neno Shekinah halionekani katika Biblia, lakini dhana inaeleweka wazi. Rabi wa Kiyahudi walitunga maneno haya ya ziada ya kibiblia, fomu ya neno la Kiebrania ambalo hasa linamaanisha "yeye alisababisha kukaa," ikiashiria kwamba ilikuwa ni kutembelewa wa Kimungu wa uwepo au makao ya Bwana Mungu duniani. Shekinah ilikuwa dhahiri kwanza wakati Waisraeli walipoondoka kutoka Sukothi katika kutoroka kwao kutoka Misri. Huko Bwana alionekana katika nguzo ya mawingu mchana na nguzo ya moto usiku: "Nao wakasafiri kutoka Sukothi, wakapiga kambi Ethamu, kwenye mpaka wa ile jangwa. BWANA naye akawatangulia mchana ndani ya wingu mfano wa nguzo, ili kuwapa nuru; wapate kusafiri mchana na usiku"(Kutoka 13:20-22).

Mungu aliongea na Musa nje ya nguzo ya wingu katika Kutoka 33, akimhakikishia kuwa uwepo Wake ungekuwa pamoja na Waisraeli (mstari wa 9). Mstari wa 11 unasema Mungu aliongea na Musa "uso kwa uso" nje ya wingu, lakini wakati Musa alipoomba kuona utukufu wa Mungu, Mungu akamwambia, "Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi"(mstari wa 20). Hivyo, inaonekana, udhihirisho unaoonekana wa utukufu wa Mungu ulikuwa hafifu kwa kiasi fulani. Wakati Musa alipouliza kuona utukufu wa Mungu, Mungu alimficha Musa katika ufa wa mwamba, akamfunika na mkono Wake, na akapita. Kisha akaondoa mkono Wake, na Musa akaona tu mgongo Wake. Hii inaonekana kuonyesha kwamba utukufu wa Mungu ni wa heshima kuu na mwenye nguvu kuonekana kabisa na mwanadamu.

Udhihirisho ulioonekana wa uwepo wa Mungu ulionekana sio tu na Waisraeli bali pia na Wamisri: "Ikaw katika zamu ya alfajiri, BWANA akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri. Akayaondoa magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa uzito; na Wamisri wakasema, Na tukimbie mbele ya Israeli; kwa kuwa BWANA anawapigania, kinyume cha Wamisri"(Kutoka 14:24-25). Uwepo tu wa utukufu wa Shekinah ya Mungu ulikuwa wa kutosha kuwashawishi adui Zake kuwa hakuwa mtu wa kupingwa.

Katika Agano Jipya, Yesu Kristo ndiye makao ya utukufu wa Mungu. Wakolosai 2:9 inatuambia kwamba "maana katika Kristo utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili," na kumfanya Yesu kutamka ghafla kwa Filipo, "Aliyeniona mimi amemwona Baba" (Yohana 14:9). Katika Kristo, tunaona udhihirisho unaoonekana wa Mungu Mwenyewe katika mtu wa pili wa Utatu. Ingawa utukufu Wake pia ulifunikwa, hata hivyo Yesu ni uwepo wa Mungu duniani. Kama vile uwepo wa Mungu ulikaa ndani ya hema ya wazi inayoitwa "hema takatifu" mbele ya Hekalu katika Yerusalemu lilijengwa, hivyo uwep ulikaa ndani ya mtu mwepesi ambaye alikuwa Yesu. "... Yeye hana umbo wala uzuri; na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani" (Isaya 53:2). Lakini tunapoingia mbinguni, tutawaona wote Mwana na Baba katika utukufu wao wote, na shekinah haitafunikwa tena (1 Yohana 3:2).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Utukufu wa Shekinah ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries